Mambo ya kwa Babu LOLIONDO

Mambo ya kwa Babu LOLIONDO

hahaha, asante mpendwa kuwa kunitikisa mbavu kidogo zimeadjust. hahahaaaaa

ubarikiwe sana

Glory to God
 
Hakika lazima awalipe vijana wanao msaidia na pia yeye anashinda kwa kutoa dawa atakula nini maana hakuna kazi nyingine anayofanya mwacheni atibu watu,tanzania kuna wagonjwa wengi sana.

Hakuna anayepinga asitibu wala watu wasitoe hela, ila kumsingizia Mungu aliyeumba mbingu na nchi kuwa anahusika na shughuli hiyo ni BIG NO in my books, nikimpima kwenye kioo cha neno la Mungu ambako kuna principles za utendaji wake wa kazi sina pa kumlocate huyo babu.
 
Good reasoning, halafu ingemsaidia nn kugawa foleni wakati wagonjwa wote angewatibu yeye mwenyewe, the joke is note well constructed namshauri mtunzi ai edit kisha atutumie hiyo edited version.
Hii nayo ni joke!!
 
Babu sasa anataka kutuua kwa presha au ndio maabara yake ili kujua ni wagonjwa wa aina gani wengi. Hii ni kali!
 
Tuondolee snaa zako hapa,nani kakuambia kuna dawa mbili kule kwa babu?
 
mi sikujua kumbe matukio yepi ni halali na yepi si halali kwa mujibu wa ukristo... Nakwa nini walikuwepo watu waliopinga miujiza ya Yesu wakati huo?nachelea kusema hawa wapingao uponyaji kwa nguvu zote ni wale akina shehe magezi ambao huichambua biblia kwa kuikariri na sio kuielewa

.
Mtizamo wako uko sahihi mkuu na wala hujakosea.
Hawa watu kwa makusudi hawataki kuielewa(amini) biblia ili wasije okolewa na kuachana na biashara zao ndani ya dini.
.
 
sina ushahidi wa aina hiyo. kabla ya huu uganga wake wala nilikuwa sijawahi kumsikia, sembuse kuyajua maisha yake? mimi nahoji aina ya imani anayotumia kufanyia shuhuli zake za uganga na sababu za kuzifungamanisha shughuli za uganga wake na Yesu/Ukristo hata kawavuta maelfu ya watu wakiwemo wakristo na tena baadhi yao wanamtetea kwa nguvu zao zote bila kujali maandiko yanasemaje. kama angekuwa anafanya shughuli zake bila kusema zimetokana na imani ya kikristo wala nisingekuwa na mengi ya kumlaumu.

nakutahadharisha ndugu yangu ujihadhari na hao unaoita 'wenye tabia za utaua" baadhi wanafanya maigizo tu. usimtazame mtu wala tabia yake hata kumwamini, bali katika kila jambo tumia neno la Mungu kama taa iangazayo njia zako. hakika ni neno pekee lililo kweli na liwekalo huru.

ubarikiwe sana mpendwa

Glory to God

.
Ni kweli kwamba kila jambo napaswa kutumia kioo cha neno la Mungu na ni hicho najaribu kutumia hata kwa huyu babu. Katika neno kuna aya inayoniambia kwamba akiisha kumiminwa Roho wa Kristo kwa watu, wazee wao wataota ndoto. Mpaka hapo mzee yupo ndani ya neno. Na pia tahadhari ya pili niliyochukua ni hii ya onyo la Mungu kwamba akitokea muonaji au nabii na kufanya ishara kubwa nazo zikatokea, halafu kisha akakuambia umwabudu mungu mwingine asiye Mungu wa kweli, mkatae tena anastahili kuuawa. Baba katika kutoa tiba yake sijaona akiwataka watu waiabudu miungu ila katika vipindi vyake vya asubuhi kabla ya kazi ya dawa anafundisha injili ya Yesu na ibada inayotolewa pale ni kwa Mungu Yehova. Hamlazimishi mtu kuifuata itikadi yake kama ambavyo Bwana Yesu asivyolazimisha. Wengi wa walioponywa na Yesu waliambiwa wakajionyeshe kwa makuhani, na wengine aliwaambia wasimuambie mtu na hata baazi ya waliotaka kufuatana nae baada ya kuponywa aliwakataza kwa kuwapa ukweli kwamba ndege wana viota vyao, mbweha wana mapango lakini yeye (Yesu) hana mahali pa kuweka kichwa. Watu ni wagonjwa na wanahitaji uponyaji sasa Mungu yeye huwaponya wote bila kuufanya huo uponyaji kama sharti la mgonjwa kumfuata. Angefanya hivyo ingeliweza kuwa Mungu anayatumia matatizo ya watu kuwalazimishia kwake hata kama hawamtaki na ingewezajengeka kwamba Mungu ni wa vile vilivyovidhaifu na vinyonge.
Sijapata kosa la babu bado katika dawa kulingana na neno maana hajaifanya hiyo dawa kuwa fundisho la kanuni ya kiibada. Humpa yeyote na kumwacha aende zake. Yanayozidi hapo kawaachia viongozi wa kidini wa hao wanaomwendea.
.
 
