Mambo ya kwa Babu LOLIONDO

Mambo ya kwa Babu LOLIONDO

Hivi Kama babu anatoa dawa na watu wanapona tatizo liko wapi? M'bona hatu question toxicity za arvs zinavyotesa watu? Je dawa za hospitali nazo tusinywe kwa kua hazinathibitishwa au hazitolewi kwa kuna la Yesu?
 
Mimi sipo hapa kumtetea babu wala Mungu wa babu. Ninachofahamu mimi ni kwamba Mungu hahitaji wanadamu wamtetee bali hujitetea mwenyewe. Pamoja na hoja nyingi ambazo zimeshatolewa na watu kuhusu kile kinachoendelea kwa babu, tena kuna wengine wamezungumza wakijibu maswali yote yaliyoinuka kuihusu tiba ya babu kwa hoja zilizoenda shule, bado wengine wanainuka na kuanzisha tread za kuuliza yale yale ambayo yashajibiwa. Nimefikia mahali pa kujishuku kwamba huenda sisi wana Jf, kiwango chetu cha ukichaa kiko juu.
Nasema hivyo kwa sababu ikiwa mtu anauliza maswali hapa jamvini na anamtaka babu ajibu hoja zake kibiblia kama kweli katumwa na Mungu. Hivi ni kweli huyu mtu anaamini kwamba babu anamda wa kufungua jf, ili ajibu hoja zake? Kwa jinsi babu alivyotingwa na kazi yake huanza kutoa tiba 06 hrs to 21hrs kabla ya kulala?
Ninachoona cha wale wote wanaompinga babu hawajawa na hoja za nguvu kwa upande wa imani. Maana hata ukirudi nyuma hakuna yeyote katika manabii wa Mungu aliwahi kukubalika na watu wa wakati wake. Hata yesu mwenyewe walimtuhumu kwamba alikuwa akiwaponya watu kwa nguvu za belzebuli. Na nashindwa kupata jibu ni kwa nini watu hasa wale wa kidini wanampa shetani mamlaka kubwa kuliko Muumba ambaye ni mmiliki wa viumbe vyote. Sasa waulize hawa wanaomtilia shaka babu na kutaka wale waliokunywa dawa wathibitishwe na daktari, sikatai jambo hilo ila wasiwasi wangu mimi kwa hawa watu kama wanae mtu hata mmoja aliyakuwa mgonjwa na baada ya kumwombea akapona na doctor akawapa ushahidi wa uthibitisho wa uponyaji. Sana sana watakuambia tulikemea pepo likatoka na hivyo daktari hawezi kuthibitisha pepo.
Mleta hoja pia anapotosha maandiko ili kukidhi matakwa yake anaposoma matay 24:24 na kueleza kwamba nabii wa uongo watadanganya hata wateule. Kinachomaanishwa kwenye huu mstari ni kwamba mteule hadanganyiki!! Mstari unasema watawadanganya yamkini hata wateule. Hiyo YAMKINI inasimama ikiwa na maana kama INGELIWEZEKANA wateule wangedanganyika. Sasa yamaanisha hawadanganyiki.
Kuhusu huduma kutolewa bure kile kiasi mgonjwa anachotoa pale kwa babu ni kama sadaka tu. Ndodi anatibu sukari kwa sh. 3m.
Tusijipotoshe wenyewe lazima tuwaze nje ya box, Yuda msaliti tunaambiwa alikuwa mweka hazina, hizo pesa alizokuwa akiweka kuna biashara gani mitume waliokuwa wakiifanya?
Kila jambo liwe. kwa jina la Yesu haina maana zaidi kilitamka jina mdomoni zaidi ya kuliishi yaani maisha yaliyomkiri Yesu na matendo yako popote watu humshuhudia Yesu ndani mwako.

Mathew 24:24 For false Christs and false prophets will arise, and they will show great signs and wonders so as to deceive {and} lead astray, if possible, even the elect (God's chosen ones).
--Amplified version--

Njia iendayo uzimani ni nyembamba ndugu. Hivyo imetupasa kuingia kupitia mlango mwembamba, Mathayo 7:13-14. Kuhusu manabii kupingwa hebu angalia ni idadi gani ya watu ilikuwa inawasapoti manabii? Ni wachache sana, tena walipuuzwa. Weeengi walikuwa against manabii. Kuwa makini sana na mambo ya mob psychology. Inawezekana hiyo sauti ya watu wachache ndiyo hasa ya kinabii.

