Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkubwa hapo nakuunga mkono! Na kw muda huu nipo mjini Arusha ila w2 ni kedekede wakielekea kwa Babu Loliondo na cjui km hata wengine wamefanya checkup!!Natumai wote ni wazima wanaJF wenzangu.
Well najua mengi yamesemwa kuhusu loliondo. Ila mimi ushauri wangu ni mdogo tu. Tuhakikishe tunafanya medical checkup kabla ya kwenda loliondo, ili ujijue kama unatatizo ama huna. Maana watu wengi hawana tatizo lolote la kiafya lakini wanaenda tu, sasa hiyo inakuwa ni kama kupoteza muda na pia fedha ambazo zingetumika kwa mambo mengine ya kimaendeleo zaidi. Ni hayo tu. Pia naomba mniwie radhi iwapo nitakuwa nimekosea jukwaa maana nilikuwa siona category mbadala ya kuiweka hii. Jioni njema wanajamvi
jamani babu hatoi kinga anatoa tiba kama mtu haumwi asiende,
kwanza mnasababisha foleni kwa babu bila sababu
pili mnawanyima wagonjwa kupata huduma mapema
tatu mnasababisha nauli kupanda nauli kutoka mikoani kwenda arusha zmepanda sana. Kama hujapima usiende, pima kwanza
Kutokana na matamshi ya baadhi ya watu wakiwemo watumishi kama Kakobe, Mwingira, na wengine wengi akiwemo RA kulaani na kupinga uwezo wa tiba ya Mch. Mwasapile,, nimeingiwa na woga kwamba asipokuwa makini atahujumiwa.
Kwa vipi? Hao wasiopenda maendeleo ya wengi, wanaweza wakahujuma na hata kuweka sumu ili tu mchungaji huyo afananishwe na KIBWETERE, na hivyo wateja wao warejee makanisani mwao. Wengine wanadai kama ni kweli eti kwanin asijitangaze apate tuzo ya noble na pesa,, hawajiulizi kwamba huyu Babu hata kama ange charge 100,000 Tsh kwa kikombe,, watu wangekwenda tena wengi tu ili mradi wanaamini kwamba wangepona. Sasa angekuwa na tamaa hapo si angetengeneza pesa lukuki? Piga hesabu tu hata kama angegawa kikombe kwa watu 100 kwa siku,, mil 10 tayari. Lakini masikini anafanya kadiri ya maono aliyopewa.
Hebu wamwache Babu wa watu atimize maono aliyopewa na Mungu. Bali angalizo langu ni lile lile kwamba watamhujumu,, aweke ulinzi mkali panapotayarishwa madawa yake.
Ni hilo tu
nani kakuambia hizi ni siku za MWISHO? na wewe acha unabii wako wa uongo!!!!
Kwa hiyo mwingira amekutuma useme hivyo? Mbona yeye mwingira anawadanganya watu watoe mali zao zote kwake na kuwaacha watu hao maskini hali yeye akibaki kuwa tajiri wa kutupwa kwa kutumia mali hizo hizo alizopora kwa watu wema. Ekari 600 za mahindi kule rukwa, hammer, benki, na mimali kibao amevitoa wapi?
Watu, ambao wanaaminika kuwa na akili vichwani wanahoji kwanini auze dawa hiyo kama ni maono ya Mungu!!!...
Mi kwa hasira nitawaita hawa wote wa jamii hii kuwa ni WAPUMBAVU!...unategemea mtu huyu ataoperate namna gani kutoa dawa kwa watu wa dunia yote, then asipate hata mkate wa shs.500, na kisha afe kwa njaa?
Mbona wahubiri wanaojiita manabii, wapakwa mafuta, mitume na majina meengi ya kujitukuza, mbona wanapokea fedha nyingi sana za sadaka toka kwa waumini wao, kwanini wanamwonea wivu babu kuchangisha siing 500 tu?
Sasa mtu atatoa huduma hiyo BURE, kwa muda gani, maana huduma hii inaonekana itakuwa ya kudumu!
Walalamishi hawa wamepoteza heshima mbele ya jamii, maana wanaonekana wamejaa wivu sana kwa babu!
Wataendelea kusema sana, lakini dawa inatolewa, inaponya, na mwishowe wenyewe watashuka kwenye madhabahu zao na kwenda kutibiwa!
As nte sana Pakajimi kwa Quote yako hii. Yesu alisema "Ukweli Utawaweka Huru". Polepole kina Kakobe, Fernandes, Mwingira na wote wa aina yao wameanza kuumbuka na kupata viwewe. Mamilioni waliyokuwa wakiwakomba watu masikini kama sadaka, fungu la kumi, shukurani na utapeli kedekede yameanza kuyeyuka baada ya waumini kukimbilia kwa Babu mpole, asiyependa sifa, majivuno wala faida binafsi kama walivyo hawa wanaomlaani. Acha wabwabwaje hadi povu liwatoke midomoni, si wamenyang'anywa tonge mdomoni? Matamshi yao, laana na hujuma zao na dhidi ya mchungaji huyu anayetoa huduma sawa na bure yanadokeza u-mbwa mwitu uliojificha ndani yao. Ni dhahiri matamshi yao yatawahukumu wenyewe muda si mrefu.Watu, ambao wanaaminika kuwa na akili vichwani wanahoji kwanini auze dawa hiyo kama ni maono ya Mungu!!!...
Mi kwa hasira nitawaita hawa wote wa jamii hii kuwa ni WAPUMBAVU!...unategemea mtu huyu ataoperate namna gani kutoa dawa kwa watu wa dunia yote, then asipate hata mkate wa shs.500, na kisha afe kwa njaa?
Mbona wahubiri wanaojiita manabii, wapakwa mafuta, mitume na majina meengi ya kujitukuza, mbona wanapokea fedha nyingi sana za sadaka toka kwa waumini wao, kwanini wanamwonea wivu babu kuchangisha siing 500 tu?
Sasa mtu atatoa huduma hiyo BURE, kwa muda gani, maana huduma hii inaonekana itakuwa ya kudumu!
Walalamishi hawa wamepoteza heshima mbele ya jamii, maana wanaonekana wamejaa wivu sana kwa babu!
Wataendelea kusema sana, lakini dawa inatolewa, inaponya, na mwishowe wenyewe watashuka kwenye madhabahu zao na kwenda kutibiwa!