Mambo ya kuzingatia uwapo safarini


Kunakitu hata siwaelewi wasichana/Wanawake?
Hivi unasafiri safari ya zaidi ya masaa matatu, kwa nini usivae pedi kabisa kwani inakupunguzia nini?
Naona mambo mengine ni kujidhalilisha tu kwa kukosa maarifa
 

Na ikiwa inaita hapokei anaiacha kidogo ichanganye mpate ladha [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Jifunze kusema Asante siyo kila kitu unachopewa na abiria mwenzako iwe kinywaji/chakula unakula tu kwani wengine siyo abiria ni wezi ukila/kunywa ukasinzia imekula kwako.



Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 

[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Hii sio chai kweli
 
Aisee juzi kati nimetoka zangu dodoma narudi dar si nikasema ngoja niende kukata tiketi ya Bm maana ndio gari mara nyingi natumia nikienda zangu dom kwenye mambo yangu sasa nikachelewa ilikuwa kama saa kumi hivi jioni ikabidi nivizie gari za kutoka mwanza aisee nikapanda Isamilo Mungu wangu sirudiii tena panda ilo gari au hayo magari ya kutoka mwanza wasukuma jaman jamani nimepanda gari wamejaaa wasukuma tupu alaf sasa hawana ustaarabu gari halina kiyoyozi wamefunga vioo alaf sisi abiria wa njian tumesimama ukiwaambia wafungue viooo hawataki alaf ndani wamepanda na samaki yani gari lina harufu Mungu mkubwa nikapata siti aisee kuna mmama hata ustaarabu hana akanyooshaa mkuu kuweka kwenye zile kingo za kuwekea mkono yani aliniboa nikaanza kujiuliza hivi huyu haoni kama mimi nimekaa hapa yani wasukuma jamani hapo kwenye kufunga vioo tu ndio balaa yani siwezi panda tena hayo mabasi yani nilijuta njia nzima nilikuwa na mlaani yule mkata tiket kwanza alinidanganya tiketi imeandikwa ally’s shubaamiti wasukuma
 
Na ikiwa inaita hapokei anaiacha kidogo ichanganye mpate ladha [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Anataka msikilizie mdundo,utajua hujui nakwambia
Ilinikuta kwenye kidinilo la ifakara sitakaa nisahau🤣🤣
 
Kama unatabia za kukoroma ukiwa na usingizi jiepushe , usiwe kero kwa wenzako
 
Kulikuwa hamna kimasihara kwel apo[emoji3][emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Alaf ikawaje sasa
 
Nyie wanaume ndo mnapata visa na mikasa tu Mbona aki na dada hawatoi ushuhuda wanavyofurahia safari.
 
Hii ilinikuta uswahilini, niliwapita wakaazi , nilipotelea chochoro, nikatokezea bafuni
Nilivyorudi kuuliza njia nkikaambiwa tulidhani unaenda kuoga tulikuwa tunajadili wa kukuletea maji
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
 
Alaf ikawaje sasa

Si tukaishia kucheka akaniambia wee chaumbea njoo ukae nikakaa yeye akanipokea kusimama, Mikese kuna abiria akashuka wa siti nyingine akakaa, sijui waliongea nini na konda nashangaa konda ananiambia sister hamia siti ya uku mpishe huyu akae sijui walimshawishi nini mpaka akakubali, nikamgomea konda sirudi nyuma [emoji23][emoji23]

Konda akasema dada utakosa mume wa kukuoa wewe! Ghafla yule bwana si akaja eti njoo yuko serious as if me mkewe, nikamwambia sitaki akasema toka kwenye siti yangu nikae, na mimi nilivyo jeuri nikanyanyuka nikaenda ile siti iliyokuwa wazi nikakaa akamwambia yule abiria aliyemtoa ile siti eti njoo ukae jamaa yangu! Akanifata nilipokaa akakaa nikajinyamazia zangu kimya!

Akaniambia kwanini ulikuwa unasoma msg zangu?! Nikanyamaza akaniambia, unajifanya mstaarabu kumbe mpenda chabo sasa twende ukamalizie kutushikia tochi ilibidi tu nicheke [emoji23][emoji23]

Jamaa ni mtu wa utani mwingi ikabidi niwe mpole niendelee kucheka na jamaa ana vituko na story za uongo! Alikuja kuniteka alivyoleta story za siasa ndio nazipenda basi tukajadili mpaka safari ikawa fupi.

Nikaja kugundua jamaa ni mfanyabiashara maeneo ya nyanda za juu kusini na alinisaidia sana kunifundisha biashara ila ilichukua muda sababu sikuwa na ilo wazo before! Mpaka leo amekuwa mtu wangu wa karibu sana!
 

Mmmmhh si useme tu ndio alikukula kimasihara na ndio baba watoto sasa hivi[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hii naomba iwe namba moja [emoji23][emoji23][emoji23]
Kwani kila atakaekuomba no au kukutongoza lazima umkubalie bibie?,ukiwa kama mwanamke kutongozwa ni lazima ila ni utashi wako kuamua kukubali ama kukataa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…