Kuhusu kumpa shetani nguvu kubwa nitakupa andiko moja tu utafakari. "And the devil said unto him, All this power will I give thee, and the glory of them: for that is delivered unto me; and to whomsoever I will I give it." —Luke 4:6
Elewa kuwa shetani ni mungu wa dunia hii.

Kuhusu Yuda labda ueleze Yesu alipokufa aliacha pesa ngapi? Kama alikuwa na pesa unakumbuka kile kisa cha temple tax? Mbona haku-droo kutoka kwa Yuda na kuwalipia wanafunzi wake wote? Kama Yuda angekuwa na michuzi hangetamani vipande 30 vya fedha kuua.

Na kuhusu "thinking outside the box biblia ndiyo yard stick yetu na ni final ( unless you believe in the authority of traditions as well).
“For I testify unto every man that heareth the words of the prophecy of this book: If any man shall add unto these things, God shall add unto him the plagues that are written in this book: And if any man shall take away from the words of the book of this prophecy, God shall take away his part out of the Book of Life, and out of the holy city, and from the things which are written in this book”

—Revelation 22:18-19
 
Mkuu inaelekea ulikipokea kikombe ukiwa katika hali ya fulu kujiachia.
Heri wewe uliyeamini hata maradhi yako yakakuacha, kuliko wale wataalamu wa mashaka na kuhoji.
Hata Yesu angelikuwepo wakati wetu huu katika mwili wangehoji juu ya mamlaka yake, wakitaka kujua ni kwa nini amemfufua lazaro kutoka wafu huku akiacha kufanya hivyo pia kwa baba yake wa kufikia Yusufu?
Hawataki kujisalimisha katika mawazo ya Mungu bali wanamlazimisha ajisalimishe katika mawazo yao.
Kamwe haitakaa iwe hivyo banaa!!!
.
mi sikujua kumbe matukio yepi ni halali na yepi si halali kwa mujibu wa ukristo... Nakwa nini walikuwepo watu waliopinga miujiza ya Yesu wakati huo?nachelea kusema hawa wapingao uponyaji kwa nguvu zote ni wale akina shehe magezi ambao huichambua biblia kwa kuikariri na sio kuielewa
 
Watembee waone na wasome vitabu vingine zaidi ya biblia..Je wale fire walkers wa FIJI island ni wachawi?take in mind that the magic of belief grants phenomenal results for all who accept it....you may gaze upon old men and women,many of them crippled,toiling up a mountain merely for the privilege of worshipping at a Holy Shrine,and you marvel that people being baptized in icy water can come up,giving cry to Alleluia even though their teeth be chattering and their bodies shaking.
 
Mkuu hapo kwenye red tukipaweka sawa unaweza kubadili mtazamo. Mathayo 7 : 16 inasema "mtawatambua kwa matunda yao" na si matendo. Matunda ni outcome. Sasa hebu pima matunda ya babu baada ya watu kubwia hicho kikombe. Kuna mabadiliko yoyote katika roho zao?

Zamani Mungu alikuwa hekaluni katika sanduku la agano. Na waisraeli iliwapasa kwenda huko kwa ajili ya kuomba toba. Lakini tangu kufa kwa Yesu Kristu na pazia kupasuka, Mungu hakai katika majengo achia mbali kwenye kikombe cha babu, bali anakaa mioyoni mwa watu waaminio. Iweje basi pale mimi ninapoamini nisiweze kutengeneza hiyo dawa na kunywa na kyponywa mpaka niende Yerusalem (kwa babu) tena anichotee mwenyewe (kama kuhani mkuu alivyofanya kwa ajili ya dhambi za wengine). Tena basi hilo neno analodai babu linaponywa halimo ndani ya dawa hiyo kwa vile mpaka babu akuchotee mwenyewe ndipo upokee uponyaji. hiyo nguvu ya uponyaji iko mkononi mwa babu.

