Mambo ya kwa Babu LOLIONDO

Mbn Mussa alitumia fimbo...tena ilikuwa inafanya kazi kwake tuu!???
Think!!!....
 

Kwenye maandamano ya Arusha TBC watu wa Chadema walionesha kuwa hawana imani na Matangazo yao,sikumbuki kama TBC walijisafisha juu ya hili sasa tutakubali vipi hii ya Loliondo ambayo nako ni Arusha.
 

Ndugu radio presenter:
Ukitaka kuongea mambo ya Mungu basi uwe unajua kweli ya Mungu na basi ingia kwenye vitabu vitakatifu na utuonyeshe mistari inayokufanya useme uliyoyasema.
Lazima kwanza uelewe, kila mmoja wetu amepewa karama yake na Mwenyezi Mungu. Hizi Karama siyo lazima kila mtu awe nayo, kila mtu anapewa kutokana na jinsi Mungu anavyopenda iwe. Nadhani ujue kuwa Mungu ana uwezo wake wa ajabu sana na mtu kwa kutumia hekima yako ya kawaida wala si rahisi kutambua. Kuna mambo ya imani zaidi ambayo nadhani kuwa ndiyo yanayotokea huko Loliondo na ndiyo maana baada ya babu kutengeneza dawa anaombea kwanza ndiyo atoe kwa kila mmoja na dozi ni moja tu na wala hairudiwi. Inawezekana Mwenyezi Mungu ana mtu wake anataka kumponya na hakika huyo akishafikiwa inaweza pia ikawa ndiyo mwisho wa dawa!
Kila kinachotokea katika ulimwengu kuna sababu. Kumbuka kuwa babu hajawahi kutangaza kuwa anabiashara ya dawa, ni watu wametoa shuhuda zao na baada ya ndugu ambao walikuwa nao karibu na kushuhudia ukweli huo ndiyo maana watu wameamini. Lakini hii ni imani zaidi! Babu alipoambiwa kwanini asiende kupima hiyo dawa alisema yeye hafanyi biashara ya dawa na hajamlazimisha mtu yoyote kwenda kunywa na anachojua yeye ni kwamba dawa kaoteshwa na Mwenyezi Mungu na ameambiwa awape binadamu. Kumbuka wengi wa wanaokwenda huko ni wale wenye afya zao ambao hata huwezi kujua wanamatatizo ya ndani. Wengi ni watu wa Mungu ambao ni pamoja na wachungaji pia.
Kuna pia madaktari na wengine ambao ni wamiliki na wahariri wa vyombo vya habari licha ya radiopresenter. Unapotaka kukashifu kitu cha watu wengi lazima uwende kwenye details na ukashifu kwa references either za kisayansi au za kiimani ambazo wewe wazijua!!!
Pia ungeweka heading yako, kuwa unataka kujua mengi kuhusu dawa ya huyo babu kwa wale waliotumia na kupona au kutopona!!!
 

Mods; Tafadhali tuondolee upupu hou hapo juu.
 
Inaonekana hujui maana ya headlines na sifa zake! how you can people read it! hehe jisomee magazeti na usikilize vichwa vya habari vya magazeti

FirstLady1 : Mimi simo, yamalizeni wenyewe huko huko! Pasome vizuri hapo kwenye red!
 
wema hawadumu!

SI KWELI,Wewe mpaka leo upo duniani hapa wewe si Mwemwa?na wengine woote waliopo wakina LIPUMBA,SLAA,MBOWE,KAFULILA,MNYIKA,LISU,KABWE,MDEE NK,Hawa wote sio wema?
Kumbuka si kila walichosema wahenga ni sahihi,suala la kufa ni mchakato wa LIFE EXPECTANCY uwe mwema au sio mwema muda wako ukiisha utangulia tu.NB:Nchi yenye life expectancy ndeefu AFRICA mpaka sasa ni LIBYA.
 
Alimaanisha breaking shuzi, maana lilimbana sasa ameshatoa ushuzi wake basi mwacheni, ukiona kwenye kamusi kuna neno mapunguani basi ujue wapo kweli, ndio maana hilo neno lipo.