Hivi kwa mawazo yenu mlio wengi wagonjwa wanahitaji hotuba ndefu na zilizopangwa vizuri zaidi ya kwamba wanahitaji kufunguliwa kutoka katika maradhi yao?
Biblia haisomwi kama kitabu cha historia na kukariri mistari yake.
Neno la Mungu lipo katikati ya mistari ya maandiko na hivyo kuna haja ya kusoma katikati ya mistari. Naomba tusaidiane kwa wale wanaochangia, hivi mtu anaekuponya maradhi yako ya mwili anaitwa nani? Nafikiri ni mganga. Na je Mungu anasifa ya kuwa mganga kwetu?
Au labda tuseme doctor maana wengine wamechukulia kuwa doctor ni zaidi ya mganga kwa ulimbukeni tuliobebeshwa na watu wa magharibi. Na wengi wa wale wanaojiita wakristo leo wanazifuata mila na desturi za kimagharibi wanazodhania kuwa ndio ukristo.
Sitaki kuwa mtumwa wa nadharia ya mtu fulani aliyoiasisi kutokana na baazi ya vifungu vya maandiko ya biblia. Mimi ni mfungwa wa Kristo na nguvu za ufufuko wake. Uhuru uliopo katika Roho wake ndio nimeitia nanga yangu.
.
 
Loliondo sasa balaa

• Serikali yataka watu wasiende kupata tiba

na David Frank
Tanzania Daima

SAFARI za watu kwenda kupata tiba kwa mchungaji mstaafu Ambilikile Mwasapile wa Kijiji cha Samunge, Loliondo zimeingia dosari baada ya kuanza kunyesha mvua za masika zilizoligeuza eneo hilo kuwa kisiwa.
Mvua hizo zilizonyesha kwa takriban siku tatu sasa zimewafanya watu kushindwa kuingia na kutoka katika eneo hilo, jambo linalosababisha usumbufu mkubwa.

Eneo hilo ambalo lipo bondeni chini ya viunga vya milima Sonjo na mingine limekuwa tumbo la kupokea maji ya mvua na mito inayotiririsha maji yake kuelekea katika kijiji hicho.
Awali kabla ya kuanza kwa mvua hizo, mchungaji Ambilikile Mwasapile anayedaiwa kutoa dawa ya kutibu magonjwa sugu yakiwemo ukimwi na kisukari kwa kutumia dawa za miti shamba aliiomba serikali iboreshe mazingira ya eneo analotolea tiba na njia zinazotumika kukifikia Kijiji cha Samunge.
Kutokana na mvua hizo, serikali ya Wilaya ya Ngorongoro imewataka watu wanaohitaji huduma ya ‘Babu wa Loliondo' kuvuta subira hadi mvua itakapokoma.

Ombi hilo la serikali limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali, ambaye alisema mazingira ya hivi sasa katika Kijiji cha Samunge si ya kuridhisha kwa binadamu.

"Mvua ni nyingi mno, kijiji hiki kimekuwa kisiwa, mustakabali wa maisha ya binadamu yako shakani, ninawaomba wale wote wenye nia ya kwenda kwa ‘Babu', kusitisha kwa muda mpaka mambo yatakapokuwa shwari," alisema.
Aliongeza kuwa mvua hizo zimeleta tafrani kubwa kwa sababu wale waliopata tiba wanataka kutoka eneo husika huku wale wasiopata kikombe wakitaka tiba hiyo, licha ya mazingira ya kuingia eneo la tukio kuwa magumu.
"Hakika hali ni ya tafrani, kwani mito yote inatiririsha maji eneo la tiba, walio ndani hawawezi kutoka na walio nje hawaingii, panahitajika helikopta kuwanusuru," alisema.

