Mambo ya kuzingatia uwapo safarini

Mambo ya kuzingatia uwapo safarini

Mambo ya kuzingatia kwenye safari ya beach

Kwenye gari machura kama wote
Nauli ya bodaboda endapo utaachwa
Kua na umoja mwenzenu akipigwa mnakua masojaa
Dereva asilewe sifa mkajikuta mpo chini
😆😆😆😆😆
 
Kisaikorojia hii imetuathiri sana wanaume( sijui kuus wanawake). Unakuta mtu umekaa siti 1 na mwanamke basi ujasiri na asilimia za kumpata vinatake place!
 
Umenikumbusha one time kuna huyu binti kwenye basi la mkoa alileta huu uswahili. Amepanda kwenye basi amevaa jeans, sweater, na kablouse. Basi hana hata pochi yaani yupo kisela sana.

Kilichotokea ni period ilimuanza ghafla bila kujua. Kilichofanya nijue ni alivua sweater lake na kulitumia kama kujifunika sasa mimi nilikuwa na sweater na zile shuka za kimasai. Nikamuuliza mbona umevua sweeter na gari wamewasha AC haikutesi?!

Akajibu kama vile mtu mwenye mawazo na aibu fulani. Ilinichukua dakika chache kunotice kuwa hakuwa sawa na nikashajua huyu ametumia sweater kujificha. Nikamwambia kwa sauti ya chini sana unahitaji msaada. Hakunijibu zaidi ya kuinama kama anaona aibu halafu anaweka lile tabasamu la aibu fulani.

Nikamwambia niandikie kwenye sms unataka msaada gani. Nikampa simu yangu aandike namba yake nikamtext akaanza kuchat akanambia ameingia Period hapo hana uhakika na kinachoendelea ila anahisi amechafua siti sasa hajui pa kuanzia.


Aiseee ni MUNGU tu alisimamia ile situation maana gari lilikuwa na utingo mwanaume tu. So ikabidi nimfuate nimpange kuwa atusaidie wakiona hata kituo cha mafuta wasimame konda akanielewa. Tukasimama akasema abiria tuchimbe dawa kidogo. Watu wakaanza shuka. Akachukua sweta akaliweka pale kwenye siti halafu nikampa shuka langu la kimasai akajifunika mwili mzima so muda tunatoka nashuka nae hakuna mtu alishtukia chochote hadi tunafika chini. Nikamwambia atangulie chini me nakwenda tafuta pedi. Nikaenda mnunulia duka liko huko barabarani kipande kidogo toka pale kwenye sheri nikamletea.

Akajiweka sawa suruali yake ilikuwa imechafuka akaisuuza na maji akavaa hivyo hivyo nikamwambia valia na hilo shuka la kimasai. Tukarejea kwenye gari. Aisee ikawa kama ni mke wangu sasa namna tulivyorudi na kukaa kwenye gari alijiegemesha kwenye kioo me namwambia niegemee kama unataka kulala.

Tulishuka sote stand ya Moshi alikuwa anataka kwenda nikamwambia sidhani kama utakuwa katika hali nzuri kuendelea na safari katika hali hiyo na muda umekwenda twende nyumbani sio mbali na hapa ukaweke mambo sawa uwe safi kesho utaendelea na safari ndugu zako waelezee situation wakitaka watumie picha kabisa halafu tukimbie na huu msala wa kuchafua siti.

Akakubali. Tulishuka sote akafika nyumbani akatoa nguo zote akazifua na kuzianika. Ilibidi nimnunulie kufuri mpya na pedi zingine za brand nzuri.

Nilimpa risala sana ule usiku. Kwamba kwann mtoto wa kike unasafiri kirahisi vile huoni namna umejihatarisha. Yaani unasafiri haubebi kitenge hata viwili na hata pedi tatu za dharula maana hata usipopata wewe anaweza pata mwanamke mwenzako ukamsitiri. Nikamwambia sasa usingekutana na mimi leo si ungefedheheka sana.

Kesho yake nikamsindikiza jioni aende kwa kwao huko Arusha. Na baada ya hapo tuliendelea kuwasiliana she is someone very close to me now.
Kudoz man. Umeturepresent vizuri [emoji109]
 
Kuvua viatu,huku ulikua una mwaka hujafua sox
 
Hiv kwann ukilala huku umekaa unanesa nesa kichwa...

Juz aibu sana nilisinzia kustuka nipo begani kwa dada wa watu usingizi noma kwny bus
 
Yani ndio Bus linatoka mule Mbezi Louis kuitafuta Morogoro road, mama na mtoto waliokaa pembeni yangu wote kwa pamoja wakaanza kutapika. Dakika sifuri tu nimepakwa matapishi dadek.

Sijawahi kusafiri kwa raha mimi.

Enzi za Mohammed trans, natoka kanda ya ziwa kuitafuta Dar. Kuna wabibi ndani ya bus wanasafiri na wajukuu wao wadogo sana kiumri. Mmoja kati yao akaachia uharo kwenye corridor zile za katikati ya siti. Bus zima tulitafutana kwa hiyo harufu yake!