:becky:
 
Hujui maana ya Breaking news wewe! usipotezee muda watu.
Ukweli ni kwamba kanywe dawa upone hata mungu wakati anateua manabii aliteua 12 tu na akawatuma wakahubiri injiri....Kama dawa hii ingetolewa na wazungu tungeamini maana watanzania na waafrika ndivyo tulivyo we don't believe and trust our findings.
mungu atuokoe kwa hili.
 
Huyu na yule wa mwembechai anayegawa majini ni sawa.
 
We m2 wa wap? Aisee kweny mambo ya mungu hakuna usomi, kwanza hujasoma bible vizur, c kila m2 ni mtakatifu wa kupewa karama ya uponyaji, mungu humteua mmoja katika kundi kwa ajili ya kudhihirisha ukuu wake, peleka upuuz wako huko
 
Radio Producer hata sioni hoja yako inasimamia wapi. Kila uponyaji unategemea na mapokezi ya mtu. Hata chloroquin kwani kila mwenye malaria alipona? je fansida au metakelfin?

Ukirudi kwenye imani, kila uponyaji una mashatri, kama hutako rejea vitabu vyako vitakatifu. Hata Yesu aliponya wenye utayari, hakuzunguka kufuata wagonjwa (na alijua kuwa wapo) wale waliojitokeza kwa unyenyekevu aliwaponya.
Yawezekana kabisa wewe na mimi tusiamini, sasa kwanini tuzuie wengine waaminio, nafsi na dhamira ya mtu itampelekea kupona au kutokupona. Umeshaitune mindset yako kuwa suala hili haliwezekani , kwa hiyo mtu kama wewe hata ukienda huwezi pona , maana umeshajiblock roho yako. Ni sawa na kumeza panadol na kusema ahhh kwanza panadol yenyewe feki tuu.
Ni suala la mtu binafsi na roho wala sioni sababu ya kushupalia ohhh Mungu gani kafanya hivi na vile, if its not your cup of tea, let others have, you dont have to be naive over something you dont have control on.
 

Hii ni Breaking News???

Halafu wewe ukianza kuzungumzia mambo ya dini YATAKUSHINDA.

Kama huamini kaa kimya waache wanaoamini waende shida yako nini hasa????
 

its an unavoidable fact!!!
 
Mbona hata ile fimbo ya ajabu Mungu alimpa Musa peke yake ina maana mungu alikuwa mchoyo kwa kufanya hivyo Na tujiulize tutajifunza nini kama kila mtu atapewa uwezo wa ajabu si tutaumizana wapendwa. Kama mtu una imani yako ni bora kumuuliza mungu kama kamtuma mtu huyo au la. Kwa kufanya hivyo unaweza kuibuka na kipaji kingine na ukaokoa watu kama hiyo dawa itakuwa ina makusudi mengine. Hapa cha msingi ni imani tu.:A S 13::A S 13:
 
watanzania tunapenda sana kuishi.. hatutaki kusacrifice maisha yetu.... kama ni kufa tutakufa tu........ hadi jana mzee kashajikusanyia bilion 1.3...... great business
support this by valid documents!!!!sio unatuwekea urojo hapa
 
Mbn Mussa alitumia fimbo...tena ilikuwa inafanya kazi kwake tuu!???
Think!!!....
Safi sana ili awaokoe wana wa Israel na walipita kabla ya maadui kufika! Sasa huyu ambaye mpaka watu wanazidiwa na kulazimika kuikimbia dunia wakisubiri fimbo yake peke yake hili linakaaje?
 

Huyo Babu analinda Hati Milki (COSOTA) yake kuhusu hiyo dawa ndio maana hataki kuwashirikisha wengine, wabongo hawakawii kuichakachaua dawa yake. Na kuhusu masharti mengine, hata Naaman (yule wa kwenye Biblia) aliwepewa masharti ya kujichovya mara saba, kapona.
 
Wewe bwana hujui mahesabu?? ni wapi ambapo Mungu alitoa kipaji kwa mtu mmoja na akapata shida na kushindwa kuwahudumia wengine haraka iwezekanavyo?? Angalia mateso wanayopata wagonjwa wakati wanasubiria dawa na uwezekano wao kupata dawa haraka na Ujiulize Mungu gani asiyeweza kuongeza watendakazi wake?? Jana alisema itafikia hadi mwezi 1 kwa mtu kupata tiba kutokana na watu wa mabara mengine kuingia nchini zaidi! Swali watakufa wangapi kila siku?? mhuyo ni Mungu??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…