Katika hatua nyingine, Mchungaji mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwasapile, ametishia kusitisha huduma yake hiyo kwa wagonjwa wanaotoroshwa kutoka hospitalini na kupelekwa kwake.
Alisema kuwa kumejengeka tabia kwa baadhi ya watu kuwatorosha wagonjwa katika hospitali wakiwa na dripu za maji, damu huku hali zao zikiwa mahututi.
Alibainisha kuwa tabia hiyo ndiyo inayochangia vifo kwa wagonjwa hao mara wafikishwapo kwake, hivyo kuanzia sasa ameamua kupiga marufuku utoroshaji huo.

"Kuanzia sasa sitawapatia matatibu wagonjwa wanaotoroshwa hospitalini huku hali zao zikiwa mbaya, nafanya hivi kwa sababu tabia hii imeanza kuota mizizi na ndiyo inayochangia vifo kuongezeka," alisema.
Alibainisha kuwa utoroshaji wa wagonjwa hao ni kitendo cha kinyama na hatari kwani miundombinu ya kufika katika kijiji anachoishi si imara kama inavyofikiriwa.

Alisema watu wanapopeleka wagonjwa wao kwake ni lazima wazingatie miundo mbinu ya kufika kijijini hapo na zaidi barabara ambayo ni mbaya kupitika. Mchungaji Mwasapile amejizolea umaarufu ndani na nje ya nchi kwa kutoa huduma ya kutibu magonjwa sugu kwa kutumia mti shamba, ambapo kila mwenye kuhitaji huduma hiyo hutakiwa kulipa kiasi cha sh 500 kwa kikombe kimoja cha maji kilichochanganywa dawa inayotokana na mti huo. Idadi ya magari na watu imekuwa ikiongezeka kadiri siku zinavyosonga mbele, ambapo hivi sasa mgonjwa anaweza kupata dawa hiyo katika kipindi cha siku tatu badala ya siku moja kama ilivyokuwa awali.

