Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Maisha ya mwanadamu yanahitaji vitu vikuu vinne:-
- Chakula
- Sehemu ya kulala
- Afya njema
- Mavazi
Chakula
Mwanadamu lazima ahakikishe, miaka yote anapata chakula stahiki, iwe bei imepanda au kushuka, na hii ataitimiza kwa kujiwekea miradi mbali mbali ya kibiashara, kilimo, na ufugaji. Ili kufanikisha hili, ni muhimu kupunguza anasa zinazofuja kipato chako.
Sehemu ya kulala (makazi)
Ni vizuri uwe na sehemu yako ya kulala; uwe una kazi ama huna kazi. Hakikisha unapata sehemu nzuri ya kupumzisha mwili wako. Na hii utafanikisha baada ya kuacha vitu vya anasa anasa.
Afya njema
Afya ndio kila kitu, vitu vya anasa ndivyo chanzo namba moja vya kuangamiza afya ya mwili. Mwili ukilegea, kutimiza malengo mengine ni vigumu; muda mwingi utakuwa unautumia kwenda gereji (hospitali). Hili utafanikisha utakapoachana na vitu vya anasa anasa.
Mavazi
Mavazi ni hitaji pia la muhimu kwa binadamu, na hili utafanikiwa baada ya kupunguza au kuacha vitu vya anasa.
Kwa uchambuzi huu; tumia pesa yako kwa mambo ya maana, achana na starehe, kwa sababu mwisho wake huwa ni mbaya.