Mambo ya kwa Babu LOLIONDO

Mambo ya kwa Babu LOLIONDO

i was puzzled, real puzzled anaejiita nabii, purpoted to save souls anapomwombea mwenzie mauti. nakumbuka alisema anamlaani sana tu babu. nawafikiria sana hata watu wanaoenda kwake(kanisani) kumsikiliza. in short hamna kitu pale. total illussions
 
Woote ni Maji ga nyanja.tena nikiongea kwa akili za kibaadamu Babu ni afadhali mara maelfu kuliko Mwingira na Kakobe. Yeye anotoa nafuu ya Maisha hawashikii watu akili hata kidogo.

Hawa wawili na wenzaao wanatumia Baalzebubu kuwekea watu mapepo, kuyatao na kupotosha neno la Mungu.

Hawa Mapigo yao yatakuwa double very soon
 
Habari za jioni ndugu, jamaa,marafik na wana JF wote.
Hali inazidi kuwa tete loliondo maelfu ya watu na magari yao wanazidi kumiminika loliondo kuelekea kwa mch ili kupata kikombe cha uzima. Wasiwasi ni wangu ni juu ya hali ya uchafuzi wa mazingira na magonjwa ya milipuko itakayoanza kutokea kutokana mvua zinazoendelea kunyesha hapa loliondo na samunge aliko babu. pia kutokana na watu kuwa wengi hivyo huduma za malazi zimekuwa shida mpaka kupelekea watu kulala nje huku wakinyeshewa na mvua.

Source: lolio
 
Muda simrefu Nimepata habari kama hizi ... watu ni wengi sana...
Na mjini arusha magari yanayoelekea huko kwa leo tu ..yamevunja rekodi!!
 
Wasi wasi wangu ni hvi vijisenti vya babu uko loliondo vinatunzwaje?
Hawa wenye biashara ya benki hawajaiona hii opportunity?

Si vingi sana but kuna umuhimu wa mabenki kuanzisha ka agency kumsaidia babu kuhifadhi makusanyo yake na pia kuwasaidia watu wanoishiwa wakiwa kwa babu.
 
Loliondo is no longer an issue! bring something "PREGNANT"! tumezichoka khabari hizi, badala ya kujadili issues za DOWANS, NAULI kupanda, Mafuta kupanda rejareja, na sasa eti Magari pia yatapanda-utashangaa mpaka yale yaliyoko kwenye YADI zetu toka miaka ya tisini yatapanda kisa TSUNAMI..wizi mtupu!!!!
 
Simchezo, na mpaka sasa bado hakuna huakika kama dawa inafanya kazi au hapana?


Hivi serikali imeshindwa kuwalipa wagonjwa wa 5, wakawapima magonjwa yao kabla kuwapeleka kwa babu. Baada ya hao wagonjwa watano kupata dawa ya babu wakasubiri mda uliotajwa na babu kwamba dawa itakuwa imeshafanya kazi kupita; wakawapima wagonjwa hao tena hili waone kama vipimo vitaonesha kwamba hawana yale magonjwa yalioonekana kwenye vipimo vya kwanza?


Hau ndio serikali yetu wanapenda kufuja hela kwanza kujenga tume wakati swala kama hili unaweza kulitatua kwa njia ndogo tu kama hio ya kuwapa offer wagonjwa wa 5 au 10.
 
Wk end na wote wanataka kurudi kwa ofisi jmatatu
 
Babu pale kwa taarifa yak hachukui hat shiling Moja.Anasema katik hiy shs 500 anayolipwa.Shs 300 anapeleka Kanisani na Shs 200 anawalipa wasaidi9 wak.Man sio kila penye vyanz vya hela benk ni lazima iwekwe.Je!CRDB wakipelek Bank yao kumbe babu anamzuka na NBC AU NMB.Bank haimfati m2 ila mtu inatakiwa aifate bank yenyewe.
 
