Mambo ya kwa Babu LOLIONDO


Kabonde mbona umekua mkali hivyo ndugu yangu? unajua hii story inafurahisha sana ingekuwa nawahi kutoka kazii mbona ningekuja kushuhudia mie.
 


Mkuu ile foleni ndefu ndio inakudhihirishia babu hawezi hudumia watu hadi elfu 40 kwa siku moja. Angekuwa na huo uwezo kusingekuwa na foleni kabisa kule. Kumbuka unavyosema watu elfu 40 ni sawa na kuujaza uwanja mpya wa Taifa (Benjamini William Mkapa Stadium) kwa karibu asilimia 67. Kwa faida yako, Babu anafanya huduma yake kati ya saa 12 asubuhi mpaka saa 12 jioni. hapo kumbuka anakuwa na muda wa kupumzika kwa ajili ya kupata chakula. Kwa mahesabu ya wastani anahudumia watu kwa masaa 10 kwa siku. sasa basi kwa idadi ya watu elfu 40 maana yake babu katika kila dakika moja (sekunde 60) anahudumia watu 67. Hii ni impossible ndugu yangu.
 
Kabonde mbona umekua mkali hivyo ndugu yangu? unajua hii story inafurahisha sana ingekuwa nawahi kutoka kazii mbona ningekuja kushuhudia mie.

Mkuu unajua mitanzania imezoea kudanganywa kila siku,mkiambiwa mtajengewa viwanja vya ndege mnakubali,mtanunuliwa meli mnacheka,mtajengewa barabara za juu kwa juu ndio mnakenua meno hamtaki kuuliza viwanja vya ndege vya nini wakati ndege hatuna,watakauliza mnawabatiza majina ya hovyo mara mdini na takataka kibao.

Sina sababu za kumchuria binadamu mwenzangu especially marehemu ninachoeleza hapa ni hali halisi ya mambo yaliyotokea bila kutia chumvi.
 
kubenea hapa naona anataka kuwa mdaku hapa kachemsha aachie watu imani zao kwa nn asizungumzie mapato ya Mwingira au mama Rwakatare au na yy kwa vile si wa imani hiyo basi akae kimya, azidi kubonyea na ashindwe.
 

Ok nimekuelewa mkuu, naona wewe uliamua kutoa live na jina la marehemu tofauti na Ngongo ye aliamua kuficha.
 
ndio walewale wenye mlengo uleeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!
 
Ok nimekuelewa mkuu, naona wewe uliamua kutoa live na jina la marehemu tofauti na Ngongo ye aliamua kuficha.


Mkuu ukitoka kazini hata saa nne usiku unaweza kupitia eneo tajwa #4 sasa hakuna tena kuzungumza kichini chini kila kitu kiko wazi.Mzee Piniel mambo yake yako wazi kwasababu ya upinzani baina ya mke mkubwa na mke mdogo.kulikuwa na patashika nguo kuchanika Mzee azikwe wapi kati ya nyumba ndogo alikokuwa akiishi au kwa mke mkubwa wa ndoa alikohama siku nyingi.

Mtu mwenye nacho msiba wake una mambo mengi hasa wanaobaki wanajaribu kufanya hila za aina mbali mbali ili wapate uhalali wa kurithi mali za marehemu ndicho kinachoendelea hapa.
 
Wewe unaempinga Kubenea tueleza ukweli ni upi si kupinga bila suluhisho.
 

Na ya babu watu wanashuhudia kupona wao matomaso eti nani kapona? wakati wanaona watu katika vyombo vya habari wakitoa shuhuda zao!
Wa TZ ni zaidi ya tomaso
 
Bora nife nikiwa nimesimama kuliko kufa napigania kikombe cha babu

umesema mungu hawezi kushusha karama zake kwa mtu mmoja kwani dunia ni kubwa,
Nikuambie tu
kisichowezekana kwa binadamu kwa mungu kinawezekana.
Kwani mbona mungu alimleta yesu mmoja dunia nzima ili atuokoe na dhambi,
kwanin hakukuwa na kina yesu kila nchi, au kila mtaa?
Vipi kwa Nabii musa mbona aliweza kuwaokaoa wana wa Israel kwa maelfu toka utumwani.
Acha porojo zako kwa babu kwanza huna ushaidi na uyasemayo.
Unasema babu siyo mlokole,hivi kujitangaza kuwa wewe ni mlokole ni sifa? Mbona hyo ni imani ya mtu binafsi,ulitaka atangaze kuwa ameokoka ili dunia nzima 2jue?
Babu ni mchungaji kitaaluma.
Wewe ndio mpinga krito, wala hatuzitaki hoja zenu za kimaslahi binafsi ktk makanisa yenu ambayo kila kukicha yanachipua kama uyoga ili m-make money kwa kujiita manabii.
 
duh!!!!! hii kwli inatisha asee arifu..!!!! mwache huyo mchawi aipate, za mwizi 40, kweli MZEE MWAIPESILE ni sir GOD anafanya kazi kupitia kwake, kweli mungu yupo asee!!!!!!!!!!!!
 
Jibuni kwa hoja na evidence please kwamba babu yuko sahihi kama jinsi vigezo vya kibiblia vilivyo tolewa kwamba hayuko sahihi

unafikiri hapa utapata mtu wa kuja na evidence za maandiko?.Hapa kuna reference moja tu, mwingira! yaani hoja iliyopo hapa ya kujibu jambo hili ni mwingira na sadaka zake, sijui na hammer lake, na benki, mashamba yake nk. yaani hapa kuna blah blah blah tu, pamegeuka THE HOME OF GREAT BELIEVERS WHO OPPOSE THINKING!!! na Bwana alishasema vipofu wakiongozana wote huishia shimoni.

kwa kifupi hata mimi nashindwa kuita huduma hii karama ya Mungu kwani sijaelewa tofauti yake na waganga wengine. we kawaulize hata Profesor maji marefu, matunge nk watakuambia dawa zao huwa wanaoteshwa au wanarithishwa! na lazima ziambatane na masharti!

TIENI AKILI ZENU VICHWANI WATU WA MUNGU, TUNAWAPENDA SANA

Glory to God
 
waache wafe, kwani wasipokunywa ndo watapona?kaka watu wamekata tamaa ndio maana unaona hivyo chochote kile chenye matumaini kwao ni kimbilio

It might be a slow poisoning medicine which can show effect in a year or so.
 
Naunga mkono hoja!
Miujiza gan bila ku2mia jina la YESU? haiwezekan bila YESU, na leo la muujiza ni ili MUNGU atukuzwe na wasio amin waamin, na ndio maana ni lazima kufundishwa neno la MUNGU ili ukipona usirud kwenye zambi lisije kukupata kubwa zaid
 
Kuna mtu kaniaga anaenda Loliondo kwa babu nikamuuliza nini kinampeleka ni kale kajitu,presha au sukari? akasema 'wala, mi naenda ku flush tu',nimechoka kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…