My bible is my yard stick.

kwa kweli kama ingewezekana kutoa thanks zaidi ya moja, mie ningekupa zaidi ya mia for this very useful posts.

kuna watu wansema hawajaridhika na maandiko tunayotoa hapa kutilia aina ya UKRISTO wa babu na mashabiki wake, tatizo ni kuwa hata hayo mafungu machache ya biblia tunayonuKuu hapa hawayaelewi vizuri kwa sababu ya uvivu wa kutafakari. kweli hali ilivyo inahitaji neema ya Mungu, vinginevyo wale wanaoelekea upotevuni ndio wengi zaidi!

nimebarikiwa sana na msimamo wako mpendwa.

tuko pamoja sana

Glory to God
 
Mathew 24:24 For false Christs and false prophets will arise, and they will show great signs and wonders so as to deceive {and} lead astray, if possible, even the elect (God's chosen ones).
--Amplified version--

Njia iendayo uzimani ni nyembamba ndugu. Hivyo imetupasa kuingia kupitia mlango mwembamba, Mathayo 7:13-14. Kuhusu manabii kupingwa hebu angalia ni idadi gani ya watu ilikuwa inawasapoti manabii? Ni wachache sana, tena walipuuzwa. Weeengi walikuwa against manabii. Kuwa makini sana na mambo ya mob psychology. Inawezekana hiyo sauti ya watu wachache ndiyo hasa ya kinabii.

Kuhusu kumpa shetani nguvu kubwa nitakupa andiko moja tu utafakari. "And the devil said unto him, All this power will I give thee, and the glory of them: for that is delivered unto me; and to whomsoever I will I give it." -Luke 4:6
Elewa kuwa shetani ni mungu wa dunia hii.

Kuhusu Yuda labda ueleze Yesu alipokufa aliacha pesa ngapi? Kama alikuwa na pesa unakumbuka kile kisa cha temple tax? Mbona haku-droo kutoka kwa Yuda na kuwalipia wanafunzi wake wote? Kama Yuda angekuwa na michuzi hangetamani vipande 30 vya fedha kuua.

Na kuhusu "thinking outside the box biblia ndiyo yard stick yetu na ni final ( unless you believe in the authority of traditions as well).
"For I testify unto every man that heareth the words of the prophecy of this book: If any man shall add unto these things, God shall add unto him the plagues that are written in this book: And if any man shall take away from the words of the book of this prophecy, God shall take away his part out of the Book of Life, and out of the holy city, and from the things which are written in this book"

-Revelation 22:18-19

ASANTE sana mpendwa kwa kutoa jibu lililokamilika kwa mtazamo wa kiby

wengi (hata wakristo wenyewe) wamekuwa wakitumia kisingizio cha eti "manabii hawakukubalika nyumbani kwao" kuhalalisha uganga wa babu kwa mujibu wa imani ya kikristo. inasikitisha sana. lazima tusimame tuitetee imani hata kama tutakuwa sehemu ya kundi dogo. shida za magonjwa na dhiki za maisha zisiwe sababu za kushabikia hata roho tusizozijua eti kisa kuna miyjiza inatendeka. yaani watu wamesahahu kabisa kuwa hata shetani anaweza kufanya miujiza!!

it is shocking. ila atakayevumilia mpaka mwiso ndiye atakayeokoka.

Glory to God
 
Hivi Kama babu anatoa dawa na watu wanapona tatizo liko wapi? M'bona hatu question toxicity za arvs zinavyotesa watu? Je dawa za hospitali nazo tusinywe kwa kua hazinathibitishwa au hazitolewi kwa kuna la Yesu?
hata mimi najiuliza hivi ile dawa ingekuwa inatolewa muhimbili wangesemaje,mbona tiba imetekwa na udini? udini si katika siasa tu!hata unapojiona imani yako ni bora na sahihi kuliko wengine ni udini...wenye kupona,kusikia nafuu na hata wasiopona ni maamuzi ya mungu.ubinadamu ni mapungufu na ndiyo maana hujui lililopo mbele yako ila unapambana na liliopo usoni mwako kwa wakati uliopo
 
Hivi Kama babu anatoa dawa na watu wanapona tatizo liko wapi? M'bona hatu question toxicity za arvs zinavyotesa watu? Je dawa za hospitali nazo tusinywe kwa kua hazinathibitishwa au hazitolewi kwa kuna la Yesu?