Hueleweki ni wewe ndio unaenda au huyu anayesoma bango?

kwani ukienda Loliondo kuna shida gani? maana na hakika tangu uzaliwe umeshapitaq kwa waganga wengi sana wa kienyeji sasa tatizo liko wapi?

oanisha kichwa cha habari na maelezo unayoyatoa siyo kujaza post zisizo na kichwa wala miguu. Na hili nalo ni tatizo ni bora ukanywe kikombe usaidiwe.
 
Sio wewe tu Mpasuajipu hata mie nimeshindwa kumuelewa kichwa cha habari na story.
 
AMEKUELEWESHA KIPI KINACHOWEZA KUMTOFAUTISHA MTUMISHI WA MUNGU NA MTUMISHI WA SHETANI.3.MEKUELEZA UTAZAMIE NINI KTK ZAMA HIZI ZA NYAKATI ZA MWISHO kama YESU alisema zipo siku za mwisho ni nani awezaye kubisha???5.FUATILIA KWA MAKINI NI WATU WENGI TU WAMEAMINI NA WAMEPONA UKIMWI KUTOKA KWA WATUMISHI MBALIMBALI.je Mungu aliposema usije mikono mitupu kwangu ulitaka hizo sadaka watu wakazipeleke kwa Mun gu kwa njia gani?????????? MWISHO NAMPONGEZA SANA SPEAKER KWA KULETA MAFUNDISHO HAYA KWA WAKATI WAKE HASA.NENO LA MUNG U LINASEMA WATU WANGU WANAPOTEA KWA KUKOSA MAARIFA SPEAKER AMEWAPA MAARIFA JINA LA BWANA NA LIBARIKIWE SANA.AMEN N

POLE SANA NDG YANGU,1.HUJAFUATILIA TIBA YA BABU IPASAVYO ie ni wakati gani babu amewahubiria wateja wake habari za YESU??? jibu ni HAKUNA ni kikombe unaanza tena ndani ya gari . 2.HUKUMSOMA / KUMWELEWA NDG SPEAKER IPASAVYO ie babu ni mganga wa kienyeji kama wengine wowote -

babu alisema yeye si mganga wa kienyeji,nimemsikia mwenyewe sijaambiwa au kusoma mahali
 
Babu wa loliondo alipoona folen imezidi kua kubwa akasema wa2 wapange mistari miwili;mstari mmoja wa2 wenye pessure ,kisukari na kansa,na wapili watu wenye HIV na AIDS,watu wooote wakapanga kwenye mstari wa kwanza.Kuona hvo babu akasema kumbe hii dawa ya ukimwi niimwage tu maana hakuna wagonjwa!wa2 wacha wapayuke usimwaaaage babuuuuu!!kaaz kwelikweli!Mweeeee!!!
 
Hello,
My greeting to you My name is Shania, single and never married, how are you i hope you are fine and well sounded in good health, i am a good hearten girl loving and caring humble and respectful. i would like to know more about you, please if you do not mind write me with this address (misshania99@yahoo.com)i hope to hear from you soon, because i have something very important to share with you.
Shania

misshania99@yahoo.com

Ukistaajabu ya musa utaona ya firauni, huyu mtu kani pm kama ilivyo, yaani copy and paste,
Nigerian at work
 
Babu wa Loliondo ageuzwa mradi
Imeandikwa na Marc Nkwame na Veronica Mheta, Arusha; Tarehe: 17th March 2011

WAKATI miundiombinu ikizidi kuharibika Loliondo, Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali ameagiza magari kutozwa ushuru na kupiga marufuku waandishi wa habari kumhoji Mchungaji mstaafu Ambilikile Mwaisapile bila kibali.

Marufuku hiyo aliyoitangaza jana, inahusu pia upigaji picha za Mchungaji huyo maarufu kama Babu ambaye anatoa dawa ya magonjwa mbalimbali yakiwamo ya kisukari, Saratani, Kifafa na Upungufu wa Kinga Mwilini (Ukimwi).