blank.gif
 
Huyu Babu wa Loliondo kwakuwa amemhusisha Mungu kwenye tiba yake inabidi tutumie pia Neno la Mungu kupima iwapo anayosema au anayoyafanya ni ya kweli au la. Baada ya kuchunguza Neno la Mungu kwa makini mimi nionavyo uponyaji wa Babu huyo hautokani na Mungu kwa misingi hii.
Kwanza: Mungu kwa njia ya Yesu Kristo anaponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina. Watanzania hawasumbuliwi na magonjwa hayo manne tu? Wengine wana mafua yasiyopona, wengine wana majipu ya muda mrefu. Wengine wana magonjwa mabaya ya ngozi nk. Ingekuwa ni Mungu amemtuma, angemwambia aponye magonjwa yote. Yesu alipokuwa hapa duniani aliponya maradhi yote.
Pili: kitendo cha kusema kwamba ni yeye tu Babu mwenye uwezo wa kufanya dawa hiyo iponye magonjwa sio cha kibiblia. Biblia inasema "na ishara hizi(uponyaji ukiwemo) zitafuatana na kila aaminiye..."
Tatu: Yesu alisema "Mtaweka mikono yenu juu ya wagonjwa nao watapata afya" Sio mtawapa kikombe na kuwaombea.
Nne: Kitendo cha kuuza dawa hiyo sio cha kibiblia. Maadam anasema amepewa uwezo huo na Mungu basi hapaswi kuuza uponyaji huo hata kwa shilingi moja. Na kama lengo ni kupata pesa hizo ili kuwapa wasaidizi wake kwanini iwe sh. 500 tu? Shilingi 500 zinafaa nini katika hali ngumu ya maisha waliyo nayo Watanzania leo?
Tano: Mungu anapowaponya watu anawaambia pia waache dhambi. Yesu alimwambia yule aliyemponya "Usitende dhambi tena lisije likakupata lililo baya zaidi kuliko hilo" Huyu Babu anawapa watu dawa tu bila kuwaambia waache ufisadi, rushwa, ujambazi...wakipona si ndio wataendelea kufanya madhambi hayo kwa nguvu zaidi? Mungu hawaponyi watu ili waendelee kufanya dhambi.
Sita: Kama hiyo dawa inaponyesha kwa imani, kwanini anaichemsha kwanza? Imani ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
Saba: Babu anadai kwamba dawa hiyo inaponyesha kwa imani. Mbona basi watu wanapotaka kujichukulia dawa hiyo anawaambia kwamba hawatapona? Yule mama (katika Biblia) aliyekuwa anatokwa damu aligusa upindo wa vazi la Yesu akapona kwa imani. Lakini huyu Babu hataki mtu ajichukulie kikombe mwenyewe hata kama anayo imani.
Nane: Watu wanapotaka kumpa huyu Babu sadaka(magari, nyumba), kwanini anakataa? Wana wa Lawi (katika Biblia) waliambiwa watakula madhabahuni. Sadaka zilipotolewa hawakukataa.
Tisa: Mungu akiponya, uponyaji wake hauwi nusu nusu. Kitabu cha Agano Jipya kinaeleza wazi jinsi watu walivyoponywa kwa ukamilifu magonjwa yao. Kwanini basi katika hao walioenda kwa Babu baadhi yao wanasema kwamba wanajisikia nafuu badala ya kusema wamepona kabisa?
Kumi: Mtumishi wa Mungu ni mtiifu. Mungu anapomwambia jambo anatii. Huyu kama Mungu alimwambia atumie dawa hiyo tangu mwaka 1991 kwanini amempinga Mungu kwa miaka 20? Ni watu wangapi wamekufa kwa magonjwa muda huo wote. Kwanini amekuwa mbishi muda huo wote? Ana huruma kweli na wagonjwa? Mungu hapendezwi na watu wasiomtii.Yona katika Biblia alipoambiwa aende Ninawi alikataa. Kilichompata ni kumezwa na Nyangumi.Kwa msingi huo siamini kwamba Mungu ndiye aliyemwambia atumie dawa hiyo. Vinginevyo Mungu asingemvumilia kwa miaka hiyo yote huku Watanzania wanaendelea kuangamia kwa magonjwa.
Mwisho, najiuliza: Yesu alipokuwa hapa duniani mbona hakuponya watu kwa kuwapa magamba ya miti, majani ya miti nk. Alisema neno tu na magonjwa yakatoweka. Ina maana mti huo utakapokwisha Loliondo na uponyaji ndio utaishia hapo?

Nikiangalia pia Maandiko Matakatifu naona kuwa walikuwepo watu waliosema Mungu amewatuma kufanya hivi au vile na kumbe ni uongo. Biblia pia inasema juu ya "mungu"(wa herufi ndogo)wa dunia hii. Naye anatenda ishara na miujiza. Wakati wa Musa, kule Misri, Musa, Mtumishi wa Mungu, alifanya ishara na miujiza mikubwa na waganga na wachawi wa Misri wakati huo nao wakafanya ishara kama hizo. Na hata waganga wa kienyeji nao pia husema kwamba wanaponya kwa uwezo wa mungu.
Maandiko Matakatifu yanatueleza pia kwamba nyakati za mwisho(naamini hizi ni nyakati za mwisho maana ishara alizozitaja Yesu zimetimia) watatokea manabii wengi wa uongo na kuwadanganya wengi.
Mwisho kabisa nawashauri wamiliki wa Jamii Forum kama inawezekana muandae mdahalo katika redio au televisheni(mdahalo huo muudhamini ninyi)na kisha muwaombe wale wanaomuunga mkono huyo Babu waje wajieleze katika mdahalo huo na wale wanaompinga Babu kama Mch Mwingira, Askofu Kakobe, Rostam nk nao wawepo kwenye mdahalo huo. Nadhani hiyo itakuwa nafasi nzuri ya watu hao kujieleza vizuri na wananchi wapewe nafasi ya kupiga simu na kuwauliza maswali ili umma wa Watanzania upate kujua ukweli na undani wa jambo hili. Huu ni wakati wa ukweli na uwazi. Asante
 
Hatuwezi kunyamaza, wakati ndugu zetu wanaangaamia.

