Yani ndio Bus linatoka mule Mbezi Louis kuitafuta Morogoro road, mama na mtoto waliokaa pembeni yangu wote kwa pamoja wakaanza kutapika. Dakika sifuri tu nimepakwa matapishi dadek.
Sijawahi kusafiri kwa raha mimi.
Enzi za Mohammed trans, natoka kanda ya ziwa kuitafuta Dar. Kuna wabibi ndani ya bus wanasafiri na wajukuu wao wadogo sana kiumri. Mmoja kati yao akaachia uharo kwenye corridor zile za katikati ya siti. Bus zima tulitafutana kwa hiyo harufu yake!
Mara nyingine tena natoka Dar kwenda Kanda ya Ziwa, ndani kuna familia ya hawa ndugu zetu wasukuma. Yani mmoja amekaa siti ya nyuma kabisa, anapiga story na mwenzie aliekaa siti ya katikati ya Bus. Walipanda na ndoo ndogo ya maji ya kunywa, wanachota kwa kikombe then wanapasiana kutoka nyuma mpaka katikati. Siku hiyo kabila lote la wasukuma lilinikwaza!
Mara ya mwisho nimepanda Bus, siti ya pembeni akakaa mzee mmoja hivi. Asee mzee alikua ananuka tumbaku sijawahi ona. Kila watu wakishuka kula na kuchimba dawa, yeye anashuka kuvuta tumbaku zake. Nilifika kwa tabu sana wakuu!