Kwa uamuzi wa Lali, magari binafsi hivi sasa yanatozwa Sh. 2,000 wakati makubwa na ya biashara kama mabasi, malori na pick-up, yanayobeba abiria yanatozwa kati ya Sh. 5,000 na Sh. 10,000 na fedha hizo ni kwa ajili ya kuboresha mazingira ya eneo la tiba.

Kwa sasa wateja wa Mchungaji huyo wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), wamekuwa wakilalamikia kuzagaa kwa takataka na uchafu kikiwamo kinyesi cha binadamu huku mvua zikianza kunyesha na kuzua hofu ya magonjwa ya mlipuko.

Kuhusu waandishi wa habari kumwona Mchungaji Mwasapila na hata kumpiga picha, alisema itabidi kwanza kupata kibali kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

“Hivi sasa mwandishi yeyote anayetaka kumhoji au kupiga picha yake, lazima aende Arusha katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kupata kibali maalumu,” Lali alisema.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Isidori Shirima alipoulizwa alihoji, “hakuna kitu kipya, Mchungaji Mwasapila amekwishaeleza kila kitu kuhusu dawa yake sasa ahojiwe nini tena?”

Aidha, Mamlaka ya Udhibiti wa Usimamizi wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) imesema haijaandaa utaratibu wa kudhibiti viwango vya nauli kwa ajili ya magari yanayokwenda Loliondo kupeleka wateja wa Mchungaji huyo, kwa kuwa suala hilo ni la dharura.

Mkurugenzi wa Sumatra wa Mkoa wa Arusha, Ahmadi Kilima, alisema , walikuwa wamesajili mabasi sita yanayofanya safari kati ya Loliondo na Arusha, lakini kutokana na kugundulika kwa dawa hiyo, magari ya aina mbalimbali yamejitokeza kusafirisha abiria.

Alisema, Mamlaka hiyo sasa haiwezi kupanga kiwango cha nauli ya Loliondo kwa magari mengine isipokuwa yaliyosajiliwa, ambayo nauli halali ni kati ya Sh. 13,500 na Sh. 35,000.

Hata hivyo, alisema uongozi wa Arusha na wadau wa usafirishaji, wanalifanyia kazi suala la kupanda nauli ya Loliondo ili kuja na kiwango kimoja.

Alisema, ni vyema suala hilo likafanyiwa kazi haraka ili abiria wajue wanatozwa kiasi gani, kwani suala hilo liko kiholela zaidi kwa kila mmoja kutangaza bei yake.
 
Kumhoji Babu wa "maji ya uzima" kwa dakika 5 shilingi 2,000
Kumpiga picha shilingi 10,000
Kupata haja kubwa vichakani shilingi 3,000
Kupata haja ndogo vichakani shilingi 1,000
Kutema mate shilingi 500
Magari binafsi ya mafisadi yatatozwa shilingi shilingi 20,000 kila gari
Kutupa uchafu wa aina yoyote ile kama maganda ya ndizi/machungwa, mifupa ya kuku n.k. shilingi 2,000

Mhhhh! naona Loliondo na Wilaya nzima ya Ngorongoro itatajirika sana mwaka huu, thanks to "babu wa maji ya uzima"
 
Hatupaswi kufanya jambo kwa kuwa wengine wanafanya,so una mtetea kwa kuwa wengine pia wanafanya uovu?

Hoja ni kwamba,kama alivo sema anatibu kiimani,ni imani ipi hiyo ambayo "yeye tu" ndo mtoa dawa?
Ingekuwa hivo Yesu alivo lisha maelfu chakula si angegawa mwenyewe?

Kwanini watu wengi wanaifuata na hata serikali imewahi kufuta kauli yake ya kumfungia kutibu?
Njia ya shetani siku zote huwa haipingwi na watu huikimbilia kwa wingi sana!


Kwanini asibariki au kuombea dawa hiyo akawapa watu wagawe kwa wagonjwa?
Kwanini tiba inatolewa sehemu moja tu?

Kuna maswali elfu ambayo ukijiuliza unaweza usitake hata kusogelea maeneo hayo!

good food for thought

Glory to God
 
Back
Top Bottom