ARVs ni scientific ila babu ni mystic. matokeo ya ARVs hupimwa kisayansi pia, lakini ya kikombe cha babu yaweza pia kupimwa kwa illusion! zingatia please

Glory to God
 
.
Nimefurahi kwa jibu lako na hasa kwenye eneo la "TABIA" naamini sana katika tabia. Tabia hunena makuu kuliko matendo au maneno. Tabia haitengenezwi bila mateso, na tabia ni ushindi sio kipawa.
Ukiona nguvu yoyote katika utendaji bila tabia ni ya kwa shetani. Ila nguvu na tabia vyafaa kutawala kama Bwana wetu Yesu alivyoshinda na kuketi katika kiti cha enzi cha baba.
Miss judi, je unao ushahidi wa utumishi wa mchungaji wa liliondo kwamba aliwahi kuanguka alipojaribiwa katika huduma yake, ili iwe kwamba ni mtu asiye na tabia ya utauwa(kiungu)?
.

sina ushahidi wa aina hiyo. kabla ya huu uganga wake wala nilikuwa sijawahi kumsikia, sembuse kuyajua maisha yake? mimi nahoji aina ya imani anayotumia kufanyia shuhuli zake za uganga na sababu za kuzifungamanisha shughuli za uganga wake na Yesu/Ukristo hata kawavuta maelfu ya watu wakiwemo wakristo na tena baadhi yao wanamtetea kwa nguvu zao zote bila kujali maandiko yanasemaje. kama angekuwa anafanya shughuli zake bila kusema zimetokana na imani ya kikristo wala nisingekuwa na mengi ya kumlaumu.

nakutahadharisha ndugu yangu ujihadhari na hao unaoita 'wenye tabia za utaua" baadhi wanafanya maigizo tu. usimtazame mtu wala tabia yake hata kumwamini, bali katika kila jambo tumia neno la Mungu kama taa iangazayo njia zako. hakika ni neno pekee lililo kweli na liwekalo huru.

ubarikiwe sana mpendwa

Glory to God
 
Naamini kabisa ile tiba ya Babu wa Loliondo ni Damu ya Yesu. Period!

Kwanini?

Kwa sababu,
1. Ukinywa tu kazi inaanza papo hapo kuanzia pale kichwani kwenye ubongo hukoo puani kwenye macho sijui kushuka hadi kifuani na kwenda sehemu zingine za mwili hadi kwenye unyayo!

2. Ule mitishamba ukitengeneza wewe mwenyewe ni sumu inayoweza kuua, lkn kwa tiba ile ya Babu ni salama maana imeguzwa na kuwa Damu ya Yesu kabisa na mtu akiinywa hadhuriki hata kidogo.

Damu ya Yesu idumu Milele na Milele. Amen.

Njia iendayo uzimani ni nyembamba. Ingia kupitia mlango mwembamba. Amua sasa ndugu.
Hizo illusions hata kwenye biblia zimetajwa.
 
mi sikujua kumbe matukio yepi ni halali na yepi si halali kwa mujibu wa ukristo... Nakwa nini walikuwepo watu waliopinga miujiza ya Yesu wakati huo?nachelea kusema hawa wapingao uponyaji kwa nguvu zote ni wale akina shehe magezi ambao huichambua biblia kwa kuikariri na sio kuielewa

Na shehe magezi wa kwanza kabisa kupinga ni Askofu Kakobe, na sababu yake kubwa (kwa mawazo yangu) anachelea uponyaji wake utagundulika na wale alowateka kuwa haufanyi kazi hivyo watamkimbia na kwenda kwa babu
 
Naamini kabisa ile tiba ya Babu wa Loliondo ni Damu ya Yesu. Period!

Kwanini?

Kwa sababu,
1. Ukinywa tu kazi inaanza papo hapo kuanzia pale kichwani kwenye ubongo hukoo puani kwenye macho sijui kushuka hadi kifuani na kwenda sehemu zingine za mwili hadi kwenye unyayo!

