Mambo ya kwa Babu LOLIONDO

Mambo ya kwa Babu LOLIONDO

Sidhani kama ni rahisi namna hiyo.
Nisikukatishe tamaa lakini, ngoja tusubirie, labda watasema
 
Mathias Biabato,

Umeongea jambo la msingi...

Wana JF fanyeni hima ...Huyu bwana asaidike ili naye apate uzima unao semaekana kutoka huko Loliondo!!
 
Natumai wote ni wazima wanaJF wenzangu.
Well najua mengi yamesemwa kuhusu loliondo. Ila mimi ushauri wangu ni mdogo tu. Tuhakikishe tunafanya medical checkup kabla ya kwenda loliondo, ili ujijue kama unatatizo ama huna. Maana watu wengi hawana tatizo lolote la kiafya lakini wanaenda tu, sasa hiyo inakuwa ni kama kupoteza muda na pia fedha ambazo zingetumika kwa mambo mengine ya kimaendeleo zaidi. Ni hayo tu. Pia naomba mniwie radhi iwapo nitakuwa nimekosea jukwaa maana nilikuwa siona category mbadala ya kuiweka hii. Jioni njema wanajamvi
 
Mkubwa hapo nakuunga mkono! Na kw muda huu nipo mjini Arusha ila w2 ni kedekede wakielekea kwa Babu Loliondo na cjui km hata wengine wamefanya checkup!!
 
lakini umeambiwa kuwa ile pia ni kinga hivo si vibaya kunywa tu.......................
 
Jamani babu hatoi kinga anatoa tiba kama mtu haumwi asiende,
kwanza mnasababisha foleni kwa babu bila sababu
pili mnawanyima wagonjwa kupata huduma mapema
tatu mnasababisha nauli kupanda nauli kutoka mikoani kwenda arusha zmepanda sana. KAMA HUJAPIMA USIENDE, PIMA KWANZA
 
jamani babu hatoi kinga anatoa tiba kama mtu haumwi asiende,
kwanza mnasababisha foleni kwa babu bila sababu
pili mnawanyima wagonjwa kupata huduma mapema
tatu mnasababisha nauli kupanda nauli kutoka mikoani kwenda arusha zmepanda sana. Kama hujapima usiende, pima kwanza

wewe hujajua kwanini wabongo wanaipenda hiyo tiba ya babu? Ni kwasababu haina cha vipimo wala majibu we pata kikombe kwanza majibu mbele kwa mbele. Wabongo wengi ni waoga kupima afya zao na hata wale wanaopima kuchukua majibu ni kazi we wanaingia mitini.
 
Kutokana na matamshi ya baadhi ya watu wakiwemo watumishi kama Kakobe, Mwingira, na wengine wengi akiwemo RA kulaani na kupinga uwezo wa tiba ya Mch. Mwasapile,, nimeingiwa na woga kwamba asipokuwa makini atahujumiwa.
Kwa vipi? Hao wasiopenda maendeleo ya wengi, wanaweza wakahujuma na hata kuweka sumu ili tu mchungaji huyo afananishwe na KIBWETERE, na hivyo wateja wao warejee makanisani mwao. Wengine wanadai kama ni kweli eti kwanin asijitangaze apate tuzo ya noble na pesa,, hawajiulizi kwamba huyu Babu hata kama ange charge 100,000 Tsh kwa kikombe,, watu wangekwenda tena wengi tu ili mradi wanaamini kwamba wangepona. Sasa angekuwa na tamaa hapo si angetengeneza pesa lukuki? Piga hesabu tu hata kama angegawa kikombe kwa watu 100 kwa siku,, mil 10 tayari. Lakini masikini anafanya kadiri ya maono aliyopewa.
Hebu wamwache Babu wa watu atimize maono aliyopewa na Mungu. Bali angalizo langu ni lile lile kwamba watamhujumu,, aweke ulinzi mkali panapotayarishwa madawa yake.
Ni hilo tu
 
Wasiwasi wako ndio unapunguza foleni, afadhali mwaya kuna mwingine pia???
 