Mwisho kabisa nawashauri wamiliki wa Jamii Forum kama inawezekana muandae mdahalo katika redio au televisheni(mdahalo huo muudhamini ninyi)na kisha muwaombe wale wanaomuunga mkono huyo Babu(Maaskofu wa KKKT na Babu mwenyewe) waje wajieleze katika mdahalo huo na wale wanaompinga Babu kama Mch Mwingira, Askofu Kakobe, Rostam nk nao wawepo kwenye mdahalo huo. Nadhani hiyo itakuwa nafasi nzuri ya watu hao kujieleza vizuri na wananchi wapewe nafasi ya kupiga simu na kuwauliza maswali ili umma wa Watanzania upate kujua ukweli na undani wa jambo hili. Huu ni wakati wa ukweli na uwazi. WE MUST DARE TO TALK OPENLY!! Thank you
 
Huyu Babu wa Loliondo kwakuwa amemhusisha Mungu kwenye tiba yake inabidi tutumie pia Neno la Mungu kupima iwapo anayosema au anayoyafanya ni ya kweli au la. Baada ya kuchunguza Neno la Mungu kwa makini mimi nionavyo uponyaji wa Babu huyo hautokani na Mungu kwa misingi hii.
Kwanza: Mungu kwa njia ya Yesu Kristo anaponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina. Watanzania hawasumbuliwi na magonjwa hayo manne tu? Wengine wana mafua yasiyopona, wengine wana majipu ya muda mrefu. Wengine wana magonjwa mabaya ya ngozi nk. Ingekuwa ni Mungu amemtuma, angemwambia aponye magonjwa yote. Yesu alipokuwa hapa duniani aliponya maradhi yote.
Pili: kitendo cha kusema kwamba ni yeye tu Babu mwenye uwezo wa kufanya dawa hiyo iponye magonjwa sio cha kibiblia. Biblia inasema "na ishara hizi(uponyaji ukiwemo) zitafuatana na kila aaminiye..."
Tatu: Yesu alisema "Mtaweka mikono yenu juu ya wagonjwa nao watapata afya" Sio mtawapa kikombe na kuwaombea.
Nne: Kitendo cha kuuza dawa hiyo sio cha kibiblia. Maadam anasema amepewa uwezo huo na Mungu basi hapaswi kuuza uponyaji huo hata kwa shilingi moja. Na kama lengo ni kupata pesa hizo ili kuwapa wasaidizi wake kwanini iwe sh. 500 tu? Shilingi 500 zinafaa nini katika hali ngumu ya maisha waliyo nayo Watanzania leo?
Tano: Mungu anapowaponya watu anawaambia pia waache dhambi. Yesu alimwambia yule aliyemponya "Usitende dhambi tena lisije likakupata lililo baya zaidi kuliko hilo" Huyu Babu anawapa watu dawa tu bila kuwaambia waache ufisadi, rushwa, ujambazi...wakipona si ndio wataendelea kufanya madhambi hayo kwa nguvu zaidi? Mungu hawaponyi watu ili waendelee kufanya dhambi.
Sita: Kama hiyo dawa inaponyesha kwa imani, kwanini anaichemsha kwanza? Imani ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
Saba: Babu anadai kwamba dawa hiyo inaponyesha kwa imani. Mbona basi watu wanapotaka kujichukulia dawa hiyo anawaambia kwamba hawatapona? Yule mama (katika Biblia) aliyekuwa anatokwa damu aligusa upindo wa vazi la Yesu akapona kwa imani. Lakini huyu Babu hataki mtu ajichukulie kikombe mwenyewe hata kama anayo imani.
Nane: Watu wanapotaka kumpa huyu Babu sadaka(magari, nyumba), kwanini anakataa? Wana wa Lawi (katika Biblia) waliambiwa watakula madhabahuni. Sadaka zilipotolewa hawakukataa.
Tisa: Mungu akiponya, uponyaji wake hauwi nusu nusu. Kitabu cha Agano Jipya kinaeleza wazi jinsi watu walivyoponywa kwa ukamilifu magonjwa yao. Kwanini basi katika hao walioenda kwa Babu baadhi yao wanasema kwamba wanajisikia nafuu badala ya kusema wamepona kabisa?
Kumi: Mtumishi wa Mungu ni mtiifu. Mungu anapomwambia jambo anatii. Huyu kama Mungu alimwambia atumie dawa hiyo tangu mwaka 1991 kwanini amempinga Mungu kwa miaka 20? Ni watu wangapi wamekufa kwa magonjwa muda huo wote. Kwanini amekuwa mbishi muda huo wote? Ana huruma kweli na wagonjwa? Mungu hapendezwi na watu wasiomtii.Yona katika Biblia alipoambiwa aende Ninawi alikataa. Kilichompata ni kumezwa na Nyangumi.Kwa msingi huo siamini kwamba Mungu ndiye aliyemwambia atumie dawa hiyo. Vinginevyo Mungu asingemvumilia kwa miaka hiyo yote huku Watanzania wanaendelea kuangamia kwa magonjwa.
Mwisho, najiuliza: Yesu alipokuwa hapa duniani mbona hakuponya watu kwa kuwapa magamba ya miti, majani ya miti nk. Alisema neno tu na magonjwa yakatoweka. Ina maana mti huo utakapokwisha Loliondo na uponyaji ndio utaishia hapo?