2. Ule mitishamba ukitengeneza wewe mwenyewe ni sumu inayoweza kuua, lkn kwa tiba ile ya Babu ni salama maana imeguzwa na kuwa Damu ya Yesu kabisa na mtu akiinywa hadhuriki hata kidogo.

Damu ya Yesu idumu Milele na Milele. Amen.

Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Halafu ukishakunywa unatoa sadaka, shilingi 500. Kwanza uponyaji wa Mungu ni for free, hutakiwi kutoa hata senti tano. Utasema ni sadaka, sawa, but hakuna mahali kwenye neno la Mungu (Bible) ambapo tumeambiwa tutoe sadaka kiasi X. Principle ya Mungu ni kutoa kwa kadiri ya uwezo wako.
 
Ni kweli uponyaji wa Mungu hauhitaji malipo yoyote ya kifedha lakini kama Babu anawatuma vijana kwenda milimani kutafuta hiyo dawa atawalipa na nini. Suala ni je babu anazifanyia nini pesa hizo. Katika Biblia kuna mistari inaongelea kutoa sadaka na ni 10% ya kipato chako.
 
Naamini kabisa ile tiba ya Babu wa Loliondo ni Damu ya Yesu. Period!

Kwanini?

Kwa sababu,
1. Ukinywa tu kazi inaanza papo hapo kuanzia pale kichwani kwenye ubongo hukoo puani kwenye macho sijui kushuka hadi kifuani na kwenda sehemu zingine za mwili hadi kwenye unyayo!

2. Ule mitishamba ukitengeneza wewe mwenyewe ni sumu inayoweza kuua, lkn kwa tiba ile ya Babu ni salama maana imeguzwa na kuwa Damu ya Yesu kabisa na mtu akiinywa hadhuriki hata kidogo.

Damu ya Yesu idumu Milele na Milele. Amen.
So ile divai tunayokunywa knisani ni pombe na siyo damu ya yesu. maana ile divai haikuniponya kabisa gonjwa langu ila kwa babuuuuu!
 
haha babu kaamua kuwapandisha wadau presha kidogo,amwage tena wkt watu wametoka mbali kufata hiyo lkn kwa gea ya sukari
 
Ni kweli uponyaji wa Mungu hauhitaji malipo yoyote ya kifedha lakini kama Babu anawatuma vijana kwenda milimani kutafuta hiyo dawa atawalipa na nini. Suala ni je babu anazifanyia nini pesa hizo. Katika Biblia kuna mistari inaongelea kutoa sadaka na ni 10% ya kipato chako.

Mungu wa wapi huyo mwenye style moja tu uponyaji, mpaka watu wakachume dawa!! Come on! I cannot reduce the creator of this world to dawa ya mti, hiyo hiyo for the whole country.

Mifano ya uponyaji tunaipata kwa Yesu, alikuwa anademonstrate how rich God is kwenye uponyaji, sio namna moja kwa kila mgonjwa...That's why i am led to believe kuna mungu kamtuma kufanya hivyo lakini si Mungu the creator of this world. He is not that little.
 
Ni kweli uponyaji wa Mungu hauhitaji malipo yoyote ya kifedha lakini kama Babu anawatuma vijana kwenda milimani kutafuta hiyo dawa atawalipa na nini. Suala ni je babu anazifanyia nini pesa hizo. Katika Biblia kuna mistari inaongelea kutoa sadaka na ni 10% ya kipato chako.

points of no point!

ooh, Lord have mercy
 
Ni kweli uponyaji wa Mungu hauhitaji malipo yoyote ya kifedha lakini kama Babu anawatuma vijana kwenda milimani kutafuta hiyo dawa atawalipa na nini. Suala ni je babu anazifanyia nini pesa hizo. Katika Biblia kuna mistari inaongelea kutoa sadaka na ni 10% ya kipato chako.
Hakika lazima awalipe vijana wanao msaidia na pia yeye anashinda kwa kutoa dawa atakula nini maana hakuna kazi nyingine anayofanya mwacheni atibu watu,tanzania kuna wagonjwa wengi sana.
 
Back
Top Bottom