Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hakika lazima awalipe vijana wanao msaidia na pia yeye anashinda kwa kutoa dawa atakula nini maana hakuna kazi nyingine anayofanya mwacheni atibu watu,tanzania kuna wagonjwa wengi sana.
Hii nayo ni joke!!Good reasoning, halafu ingemsaidia nn kugawa foleni wakati wagonjwa wote angewatibu yeye mwenyewe, the joke is note well constructed namshauri mtunzi ai edit kisha atutumie hiyo edited version.
mi sikujua kumbe matukio yepi ni halali na yepi si halali kwa mujibu wa ukristo... Nakwa nini walikuwepo watu waliopinga miujiza ya Yesu wakati huo?nachelea kusema hawa wapingao uponyaji kwa nguvu zote ni wale akina shehe magezi ambao huichambua biblia kwa kuikariri na sio kuielewa
sina ushahidi wa aina hiyo. kabla ya huu uganga wake wala nilikuwa sijawahi kumsikia, sembuse kuyajua maisha yake? mimi nahoji aina ya imani anayotumia kufanyia shuhuli zake za uganga na sababu za kuzifungamanisha shughuli za uganga wake na Yesu/Ukristo hata kawavuta maelfu ya watu wakiwemo wakristo na tena baadhi yao wanamtetea kwa nguvu zao zote bila kujali maandiko yanasemaje. kama angekuwa anafanya shughuli zake bila kusema zimetokana na imani ya kikristo wala nisingekuwa na mengi ya kumlaumu.
nakutahadharisha ndugu yangu ujihadhari na hao unaoita 'wenye tabia za utaua" baadhi wanafanya maigizo tu. usimtazame mtu wala tabia yake hata kumwamini, bali katika kila jambo tumia neno la Mungu kama taa iangazayo njia zako. hakika ni neno pekee lililo kweli na liwekalo huru.
ubarikiwe sana mpendwa
Glory to God
Huyu Babu wa Loliondo kwakuwa amemhusisha Mungu kwenye tiba yake inabidi tutumie pia Neno la Mungu kupima iwapo anayosema au anayoyafanya ni ya kweli au la. Baada ya kuchunguza Neno la Mungu kwa makini mimi nionavyo uponyaji wa Babu huyo hautokani na Mungu kwa misingi hii.
Kwanza: Mungu kwa njia ya Yesu Kristo anaponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina. Watanzania hawasumbuliwi na magonjwa hayo manne tu? Wengine wana mafua yasiyopona, wengine wana majipu ya muda mrefu. Wengine wana magonjwa mabaya ya ngozi nk. Ingekuwa ni Mungu amemtuma, angemwambia aponye magonjwa yote. Yesu alipokuwa hapa duniani aliponya maradhi yote.
Pili: kitendo cha kusema kwamba ni yeye tu Babu mwenye uwezo wa kufanya dawa hiyo iponye magonjwa sio cha kibiblia. Biblia inasema "na ishara hizi(uponyaji ukiwemo) zitafuatana na kila aaminiye..."
Tatu: Yesu alisema "Mtaweka mikono yenu juu ya wagonjwa nao watapata afya" Sio mtawapa kikombe na kuwaombea.
Nne: Kitendo cha kuuza dawa hiyo sio cha kibiblia. Maadam anasema amepewa uwezo huo na Mungu basi hapaswi kuuza uponyaji huo hata kwa shilingi moja. Na kama lengo ni kupata pesa hizo ili kuwapa wasaidizi wake kwanini iwe sh. 500 tu? Shilingi 500 zinafaa nini katika hali ngumu ya maisha waliyo nayo Watanzania leo?
Tano: Mungu anapowaponya watu anawaambia pia waache dhambi. Yesu alimwambia yule aliyemponya "Usitende dhambi tena lisije likakupata lililo baya zaidi kuliko hilo" Huyu Babu anawapa watu dawa tu bila kuwaambia waache ufisadi, rushwa, ujambazi...wakipona si ndio wataendelea kufanya madhambi hayo kwa nguvu zaidi? Mungu hawaponyi watu ili waendelee kufanya dhambi.