Nikiangalia pia Maandiko Matakatifu naona kuwa walikuwepo watu waliosema Mungu amewatuma kufanya hivi au vile na kumbe ni uongo. Biblia pia inasema juu ya "mungu"(wa herufi ndogo)wa dunia hii. Naye anatenda ishara na miujiza. Wakati wa Musa, kule Misri, Musa, Mtumishi wa Mungu, alifanya ishara na miujiza mikubwa na waganga na wachawi wa Misri wakati huo nao wakafanya ishara kama hizo. Na hata waganga wa kienyeji nao pia husema kwamba wanaponya kwa uwezo wa mungu.
Maandiko Matakatifu yanatueleza pia kwamba nyakati za mwisho(naamini hizi ni nyakati za mwisho maana ishara alizozitaja Yesu zimetimia) watatokea manabii wengi wa uongo na kuwadanganya wengi.
Mwisho kabisa nawashauri wamiliki wa Jamii Forum kama inawezekana muandae mdahalo katika redio au televisheni(mdahalo huo muudhamini ninyi)na kisha muwaombe wale wanaomuunga mkono huyo Babu waje wajieleze katika mdahalo huo na wale wanaompinga Babu kama Mch Mwingira, Askofu Kakobe, Rostam nk nao wawepo kwenye mdahalo huo. Nadhani hiyo itakuwa nafasi nzuri ya watu hao kujieleza vizuri na wananchi wapewe nafasi ya kupiga simu na kuwauliza maswali ili umma wa Watanzania upate kujua ukweli na undani wa jambo hili. Huu ni wakati wa ukweli na uwazi. Asante

wewe kakobe .... acha wivu .... watu wamepona .... wewe unaleta fundamentalism .... ponya watu kwa hayo maandiko basi kama unaweza .... mmechoka kuhubiri kwenye dala dala sasa mnamuonea wivu babu wa watu .... huna hoja haujalazimishwa kwenda loliondo wala huna uhalali wa kuwakataza watu waende loliondo
 
