MIXOLOGIST
JF-Expert Member
- Mar 1, 2016
- 14,311
- 36,056
Wasalaam wana JF,
Kesho jamii nzima ya kikristo au sisi wakatoliki tunaanza kwaresma siku 40 za kufunga na kufanya ibada nyingi.
Pamoja na zoezi hilo, naomba niorodheshe mambo yanayonikera kanisani kama yafuatayo:
1. Kwaya kuimba nyimbo ambazo waumini hawazijui. Yaani wanaimba wenyewe tu mavitu ambayo hatuelewi na hatushiriki;
2. Wingi wa matangazo, makanisa yanakua kama platforms za matangazo, yanapoteza muda na kurefusha ibada;
3. Urefu wa mahubiri, mapadre wanaongea sana, waongee kwa kiasi ujumbe utafika tu;
4. Sadaka za kushtukiza, watu wapewe taarifa mapema watatoa tu; na
5. Kushindwa kufuata ratiba za ibada. Hii ni mikoani zaidi, unakaa zaidi ya nusu saa ibada haijatoka tofauti na ilivyoandikwa kwenye time table.
Nawatakia kwaresma njema.