Alex Muuza Maembe
JF-Expert Member
- Dec 13, 2024
- 655
- 1,413
(1) Ukipiga mihayo (yawning), chafya au kukohoa, funika mdomo na pua kwa mikono yote miwili.
(2) Usiteme mate, kutapika, kupenga kamasi, wenzako wakiwa wanakula.
(3) Ukienda nyumbani kwa mtu, hususan rafiki, usitangaze madhaifu utakayoyaona. Mfano: Watoto wao wanashindia nguo zilizochanika au wanakula dagaa kila siku.
(4) Rafiki yako unayeheshimiana naye, usiwe na namba ya simu ya mkewe ili kuepuka kutembea naye. Kamwe usitembee na mke wa best friend yako.
(5) Ukiacha kazi ofisini, usiwatukane former employers wako kwa maana katika maisha kuna leo na kesho.
(6) Ni vema ukapakua chakula kidogo kisha ukaongeza kuliko kupakua kingi alafu ukashindwa kukimaliza.
(7) Ukienda kwenye sherehe, hata kama wewe ni ndugu za karibu, usikae sehemu za VIP bila kukaribishwa. Ni aibu sana kuambiwa uondoke kwenye seat za VIP uende kwa wageni wa kawaida.
(8) Ukigundua spouse wa rafiki yako ana uhusiano wa nje ya ndoa, mfuate na mkanye ila usimwambie mumewe/mkewe.
(9) Mtu akikusaidia mara moja, usimgeuzi kitega uchumi cha kumuomba mara kwa mara. Kumbuka yeye pia ana majukumu yake binafsi.
(10) Ukiongea kwenye simu na mtu wa mbali sio vizuri kusema "fulani (Alex) nipo naye hapa ongea naye pia. Kama huyo Alex hajakuomba kuongea na mhusika basi kaa kimya.
(11) Ukipata mshahara mwisho wa mwezi, wape kidogo mfanya usafi pamoja na mpika chai hapo ofisini kwenu. Hao ndio informers na wanajua mengi ya hapo ofisini kwenu.
(12) Usiache kwenda likizo ya mapumziko kwa kuambiwa eti "tutakufidia kwa fedha hizo siku 28 za mapumziko". Afya yako ya akili ni kitu cha msingi sana.
(13) Ukienda ugenini kisha ukaachwa peke yako sebuleni, usishike chochote kama mwenyeji wako hayupo (ameenda kunununulia soda kwa mfano). Hata kama ni gazeti umelikuta hapo, subiri akirudi ndio umuombe.
ANGALIZO: Mimi sio malaika. Mimi nina mapungufu yangu. Ila tujitahidi sana kutenda yaliyo mema kadri ya uwezo wetu.
ONGEZEA NA WEWE NDUGU YANGU......
Ni mimi,
Alex Muuza Maembe
======