Mambo ya kuzingatia uwapo safarini

Mambo ya kuzingatia uwapo safarini

4. Usiongee na simu kwa sauti kubwa hasa mambo yako binafsi kwani hakuna anayehitaji kujua mambo yako.
Zote zipo sahihi lakini hii hapa imenigusa zaidi. Kuna siku mama mmoja aliboa kwenye gari hadi abiria wote wakawa wanamshangaa jinsi anavyoongea mambo yake binafsi (tena ya kishambenga) kwenye gari kwa sauti kubwa karibu safari nzima. Kuna wamama wanajua kuongea wewe acha tu mkuu! 😀 😀 😀
 
Mim namuuliza kabisa mkata tiketi, nikatie siti ya Kati i.e not dirishani napembeni mweke mwanaume mwembamba mrefu.
Nikikngia namsalim, namwonesha Niko poa, hamna matata kama vipi!!!!
Kwa akili take anajua kimasihara anaopoa ataishia kusifiwa na kupewa Asante,
Namba namwambia dunia duara tutakutana kwenye tukio lingine.
 
Hakuna kitu napenda safarini kama Mwanamke kusinzia na kuniegemea Mimi

Wallah nitampet pet safari nzima, hata kushuka kwenda kula sintashuka..nitamkula yeye

Wabillah Tawfiq
Hakuna safari ninayoifurahiaga kama kukaa seat moja na mkaka/mubabaa anaenukia,haongei sana halafu nimlalie lalie…kele🙆‍♀️🙆‍♀️….safari naionaga fupi
 
Unakutana na mtu ana constipated au ana halitosis kubabake. Unaweza omba kubadilishiwa siti. Halafu watu wanaonuka midomo wanapenda sana kuleta story sijui kwann. Nikama wanakuwa wameshahisi kuwa midomo yao inatema ila wao wapo busy kulazimisha kuwa haitemi.
Fala juzi nimekaa nae Siti moja ni mnene Sana anatumia simu kwa mikono miwili huku kajitanua mkono unakufata kifuani
 
1. Salimia unayemkuta kwenye siti maana hujui ya baadae. Inakera hukusalimia halafu baadae unaanza kuuliza "Eti hapa tumefika wapi?" 🙄🙄🙄

2. Kuwa mstaarabu unapoingia kwenye basi hasa kama tayari unajua siti yako haina haja ya kugombania mlangoni.

3. Sikiliza nyimbo na video za kwenye simu yako kwa kutumia earphones kwani kinachokufurahisha wewe kwa mwingine yawezekana ni kero.

4. Usiongee na simu kwa sauti kubwa hasa mambo yako binafsi kwani hakuna anayehitaji kujua mambo yako.

5. Kuwa mwangalifu unaposinzia epuka kumlalia jirani yako unaposinzia. Sambamba na hilo soma gazeti lako kwa uangalifu sio unalitandaza hadi linagusa pua ya mwenzako.

6. Usilazimishe kuchungulia dirishani kila mara wakati umekaa siti ya katikati, hiyo ni kero kwa aliyekaa dirishani.

7. Kama unasafiri na watoto wakatie siti yao isiwe kero kwa jirani yako. Unasafiri na watoto watatu kwenye siti moja ni kero kwa jirani yako na kwa watoto.

8. Usipake pafyumu kali za kukereketa wenzio. Sambamba na hilo piga mswaki vizuri ni kero kukaa na abiria anayenuka mdomo hasa anapokusemesha.

9. Msome abiria uliyekaa naye kama hapendi kusemeshwa usimsemeshe semeshe, mwache, wengine wana mambo yao kichwani, wengine wanaenda kwenye misiba, wengine wamefukuzwa na waume zao huko walikotoka, sio kila mtu anapenda kuongea safarini.

10. Kama unajijua una tatizo la kutapika safarini jiandae mapema kwa kuwa na vifaa vya kukusaidia kwenye hali hiyo.

Ongezea la kwako hapo kama unalo.

Namba 4. ni tabia ya wasukuma, washamba sana, wanaongea kwa sauti sanaaaa kwenye mabus
 
Umenikumbusha one time kuna huyu binti kwenye basi la mkoa alileta huu uswahili. Amepanda kwenye basi amevaa jeans, sweater, na kablouse. Basi hana hata pochi yaani yupo kisela sana.

Kilichotokea ni period ilimuanza ghafla bila kujua. Kilichofanya nijue ni alivua sweater lake na kulitumia kama kujifunika sasa mimi nilikuwa na sweater na zile shuka za kimasai. Nikamuuliza mbona umevua sweeter na gari wamewasha AC haikutesi?!

Akajibu kama vile mtu mwenye mawazo na aibu fulani. Ilinichukua dakika chache kunotice kuwa hakuwa sawa na nikashajua huyu ametumia sweater kujificha. Nikamwambia kwa sauti ya chini sana unahitaji msaada. Hakunijibu zaidi ya kuinama kama anaona aibu halafu anaweka lile tabasamu la aibu fulani.

Nikamwambia niandikie kwenye sms unataka msaada gani. Nikampa simu yangu aandike namba yake nikamtext akaanza kuchat akanambia ameingia Period hapo hana uhakika na kinachoendelea ila anahisi amechafua siti sasa hajui pa kuanzia.