Mara nyingine tena natoka Dar kwenda Kanda ya Ziwa, ndani kuna familia ya hawa ndugu zetu wasukuma. Yani mmoja amekaa siti ya nyuma kabisa, anapiga story na mwenzie aliekaa siti ya katikati ya Bus. Walipanda na ndoo ndogo ya maji ya kunywa, wanachota kwa kikombe then wanapasiana kutoka nyuma mpaka katikati. Siku hiyo kabila lote la wasukuma lilinikwaza!

Mara ya mwisho nimepanda Bus, siti ya pembeni akakaa mzee mmoja hivi. Asee mzee alikua ananuka tumbaku sijawahi ona. Kila watu wakishuka kula na kuchimba dawa, yeye anashuka kuvuta tumbaku zake. Nilifika kwa tabu sana wakuu!
[emoji23][emoji23][emoji119]

Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
 
1. Salimia unayemkuta kwenye siti maana hujui ya baadae. Inakera hukusalimia halafu baadae unaanza kuuliza "Eti hapa tumefika wapi?" 🙄🙄🙄

2. Kuwa mstaarabu unapoingia kwenye basi hasa kama tayari unajua siti yako haina haja ya kugombania mlangoni.

3. Sikiliza nyimbo na video za kwenye simu yako kwa kutumia earphones kwani kinachokufurahisha wewe kwa mwingine yawezekana ni kero.

4. Usiongee na simu kwa sauti kubwa hasa mambo yako binafsi kwani hakuna anayehitaji kujua mambo yako.

5. Kuwa mwangalifu unaposinzia epuka kumlalia jirani yako unaposinzia. Sambamba na hilo soma gazeti lako kwa uangalifu sio unalitandaza hadi linagusa pua ya mwenzako.

6. Usilazimishe kuchungulia dirishani kila mara wakati umekaa siti ya katikati, hiyo ni kero kwa aliyekaa dirishani.

7. Kama unasafiri na watoto wakatie siti yao isiwe kero kwa jirani yako. Unasafiri na watoto watatu kwenye siti moja ni kero kwa jirani yako na kwa watoto.

8. Usipake pafyumu kali za kukereketa wenzio. Sambamba na hilo piga mswaki vizuri ni kero kukaa na abiria anayenuka mdomo hasa anapokusemesha.

9. Msome abiria uliyekaa naye kama hapendi kusemeshwa usimsemeshe semeshe, mwache, wengine wana mambo yao kichwani, wengine wanaenda kwenye misiba, wengine wamefukuzwa na waume zao huko walikotoka, sio kila mtu anapenda kuongea safarini.

10. Kama unajijua una tatizo la kutapika safarini jiandae mapema kwa kuwa na vifaa vya kukusaidia kwenye hali hiyo.

Ongezea la kwako hapo kama unalo.
Eeeh yani ukae siti moja na msukuma anatoka huko machimboni anaenda likizo woiiiii utajuta.
 
Wakati watu wakiwa wanakata tiketi wanaangalia majina. Siku moja nasafiri, kuangalia list ya abiria kwenye chat, nikaona jina Irene Emmanuel si nikajiweka pembeni yake. Kilichonipata ndio hiki sasa!!!!
Kumbe zigo lenyewe ndio hili, nilisafiri kwa kukalia nusu tako toka Dar hadi Kigoma.

View attachment 2594669
Mishandling kama hii inatakiwa ikate siti mbili kwakweli
 
Binafsi

Nabeba maji, Juice, Gums
Dawa za kuzuia kuharisha, Paracematol
Cakes au cookies
Wipes/ Sanitizer

Huwa nikishasalimia watu nalala hadi gari lisimame
 
Kuna siku nilikua nimelewa sana halafu kwenye bus nilipanda kama staff(dereva tunajuana,classmate wangu)....
Sasa ile naingia tu harufu ya konyagi ikasambaa bus lote..

Kuna mwanamke akaropoka"naona mmepakia pipa la komoni humu mnatukera"...kumbe naenda kukaa nae kwenye seat moja,,,nilisafiri kwa manyanyaso...

Mwisho dereva akaniita nikaenda kukaa nae pale mbele akaninunulia na konyagi nyengine...
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mara zote nikinyoosha zile seat za kulala(sleeping coach) abiria wa seat ya nyuma lazima anikataze, Hadi najiuliza sasa hawa wachina ilikuaje hizi seat kuziweka option ya kuzilaza ilhali ukiilaza unakatazwa? Kiukweli inanikera sana
 
Mara zote nikinyoosha zile seat za kulala(sleeping coach) abiria wa seat ya nyuma lazima anikataze, Hadi najiuliza sasa hawa wachina ilikuaje hizi seat kuziweka option ya kuzilaza ilhali ukiilaza unakatazwa? Kiukweli inanikera sana
Kulaza siti ni kwa wastani, usiwe mshamba mshamba kama wasukuma bhana. Unalaza siti kiasi kwamba mtu wa siti ya nyuma yako anashindwa hata kutoka kwenye siti yake?

Huo ni ushamba na unatakiwa ujue hilo.
 
Kulaza siti ni kwa wastani, usiwe mshamba mshamba kama wasukuma bhana. Unalaza siti kiasi kwamba mtu wa siti ya nyuma yako anashindwa hata kutoka kwenye siti yake?

Huo ni ushamba na unatakiwa ujue hilo.
Mkuu hata hiyo wastanj unayosema jamaa wanazingua kiasi kwamba inanibidi nisilaze kabisa
 
Back
Top Bottom