Watu, ambao wanaaminika kuwa na akili vichwani wanahoji kwanini auze dawa hiyo kama ni maono ya Mungu!!!...
Mi kwa hasira nitawaita hawa wote wa jamii hii kuwa ni WAPUMBAVU!...unategemea mtu huyu ataoperate namna gani kutoa dawa kwa watu wa dunia yote, then asipate hata mkate wa shs.500, na kisha afe kwa njaa?
Mbona wahubiri wanaojiita manabii, wapakwa mafuta, mitume na majina meengi ya kujitukuza, mbona wanapokea fedha nyingi sana za sadaka toka kwa waumini wao, kwanini wanamwonea wivu babu kuchangisha siing 500 tu?

Sasa mtu atatoa huduma hiyo BURE, kwa muda gani, maana huduma hii inaonekana itakuwa ya kudumu!
Walalamishi hawa wamepoteza heshima mbele ya jamii, maana wanaonekana wamejaa wivu sana kwa babu!

Wataendelea kusema sana, lakini dawa inatolewa, inaponya, na mwishowe wenyewe watashuka kwenye madhabahu zao na kwenda kutibiwa!
 
Ndugu yangu una hoja; tena hoja nzito. Kila mtu anatazama suala la Babu kwa jicho na hisia tofauti - nyingine mbaya! Kama watu wameweza kusimama madhabahuni na kumwombea Babu kifo (magazeti ya leo yameandika) basi wanaweza kufanya lolote. Wengine wanalitazama kidini tena kwa hisia mbaya - hawa pia wanaweza kufanya lolote. Wengine wanalitazama kwa maslahi ya kifisadi zaidi - hawa nao kufanya kitu kibaya inawezekena.

Serikali inatakiwa ihakikishe usalama wa Babu na wote wenye kuhitaji huduma yake dhidi ya wote wenye hila mbaya na hii ndio kazi ya msingi ya serikali.
 
Umeenda mbali sana, kumwekea sumu ili afe,.... hapana.
 
nani kakuambia hizi ni siku za MWISHO? na wewe acha unabii wako wa uongo!!!!

Hakuna ajuae siku wala saa,ila mtatambua nyakati za mwisho kwa mambo yatakayo kuwa yanatokea
soma

(Matthew 24:3),
Jesus said, "Ye shall hear of wars and rumours of wars: See that ye be not troubled: for all these things must come to pass, but the End is not yet.For nation shall rise against nation, and kingdom against kingdom

Hauhitaji uelewa mwingine kujua kuwa tuko katika nyakati za mwisho
 
Kwa hiyo mwingira amekutuma useme hivyo? Mbona yeye mwingira anawadanganya watu watoe mali zao zote kwake na kuwaacha watu hao maskini hali yeye akibaki kuwa tajiri wa kutupwa kwa kutumia mali hizo hizo alizopora kwa watu wema. Ekari 600 za mahindi kule rukwa, hammer, benki, na mimali kibao amevitoa wapi?

Hatupaswi kufanya jambo kwa kuwa wengine wanafanya,so una mtetea kwa kuwa wengine pia wanafanya uovu?

Hoja ni kwamba,kama alivo sema anatibu kiimani,ni imani ipi hiyo ambayo "yeye tu" ndo mtoa dawa?
Ingekuwa hivo Yesu alivo lisha maelfu chakula si angegawa mwenyewe?

Kwanini watu wengi wanaifuata na hata serikali imewahi kufuta kauli yake ya kumfungia kutibu?
Njia ya shetani siku zote huwa haipingwi na watu huikimbilia kwa wingi sana!

Kwanini asibariki au kuombea dawa hiyo akawapa watu wagawe kwa wagonjwa?
Kwanini tiba inatolewa sehemu moja tu?

Kuna maswali elfu ambayo ukijiuliza unaweza usitake hata kusogelea maeneo hayo!
 
Watu, ambao wanaaminika kuwa na akili vichwani wanahoji kwanini auze dawa hiyo kama ni maono ya Mungu!!!...
Mi kwa hasira nitawaita hawa wote wa jamii hii kuwa ni WAPUMBAVU!...unategemea mtu huyu ataoperate namna gani kutoa dawa kwa watu wa dunia yote, then asipate hata mkate wa shs.500, na kisha afe kwa njaa?
Mbona wahubiri wanaojiita manabii, wapakwa mafuta, mitume na majina meengi ya kujitukuza, mbona wanapokea fedha nyingi sana za sadaka toka kwa waumini wao, kwanini wanamwonea wivu babu kuchangisha siing 500 tu?

Sasa mtu atatoa huduma hiyo BURE, kwa muda gani, maana huduma hii inaonekana itakuwa ya kudumu!
Walalamishi hawa wamepoteza heshima mbele ya jamii, maana wanaonekana wamejaa wivu sana kwa babu!

