Azimio Jipya
JF-Expert Member
- Nov 27, 2007
- 3,362
- 1,133
Mchungaji mtikila amesema anashangazwa na jinsi watu mbalimbali pamoja na viongozi wa serikali wanavyobabaika na tiba ya babu.'serikali inadiriki kutaka kuboresha miundo mbinu eti kisa dawa ya kishirikina ya mchungaji mwasapile anayetambuliwa na askofu laizer tu', alisema mtikila.Mtikila alisema serikali na viongozi wake inabidi wawe makini na wasiendekeze mambo ya kishirikina kwa kumtukuza mchungaji mwasapile.
Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Halafu ukishakunywa unatoa sadaka, shilingi 500. Kwanza uponyaji wa Mungu ni for free, hutakiwi kutoa hata senti tano. Utasema ni sadaka, sawa, but hakuna mahali kwenye neno la Mungu (Bible) ambapo tumeambiwa tutoe sadaka kiasi X. Principle ya Mungu ni kutoa kwa kadiri ya uwezo wako.
Hakuna anayepinga asitibu wala watu wasitoe hela, ila kumsingizia Mungu aliyeumba mbingu na nchi kuwa anahusika na shughuli hiyo ni BIG NO in my books, nikimpima kwenye kioo cha neno la Mungu ambako kuna principles za utendaji wake wa kazi sina pa kumlocate huyo babu.
Mimi namwona mchungaji mtikila kama kichaa mwenye confidence na maneno yake,mtanisamehe kwa mtazamo wangu.
MTIKILA NI KATI YA WATU MAKINI NILIOWAHI KUWATAMBUA....take his words