Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Moja,mtongoze mwanamke lakini usimuonyeshe bila yeye huwezi pata mwanamke mwingine,kadri utakavyo zidi kumfuatilia sana basi tambua ndio jinsi atakavyo kaa mbali na wewe na kukusumbua sana
Mbili,hata umpe mwanamke wako hela nyingi kiasi gani,au uisugue mbususu kiasi gani au usimamie kucha kiasi gani haita mzuia yeye kukuacha,akiamua kukuacha atakuacha tu
Tatu,mjali mpenzi wako au mke wako lakini usijisahau nawe kujiwekea kipaumbele,jithamini nawe pia,usikose vitu vizur au mambo mazuri kwasababu ya kujinyima ili mwanamke wako afurahi
Nne,jitahidi kumridhisha mwanamke kitandani kwa kadri ya uwezo wako,lakini usiharibu afya yako ya uzazi kwa kutumia sijui mkongo na aina nyingine za viagra,mwisho wa siku ukawa mtegemezi wa mambo hayo
Tano,mhudumie mwanamke kwa mapenzi yako na kwa utashi wako,lakini kamwe usidhani kwa kufanya hivyo ndio sababu ya kutoachwa,jua tu kwamba hizo ni huduma tu na si agano au kinga ya kutoachwa,ili ukiachwa usipate msongo wa mawazo kuwa umemgharamia sana
Sita,mpende mwanamke unavyo mpenda lakini usipoteze uanaume wako,kuwa na msimamo,ukisema mbele tembea na iwe hivyo,na ukisema nyuma geuka na iwe hivyo,wanawake wanapenda kuongozwa na sio kuwa na mwanaume ambaye hajui nafasi yake
Saba,kumfuatilia sana mwanamke na kumchunguza ni dalili kwamba una udhaifu mkubwa juu yake au dhaifu kiasi kwamba hujiamini kama anaweza kuwa wako peke yako,hivyo unataka kumlinda kitu ambacho hauta kiweza kamwe
Nane,kuwa na mwanamke au mkeo lakini usimfanye yeye ndio kila kitu chako,kwa maana furaha yako isitegemee uwepo wake maishani mwako,ili siku akiondoka uweze kuendelea na maisha kama kawaida,katika ulimwengu wa mapenzi moyo umeficha mengi
Tisa,kama ambavyo maisha ni kupanda na kushuka,basi hata mapenzi nayo yapo hivyo,leo utalia na kesho utafurahi,mzungumko uko hivyo,kwahiyo wakati wa kufurahi furahi na wakati wa kulia we lia,maisha ndio yalivyo
Kumi,hakuna mjanja katika mapenzi,kwakuwa hujapata misukosuko sasa basi usiwaone wengine ni wajinga,trust me siku yako inakuja na utaelewa hiki ninachosema
Mwisho,Mapenzi hayana mwenyewe ndio maana kila mtu anaumizwa kwa namna moja au nyingine,iwe tajir au maskini wote wamewahi kuumizwa na wanaendelea kuumizwa
Natamani mwanangu wa kiume wa kwanza ayajuaye haya mapema,au Mungu anipe umri mrefu ili ifikie kipindi tuyazungumze haya man to man
Ni hayo tu!