Mambo yanayokatisha tamaa kuwapa lifti baadhi ya watu

Braza Kede

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2012
Posts
3,840
Reaction score
6,844
Unapotoa lifti kwa baadhi ya watu tegemea mambo haya,

- Wizi/ukwapuaji - si ajabu umempakiza mkaka mtanashati au mdada mlimbwende lakini anaposhuka akaondoka na kitu chako hasa hivi vitu vya thamani mfano laptop. Umefika unakoenda unachungulia kitu chako ukawajibike unakuta holaah hamna kitu! kumbe yule mwamba au mlimbwende uliyempa lifti alishashuka nacho.

- Uharibifu - unaweza kukuta hapo kabla milango ya gari ilikuwa inafunga vizuri tu lakn baada ya kutoa lifti au kuazimisha chombo, milango haifungi au haifunguki kama mwanzo. mwingine unakuta amejining'iniza kwenye ile support hanger ya juu [pale unapoweka suti zako] hadi ameivunja hadi unashangaa sasa huyu alikuwa anabembea hapo juu au alikuwa anafanya nini hadi kavunja?

- Harufu - mwingine upo naye mnapiga stori kumbe mwenzio katoka zake huko bila kuoga au ana fangasi zake zinatema vibaya mno unajaribu kuongeza kiyoyozi unakuta hakifui dafu unaamua kuacha wazi madirisha labda hali itakaa sawa lakini wapi. hapo sasa unakuta huyo mhusika mwenyewe hana wasiwasi anakupigisheni stori tu utafikiri hakuna kinachokera humo ndani.

- Kubeba watu mishikaki - Unamsimama kumpa mtu lifti nayeye anaamua kumwita mwenzake au wenzake kadhaa ili waingie wote kwenye huo usafiri wako. mambo ya ajabu kabisa haya. yaani mimi nimekupa ofa ya usafiri wewe hlf nawew unaita washkaji zako wengine. daah!

- Kujipa u-DJ
- wewe umepewa lifti tu lakn sasa umeshajigeuza umejifanya wewe sasa ndo DJ kwenye gari hata isiyo yako. unaweka mamiziki yako kwa sauti ya vipimo vyako bila hata kujali kama unakera wenzio.

- Kupakia mizigo - wewe umepewa hisani ya lifti lakini sasa bwana wewe au bi wewe umegeuza gari kama ya kwako kila unachokiona huko barabarani unataka kukinunua kiingie kwenye gari. haya sasa unataka kuchoma gari ya watu na magunia ya huko mkaa wako ulionunua huko mabarabarani.

Kwakweli kuna mambo yanafanywa na baadhi ya watu unaweza kuyaona ni madogomadogo lakini kiukweli yana maudhi yake.

Mtaongezea....
 
Unapotoa lifti kwa baadhi ya watu tegemea mambo haya,

- Wizi/ukwapuaji - si ajabu umempakiza mkaka mtanashati au mdada mlimbwende lakini anaposhuka akaondoka na kitu chako hasa hivi vitu vya thamani mfano laptop. Umefika unakoenda unachungulia kitu chako ukawajibike unakuta holaah hamna kitu! kumbe yule mwamba au mlimbwende uliyempa lifti alishashuka nacho.

- Uharibifu - unaweza kukuta hapo kabla milango ya gari ilikuwa inafunga vizuri tu lakn baada ya kutoa lifti au kuazimisha chombo, milango haifungi au haifunguki kama mwanzo. mwingine unakuta amejining'iniza kwenye ile support hanger ya juu [pale unapoweka suti zako] hadi ameivunja hadi unashangaa sasa huyu alikuwa anabembea hapo juu au alikuwa anafanya nini hadi kavunja?

- Harufu - mwingine upo naye mnapiga stori kumbe mwenzio katoka zake huko bila kuoga au ana fangasi zake zinatema vibaya mno unajaribu kuongeza kiyoyozi unakuta hakifui dafu unaamua kuacha wazi madirisha labda hali itakaa sawa lakini wapi. hapo sasa unakuta huyo mhusika mwenyewe hana wasiwasi anakupigisheni stori tu utafikiri hakuna kinachokera humo ndani.

- Kubeba watu mishikaki - Unamsimama kumpa mtu lifti nayeye anaamua kumwita mwenzake au wenzake kadhaa ili waingie wote kwenye huo usafiri wako. mambo ya ajabu kabisa haya. yaani mimi nimekupa ofa ya usafiri wewe hlf nawew unaita washkaji zako wengine. daah!

- Kujipa u-DJ - wewe umepewa lifti tu lakn sasa umeshajigeuza umejifanya wewe sasa ndo DJ kwenye gari hata isiyo yako. unaweka mamiziki yako kwa sauti ya vipimo vyako bila hata kujali kama unakera wenzio.

- Kupakia mizigo - wewe umepewa hisani ya lifti lakini sasa bwana wewe au bi wewe umegeuza gari kama ya kwako kila unachokiona huko barabarani unataka kukinunua kiingie kwenye gari. haya sasa unataka kuchoma gari ya watu na magunia ya huko mkaa wako ulionunua huko mabarabarani.

Kwakweli kuna mambo yanafanywa na baadhi ya watu unaweza kuyaona ni madogomadogo lakini kiukweli yana maudhi yake.

Mtaongezea....

1. Uhalifu ni sababu nyingine.

Unaweza ukampa lifti mtekaji.

2. Kubambikiwa Kesi.

Unaweza ukampa lifti Mtu matokeo yake unaweza kuja Kubambikiwa Kesi mbaya sana na Mambo yako yanaweza kuja kuharibikiwa.
 
Back
Top Bottom