Sita: Kama hiyo dawa inaponyesha kwa imani, kwanini anaichemsha kwanza? Imani ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
Saba: Babu anadai kwamba dawa hiyo inaponyesha kwa imani. Mbona basi watu wanapotaka kujichukulia dawa hiyo anawaambia kwamba hawatapona? Yule mama (katika Biblia) aliyekuwa anatokwa damu aligusa upindo wa vazi la Yesu akapona kwa imani. Lakini huyu Babu hataki mtu ajichukulie kikombe mwenyewe hata kama anayo imani.
Nane: Watu wanapotaka kumpa huyu Babu sadaka(magari, nyumba), kwanini anakataa? Wana wa Lawi (katika Biblia) waliambiwa watakula madhabahuni. Sadaka zilipotolewa hawakukataa.
Tisa: Mungu akiponya, uponyaji wake hauwi nusu nusu. Kitabu cha Agano Jipya kinaeleza wazi jinsi watu walivyoponywa kwa ukamilifu magonjwa yao. Kwanini basi katika hao walioenda kwa Babu baadhi yao wanasema kwamba wanajisikia nafuu badala ya kusema wamepona kabisa?
Kumi: Mtumishi wa Mungu ni mtiifu. Mungu anapomwambia jambo anatii. Huyu kama Mungu alimwambia atumie dawa hiyo tangu mwaka 1991 kwanini amempinga Mungu kwa miaka 20? Ni watu wangapi wamekufa kwa magonjwa muda huo wote. Kwanini amekuwa mbishi muda huo wote? Ana huruma kweli na wagonjwa? Mungu hapendezwi na watu wasiomtii.Yona katika Biblia alipoambiwa aende Ninawi alikataa. Kilichompata ni kumezwa na Nyangumi.Kwa msingi huo siamini kwamba Mungu ndiye aliyemwambia atumie dawa hiyo. Vinginevyo Mungu asingemvumilia kwa miaka hiyo yote huku Watanzania wanaendelea kuangamia kwa magonjwa.
Mwisho, najiuliza: Yesu alipokuwa hapa duniani mbona hakuponya watu kwa kuwapa magamba ya miti, majani ya miti nk. Alisema neno tu na magonjwa yakatoweka. Ina maana mti huo utakapokwisha Loliondo na uponyaji ndio utaishia hapo?
Nikiangalia pia Maandiko Matakatifu naona kuwa walikuwepo watu waliosema Mungu amewatuma kufanya hivi au vile na kumbe ni uongo. Biblia pia inasema juu ya "mungu"(wa herufi ndogo)wa dunia hii. Naye anatenda ishara na miujiza. Wakati wa Musa, kule Misri, Musa, Mtumishi wa Mungu, alifanya ishara na miujiza mikubwa na waganga na wachawi wa Misri wakati huo nao wakafanya ishara kama hizo. Na hata waganga wa kienyeji nao pia husema kwamba wanaponya kwa uwezo wa mungu.
Maandiko Matakatifu yanatueleza pia kwamba nyakati za mwisho(naamini hizi ni nyakati za mwisho maana ishara alizozitaja Yesu zimetimia) watatokea manabii wengi wa uongo na kuwadanganya wengi.
Mwisho kabisa nawashauri wamiliki wa Jamii Forum kama inawezekana muandae mdahalo katika redio au televisheni(mdahalo huo muudhamini ninyi)na kisha muwaombe wale wanaomuunga mkono huyo Babu waje wajieleze katika mdahalo huo na wale wanaompinga Babu kama Mch Mwingira, Askofu Kakobe, Rostam nk nao wawepo kwenye mdahalo huo. Nadhani hiyo itakuwa nafasi nzuri ya watu hao kujieleza vizuri na wananchi wapewe nafasi ya kupiga simu na kuwauliza maswali ili umma wa Watanzania upate kujua ukweli na undani wa jambo hili. Huu ni wakati wa ukweli na uwazi. Asante
Uislamu upo wazi hauna löngolongo umekamilika na walishasema BABU "NO". Tatizo ukiristo haujakamilika ndo maana babu kajitokeza kila mtu anaongea lwake leo kakobe, kesho pengo mara upako hakuna dira kabisa.
Mbona hao walikuwepo tangu enzi na hawakuwa na jipya mkuu, vipi yeye?babu ni mganga wa jadi.
-------the end-----