Mambo ya kuzingatia uwapo safarini

Mambo ya kuzingatia uwapo safarini

Kuna siku enzi hizo janki nasoma, natoka shule Tosamaganga naenda home Tanga. Basi ikafika Kitonga Comfort Hotel, nikala msosi wangu kisha nikachukua viroba kama nane hivi nikawa nafyonza mdogo mdogo.

Aisee nikazima. Nilitakiwa kushuka Chalinze niunge gari za kwenda Tanga, nikajikuta niko Mnazi Mmoja naamshwa nishuke, tumefika.
😂😂😂😂Ulikoma
 
Kuna siku nilikua nimelewa sana halafu kwenye bus nilipanda kama staff(dereva tunajuana,classmate wangu)....
Sasa ile naingia tu harufu ya konyagi ikasambaa bus lote..

Kuna mwanamke akaropoka"naona mmepakia pipa la komoni humu mnatukera"...kumbe naenda kukaa nae kwenye seat moja,,,nilisafiri kwa manyanyaso...

Mwisho dereva akaniita nikaenda kukaa nae pale mbele akaninunulia na konyagi nyengine...
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Salimia unayemkuta kwenye siti maana hujui ya baadae. Inakera hukusalimia halafu baadae unaanza kuuliza "Eti hapa tumefika wapi?" 🙄🙄🙄
Hii ni muhimu mno.

Nilikuwa nakwenda Morogoro na basi la Abood la mwisho kabisa kutoka Dar.

Nilipata siti ya mwanzo nyuma ya dereva. Nilikuta kuna binti tayari keshakaa jirani ya siti yangu. Kama ilivyo uungwana nikamsalimia. Binti alinishusha na kunipandisha akachuna.

Nilikuwa nimechoka na mambo yangu, sikumtilia maanani nikauchuna na simu yangu.

Tulipofika chalinze nilinunua maji na korosho, nimkamkaribisha demu, kimya. Hapo hapo na yeye alinunua maji akatoa noti ya 10,000. Jamaa akamwambia hana chenji na bus linataka kuondoka. Nikamwambia jamaa (ni wale wanaouza ndani ya bus) ampe nikamlipa. Kwa aibu akatoa asante ya chini chini. Sikumjibu.

Kufika Morogoro sasa, kumbe ilikuwa anaenda kukutana na mwanaume. Jamaa kila akipigiwa simu hapokei na mwisho akazima simu kabisa. Nililijua hili maana alianza kupiga simu toka tupo Mikese.

Nilipakia spare kwenye boot, hivyo tulipofika Moro ilibidi niwe mpole mpaka mizigo ya wengine iishe. Ndio bi dada ikabidi ajilete kiupole kuuliza kama mimi ni mwenyeji Morogoro. Nikamwambia si mwenyeji nimekuja mara moja nageuza kesho yake.

Ikabidi sasa usister duu aweke pembeni aanze kufunguka ukweli. Kuwa alikuja kukutana na bwana 'ake na ndie aliemtumia nauli.
Ilikuwa ana Sh. 10,000 tu mfukoni na hajui pa kwenda maana mshkaji kaingia chaka.

Ikabidi nimwambie asubiri nichukue mizigo yangu halafu nitaona cha kumsaidia.
Uzuri mwenye spare ilikuwa anazipokelea hapo hapo Msamvu.

Nikaenda kuchukua chumba lodge na mgeni wangu nyuma. Baada ya hapo hatukutongozana tena. Alijuwa wajibu wake na maringo alitupa pembeni tena.

Msela wake alikuja kumtafuta kwenye simu asubuhi tukiwa tunajiandaa kuondoka akiomba samahani kuwa simu ili stuck touch akashindwa kupokea. Itoshe kusema kuwa jamaa alitukanwa kila tusi la duniani.

Mimi na cha maringo wangu tukarudi dar na kuendeleza libeneke kwa miezi kadhaa mbele mpaka nilipoamua kumpotezea kutokana na demu kuwa na shida za kila siku kuliko hata mkimbizi wa Sudan.
 
Usitanue miguu na kujiachia kama uko kwenye sofa lako nyumbani

Inaboaaa kinyama
Mbaba tuliesafiri wote jana na nacharo kutoka Tanga kwenda Dar umenikeraaa
Unatanua miguu siti yangu ukanibana
Unaniongelesha sana na nilikuwa busy na vitu vyangu nimedownload
Unalala nakuegamia upande wangu
Mdomo unanuka na unalazimisha maongezi
Aiseee sijapendaaaa
 
Usitanue miguu na kujiachia kama uko kwenye sofa lako nyumbani

Inaboaaa kinyama
Mbaba tuliesafiri wote jana na nacharo kutoka Tanga kwenda Dar umenikeraaa
Unatanua miguu siti yangu ukanibana
Unaniongelesha sana na nilikuwa busy na vitu vyangu nimedownload
Unalala nakuegamia upande wangu
Mdomo unanuka na unalazimisha maongezi
Aiseee sijapendaaaa
 
Kuna siku nilikuwa kwenye safari Arusha to dodoma , si haba gari nililopanda lilikuwa na wadada wazuri na warembo , safari ilikuwa ya utulivu mno , mpka kajamaa flan iv kwa umbo ni mfupi alipoanza mbwembwe za kupokea simu za madili ya pesa kwa sauti ya juu [emoji1787] dah yani ilikua kero mno ,ila nafikiri alikuwa katika uwindaji cha kushangza kuna pisi moja matata Ali data akashuka nae singida, tuliona ni mjinga ila mkali nafikiri alitimiza malengo yake.
 
nilipanda na kakijana kanenda chuo arusha makumira kamevimba na earphone zake sijui simu gani ile ilikuwa na charge siku nzima tunatoka bk kuja moshi hakikunisemesha kabisa kufika ar 6usiku kanaanza na kuomba miongozo sema nilikuwa nimeokoka siku hio...
 
Back
Top Bottom