Aiseee ni MUNGU tu alisimamia ile situation maana gari lilikuwa na utingo mwanaume tu. So ikabidi nimfuate nimpange kuwa atusaidie wakiona hata kituo cha mafuta wasimame konda akanielewa. Tukasimama akasema abiria tuchimbe dawa kidogo. Watu wakaanza shuka. Akachukua sweta akaliweka pale kwenye siti halafu nikampa shuka langu la kimasai akajifunika mwili mzima so muda tunatoka nashuka nae hakuna mtu alishtukia chochote hadi tunafika chini. Nikamwambia atangulie chini me nakwenda tafuta pedi. Nikaenda mnunulia duka liko huko barabarani kipande kidogo toka pale kwenye sheri nikamletea.

Akajiweka sawa suruali yake ilikuwa imechafuka akaisuuza na maji akavaa hivyo hivyo nikamwambia valia na hilo shuka la kimasai. Tukarejea kwenye gari. Aisee ikawa kama ni mke wangu sasa namna tulivyorudi na kukaa kwenye gari alijiegemesha kwenye kioo me namwambia niegemee kama unataka kulala.

Tulishuka sote stand ya Moshi alikuwa anataka kwenda nikamwambia sidhani kama utakuwa katika hali nzuri kuendelea na safari katika hali hiyo na muda umekwenda twende nyumbani sio mbali na hapa ukaweke mambo sawa uwe safi kesho utaendelea na safari ndugu zako waelezee situation wakitaka watumie picha kabisa halafu tukimbie na huu msala wa kuchafua siti.

Akakubali. Tulishuka sote akafika nyumbani akatoa nguo zote akazifua na kuzianika. Ilibidi nimnunulie kufuri mpya na pedi zingine za brand nzuri.

Nilimpa risala sana ule usiku. Kwamba kwann mtoto wa kike unasafiri kirahisi vile huoni namna umejihatarisha. Yaani unasafiri haubebi kitenge hata viwili na hata pedi tatu za dharula maana hata usipopata wewe anaweza pata mwanamke mwenzako ukamsitiri. Nikamwambia sasa usingekutana na mimi leo si ungefedheheka sana.

Kesho yake nikamsindikiza jioni aende kwa kwao huko Arusha. Na baada ya hapo tuliendelea kuwasiliana she is someone very close to me now.
Wahuni watahisi huko mbeleni ulikula tunda kimasihara
 
1. Salimia unayemkuta kwenye siti maana hujui ya baadae. Inakera hukusalimia halafu baadae unaanza kuuliza "Eti hapa tumefika wapi?" 🙄🙄🙄

2. Kuwa mstaarabu unapoingia kwenye basi hasa kama tayari unajua siti yako haina haja ya kugombania mlangoni.

3. Sikiliza nyimbo na video za kwenye simu yako kwa kutumia earphones kwani kinachokufurahisha wewe kwa mwingine yawezekana ni kero.

4. Usiongee na simu kwa sauti kubwa hasa mambo yako binafsi kwani hakuna anayehitaji kujua mambo yako.

5. Kuwa mwangalifu unaposinzia epuka kumlalia jirani yako unaposinzia. Sambamba na hilo soma gazeti lako kwa uangalifu sio unalitandaza hadi linagusa pua ya mwenzako.

6. Usilazimishe kuchungulia dirishani kila mara wakati umekaa siti ya katikati, hiyo ni kero kwa aliyekaa dirishani.

7. Kama unasafiri na watoto wakatie siti yao isiwe kero kwa jirani yako. Unasafiri na watoto watatu kwenye siti moja ni kero kwa jirani yako na kwa watoto.

8. Usipake pafyumu kali za kukereketa wenzio. Sambamba na hilo piga mswaki vizuri ni kero kukaa na abiria anayenuka mdomo hasa anapokusemesha.

9. Msome abiria uliyekaa naye kama hapendi kusemeshwa usimsemeshe semeshe, mwache, wengine wana mambo yao kichwani, wengine wanaenda kwenye misiba, wengine wamefukuzwa na waume zao huko walikotoka, sio kila mtu anapenda kuongea safarini.

10. Kama unajijua una tatizo la kutapika safarini jiandae mapema kwa kuwa na vifaa vya kukusaidia kwenye hali hiyo.

Ongezea la kwako hapo kama unalo.
kama unaweza kufunga ,funga, usikariri kuwa safarini lazima ule. binafsi huwa sili wala kunywa safarini
 
Duuh, umenitamanisha aisee
55690384-9676-4BED-A639-88D9DE1AFDA4.jpeg
 
Mara nyingine tena natoka Dar kwenda Kanda ya Ziwa, ndani kuna familia ya hawa ndugu zetu wasukuma. Yani mmoja amekaa siti ya nyuma kabisa, anapiga story na mwenzie aliekaa siti ya katikati ya Bus. Walipanda na ndoo ndogo ya maji ya kunywa, wanachota kwa kikombe then wanapasiana kutoka nyuma mpaka katikati. Siku hiyo kabila lote la wasukuma lilinikwaza!
😂😂😂
 
Back
Top Bottom