The ‘Loliondo miracle cure’, which may be aptly captured by the expression ‘Loliondo-mania’, has electrified the sensibilities, anxieties, curiosity, hopes and expectations of people in, and beyond Tanzania.
Predictably, it has triggered a debate pitting those who associate it with superstition against those who assign a scientific credit to it, albeit coupled with a divine touch.
On the whole, however, the pendulum seems titled in favour of those who believe that the herbal ‘mugariga’ concoction administered by retired Lutheran Pastor Ambilikile Masapila is potent, going by testimonies of outright or partial cure, as well as considerable relief by patients of diseases that include the still vaccine-and-cure defiant HIV/Aids.
It is inconceivable that those claiming medical salvation or relief can be part of a fictitious theatrical show, for, who can sacrifice or volunteer one’s poor health to be manipulated as a tool for amusing or fooling the rest of mankind? And at what cost in return? We submit that, people can, in their thousands, as has happened and may do so in future, be ensnared in such ‘wajinga ndio waliwao’ (fools paradise) traps as the Deci pyramid scheme, due to the itch for rapid financial fortunes.
That ensnarement cannot conceivably be replicated in the health of individuals and their beloved ones, by manifesting it through trooping or escorted in droves to the until-recently sleepy Samunge village some 400 kilometres from Arusha, including terminally ill patients de-hooked from drips in hospital beds.
The cure seekers include academically highly advanced, widely travelled, scientifically and technologically vastly exposed politicians, corporate executives, public sector technocrats, business sector wheeler-dealers and socially high-profile opinion leaders, who cannot even remotely be associated with primitive beliefs paradoxically, some medical doctors have not only shunted modern medicine aside and partaken of Reverend Masapila’s ‘mugariga’ dose, but have expressed amazement over persons they knew had been HIV-positive but had subsequently tested negative! Springing from ‘Loliondo-mania’ however, are aspects like mismanaged medical service, horrible sanitation, political opportunism, religious bigotry and wild dreams, which we must critically ponder.
Relatively simple ailments like coughing and diarrhea can be fixed by simple medication, but torture many people due to poverty that shuts them from the mainstream medical service; or, the woefully under-facilitated public dispensaries and hospitals. Periodic outbreaks of cholera jolt authorities into short-lived sanitation improvement campaign; after which poor sanitation reigns. Should the solution lie in the ‘mugariga’ dose; for millions of people; and for how long ?
Only a few philanthropists and charitable institutions assist medically critically needy persons ; otherwise hundreds die for lack of money to finance relatively simple surgical operations.
The sudden upsurge of generosity by politicians to finance trips for their constituents to and from Loliondo is opportunism par excellence; pure and simple! Responses to ‘Loliondo-mania’ should reflect as pan-territorial a character as witnessed, in, say, mobilisations over the Dowans saga. The ‘Me-and-my-constituents’ and ‘we-and-our-MP’ approach punches holes in the ‘wananchi servants’ projections of the sectionalist politicians.
The move by certain clerics to demonise Reverend Masapila over his alleged divine-propelled medication can only be characterised as sheer envy by self-ascribed messiahs, whose messianic powers are doubted, or an outright hoax.
We at The Guardian on Sunday are advocating sobriety in probing, assessing , and drawing lessons from ‘Loliondo-mania’. The positive aspects should be appreciated, exaggerations should be ignored, spiritualism shouldn’t be ignored, and false hopes shouldn’t be trumpeted.
A judicious blend should be struck between the essentially complementary traditional and modern medicine, without undermining other considerations. Preying on people’s ignorance and poverty for political gain or social glory is deplorable, sinful in the eyes of God, and thus damnable.
SOURCE: EDITORIAL - GUARDIAN ON SUNDAY
 
Uislamu upo wazi hauna löngolongo umekamilika na walishasema BABU "NO". Tatizo ukiristo haujakamilika ndo maana babu kajitokeza kila mtu anaongea lwake leo kakobe, kesho pengo mara upako hakuna dira kabisa.

Uislam upo wazi eeh?? Kalabaghao...! Endelea kukaa na majini yako maimuna,makata n.k na mihirizi then kwa neno la Yesu Kristo watu wanapona na wanajiandaa kwa Paradiso,ww na majini unaedai niviumbe ka viumbe wengine i hope unajua makata,maimuna watakakoenda baada yamaisha then uungane nao! Kam to Jesus,acha kuzubaishwa najua si makosa yako umepumbazwa na moyo wako unaufanya kuwa mgumu! Jinyenyekeze nawe utapata taji la uzima wa milele kwa Bw.Yesu Kristo.
 
Mchungaji mtikila amesema anashangazwa na jinsi watu mbalimbali pamoja na viongozi wa serikali wanavyobabaika na tiba ya babu.'serikali inadiriki kutaka kuboresha miundo mbinu eti kisa dawa ya kishirikina ya mchungaji mwasapile anayetambuliwa na askofu laizer tu', alisema mtikila.Mtikila alisema serikali na viongozi wake inabidi wawe makini na wasiendekeze mambo ya kishirikina kwa kumtukuza mchungaji mwasapile.
 
Hivi Mtikilila alipewa uchungaji na nani vile? Alijipachika.
 
MTIKILA NI KATI YA WATU MAKINI NILIOWAHI KUWATAMBUA....take his words
 
Back
Top Bottom