Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Afande pia ni binadam kama sisi na kama ni maradhi hata yeye anaweza kuwa nayo,big up afande kwa kuokoa maisha yako huku ukiwaacha watu wanashangaa.
Humu JF kuna baadhi yetu wamekwisha kwenda kwa babu na kupata tiba ya magonjwa sugu.Na wengi wanatumia ID za kubuni.
Jamani jitokezeni mtupatie udhibitisho wa kupona baasda ya kutumia dawa hii ya 'babu' ili na sisi tulioko mbali tuanze kudunduliza ili twende.
Tunawategemea sana waliokwisha kunywa.Tupe matokeo
Nawasilisha
Wewe kikombe unacho hapo si ulete majibu au sio cha babu hicho? :A S-coffee::ranger:Sidhani kama ni rahisi namna hiyo.
Nisikukatishe tamaa lakini, ngoja tusubirie, labda watasema
Watu, ambao wanaaminika kuwa na akili vichwani wanahoji kwanini auze dawa hiyo kama ni maono ya Mungu!!!...
Mi kwa hasira nitawaita hawa wote wa jamii hii kuwa ni WAPUMBAVU!...unategemea mtu huyu ataoperate namna gani kutoa dawa kwa watu wa dunia yote, then asipate hata mkate wa shs.500, na kisha afe kwa njaa?
Mbona wahubiri wanaojiita manabii, wapakwa mafuta, mitume na majina meengi ya kujitukuza, mbona wanapokea fedha nyingi sana za sadaka toka kwa waumini wao, kwanini wanamwonea wivu babu kuchangisha siing 500 tu?
Sasa mtu atatoa huduma hiyo BURE, kwa muda gani, maana huduma hii inaonekana itakuwa ya kudumu!
Walalamishi hawa wamepoteza heshima mbele ya jamii, maana wanaonekana wamejaa wivu sana kwa babu!
Wataendelea kusema sana, lakini dawa inatolewa, inaponya, na mwishowe wenyewe watashuka kwenye madhabahu zao na kwenda kutibiwa!
Tahadhari! Hebu tujiulize. Hivi dawa ya babu kama ni sumu ya kuondoa pole pole itakuwaje? Nani anajua athari zake? Huyu Babu mwenyewe umri umeenda inawezekana akili zake zimeanza kupoteza majira lakini kila mtu anakimbia huko.
Hiii sii hoja hoja ni kwamba Hivi kweli watanzania uwezo wa kufikiri umefika mwisho?
Hivi tutaendelea kubahatisha mambo mpaka lini? Wasomi wako wapi?Madaktari nao wamefta mkia kama Kakobe? Je? Serikali nayo inaongozwa kwa bahati nasibu.Madhara yakitokea watatuambia JANGA?
Kwa staili hii tusitegemee kupata maendeleo kwa lolote katika nchi hii. Na ninani alaumiwe kwa hili?
CHUKUA HATUA LEO USISUBIRI KESHO.
Poleni watanzania mtakaodhurika na mogariga.