Wataendelea kusema sana, lakini dawa inatolewa, inaponya, na mwishowe wenyewe watashuka kwenye madhabahu zao na kwenda kutibiwa!

Hapo kwenye red panakudhihirisha wewe zaidi. Heshimu uhuru wa mawazo. Halafu soma gazeti la raia mwema la leo kuna makala ndefu ya kiuchunguzi kuhusu huyo "nabii". Labda utalegeza msimamo wako. Tuombe Mungu watu wapone kweli, vinginevyo aibu itakuwa juu ya serikali ambayo imegeuka wakala wa babu. Kama mgonjwa anatoroka hospitali halafu anakutana uso kwa uso na daktari wake kwa babu, then mfumo wetu wa afya sio reliable. Tunapeleka signals nzuri sana kwa serikali za nchi jirani. Nadhani waliosema Tanzania inaongoza kwa kuamini nguvu za giza afrika hawahitaji vigezo zaidi!
 
Watu, ambao wanaaminika kuwa na akili vichwani wanahoji kwanini auze dawa hiyo kama ni maono ya Mungu!!!...
Mi kwa hasira nitawaita hawa wote wa jamii hii kuwa ni WAPUMBAVU!...unategemea mtu huyu ataoperate namna gani kutoa dawa kwa watu wa dunia yote, then asipate hata mkate wa shs.500, na kisha afe kwa njaa?
Mbona wahubiri wanaojiita manabii, wapakwa mafuta, mitume na majina meengi ya kujitukuza, mbona wanapokea fedha nyingi sana za sadaka toka kwa waumini wao, kwanini wanamwonea wivu babu kuchangisha siing 500 tu?

Sasa mtu atatoa huduma hiyo BURE, kwa muda gani, maana huduma hii inaonekana itakuwa ya kudumu!
Walalamishi hawa wamepoteza heshima mbele ya jamii, maana wanaonekana wamejaa wivu sana kwa babu!

Wataendelea kusema sana, lakini dawa inatolewa, inaponya, na mwishowe wenyewe watashuka kwenye madhabahu zao na kwenda kutibiwa!
As nte sana Pakajimi kwa Quote yako hii. Yesu alisema "Ukweli Utawaweka Huru". Polepole kina Kakobe, Fernandes, Mwingira na wote wa aina yao wameanza kuumbuka na kupata viwewe. Mamilioni waliyokuwa wakiwakomba watu masikini kama sadaka, fungu la kumi, shukurani na utapeli kedekede yameanza kuyeyuka baada ya waumini kukimbilia kwa Babu mpole, asiyependa sifa, majivuno wala faida binafsi kama walivyo hawa wanaomlaani. Acha wabwabwaje hadi povu liwatoke midomoni, si wamenyang'anywa tonge mdomoni? Matamshi yao, laana na hujuma zao na dhidi ya mchungaji huyu anayetoa huduma sawa na bure yanadokeza u-mbwa mwitu uliojificha ndani yao. Ni dhahiri matamshi yao yatawahukumu wenyewe muda si mrefu.
Ati? wanasema Babu anatumia mapepo? si kweli hata kidogo! Nani kasema kuponda majani ya mti na kuyatumia kama chakula au dawa ni kuendekeza mapepo? Kwa uelewa wangu zile leso, mashati na nguo za wenza wenye kichwa ngumu wanazowaagiza "waongofu" wao ili ziende kuombewa ndiyo ushirikina wa waziwazi. Swali la mwisho ni hivi ni Yesu gani anayefugwa kwenye makanisa yao na anayefanya kazi za "Kutenda miujiza siku, saa, mahali na wa staili wanayoamua watu hawa waliojipachika uchungaji, uaskofu, u-nabii na hata u- mitume? kama ni kweli kwamba Yesu anaweza kufungiwa mahali hadi aje funguliwa na Kakobe, akafanya miujiza hadi atakapoamuliwa na Kakobe kwamba "sasa basi" akaifunga "shughuli"na kuiahirisha hadi siku nyingine; basi huyo ni Yesu asiye na Sovereign. Ndiyo, si Yesu tunayemfahamu sisi. Ni Yesu mwenye kukosa vigezo vya u-Mungu. Kwa hiyo Tafakari, Chukua Hatua.
 
Back
Top Bottom