Mambo yanayonikasirisha Kanisani

Mambo yanayonikasirisha Kanisani

Mkuu nina imani unao utashi wa kuelewa kitu kinaitwa ratiba na kitu kinaitwa dharura.

Usually maisha ya binadamu lazima awe na ratiba,Kikanisa na zaidi kiimani ratiba zimewekwa ili watu wapate muda wa kufanya yale yaliyo nje ya kumuabudu Mungu ktk ile siku maalumu (na siyo kwenda kufanya zile kazi ngumu ni kipindi hiki tu waamini tumekuwa viburi au sijui ndo ugumu wa maisha)

Lakini tukija kiimani hasa inapotokea dharura lazima tuelewe kwamba ratiba zetu na Mungu ni vitu viwili tofauti,let's say siku hiyo imepangwa kutolewa mahubiri na padre mwenye karama ya kitu fulani na lazima kwa sababu ni mara chache atakuja parokiani kwenu itabidi atumie muda mrefu kuhubiri ili kiu ya waamini iishe ktk situation kama hii kipi muhimu?utoke kanisani kwa sababu ratiba mliyojiwekea imevunjwa uache kusikiliza neno la Mungu uende ukakae nyumbani au bar huku umefura kwa hasira ukilalamika muda waliokupotezea kwenye Ibada?
Ibada zinaingiliwa na mambo ya kipuuzi ndiyo maana wanashindwa kufuata ratiba. Ukifuatilia ni matangazo na siasa za walei, ujinga mwingi sana
 
Kule kwetu usweken ndaani ndani huko Rukwa, Kuna matangazo hata yasiyo husu kanisa. Kama ulikunywa Lisute hukulipa ujue watakuumbua kwenye matangazo kanisani.

Halafu watu wa kule wanajifanya waumini saana lkn wachawi ndio hao hao na wapenda wasimbe ndio hao hao.

Msimbe ndio single mother huku mjini.
 
Dini zimejengwa kwenye kutisha waumini wake ili waipate adhabu huko rohoni siku ya kufa..uzuri ni kwamba yote mazuri na mabaya huwapata wanao sali nawasio sali..hata maandiko yameweka wazi kuwa Mungu huwanyeshea mvua waovu na wasio waovu.

Live your life chamsingi ishi katika haki na utauwa pia dini iliyosafi ni ile inayosidia wahitaji katika uhitaji wao.

Tofauti na hapo endeleeni kulipa kodi ya koloni rome kila jpl mpelekapo sadaka..huku divai wakishindialia mapadri na kutoka vitambi.

#MaendeleoHayanaChama
All the best mkuu.

Ni mtizamo wako siwezi kuwa against na wewe,Mungu akuongoze.
 
Kila swali ni la msingi. Sasa utatumia vigezo gani kujua maswali ya msingi na utatumia mbinu gani kichagua wauliza maswali. Vipi kuhusu wale ambao hawapata nafasi ya kuuliza.
3 questions to be picked randomly
 
Kule kwetu usweken ndaani ndani huko Rukwa, Kuna matangazo hata yasiyo husu kanisa. Kama ulikunywa Lisute hukulipa ujue watakuumbua kwenye matangazo kanisani.
Halafu watu wa kule wanajifanya waumini saana lkn wachawi ndio hao hao na wapenda wasimbe ndio hao hao.
Msimbe ndio single mother huku mjini.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my TECNO LC6a using JamiiForums mobile app
 
Muda standard kwa ibada usizidi 90 mins.

Zaidi ya hapo ni kupoteza muda.
Hii habari wafikishie maaskofu, wachungaji na wainjilisti wa KKKT.

Hawa watu sijui Kama wanavaa saa. Hasa wainjilisti. Yani muinjilisti Kama ndio mtoa neno siku hiyo utakuta nusu ya watu wanakoroma na kinamama wanene wanene Hadi udenda.
 
Hii habari wafikishie maaskofu, wachungaji na wainjilisti wa KKKT.
Hawa watu sijui Kama wanavaa saa. Hasa wainjilisti. Yani muinjilisti Kama ndio mtoa neno siku hiyo utakuta nusu ya watu wanakoroma na kinamama wanene wanene Hadi udenda.
Wana watwisha watu mizigo mizito ya lawama.
 
Mimi nachukia kunyimwa ekaristi takatifu kisa dhambi zangu lakini hapo hapo sadaka zangu wanazipokea au hata kunidai nisipotoa.
ukumbuke kabla hujaitoa ikiwa mfukoni mwako ile ni hela utoapo tu mfukoni na kuiweka kwenye vilevikapo inabadilika kua sadaka ,inaombewa

Ile ile pesayako uliyotoa hata Kama umeipata kwakuua haina madhara katika kanisa ikishaingia

Damu ya yesu ili ule vizuri lazima utubu dhambi zooote usikike
 
Kanisani Wana himiza kutoa kutoa na kutoa.

Wanasahau kuwaeleza waumini pesa hiyo wanayotoa inatumikaje.

Mchungaji wa KKKT anapata mshahara Ila akiumwa achangiwe pesa ya matibabu.

Mishahara Yao ni ya nini?

Kazi yake ni kuhubiri neno ili watu waache dhambi lakini akisimama pale mbele na kutoa neno akimaliza tu anapewa posho.

Posho kwa kufanya kazi yake?
 
Wasalaam wana JF,

Kesho jamii nzima ya kikristo au sisi wakatoliki tunaanza kwaresma siku 40 za kufunga na kufanya ibada nyingi.

Pamoja na zoezi hilo, naomba niorodheshe mambo yanayonikera kanisani kama yafuatayo:

1. Kwaya kuimba nyimbo ambazo waumini hawazijui. Yaani wanaimba wenyewe tu mavitu ambayo hatuelewi na hatushiriki;

2. Wingi wa matangazo, makanisa yanakua kama platforms za matangazo, yanapoteza muda na kurefusha ibada;

3. Urefu wa mahubiri, mapadre wanaongea sana, waongee kwa kiasi ujumbe utafika tu;

4. Sadaka za kushtukiza, watu wapewe taarifa mapema watatoa tu; na

5. Kushindwa kufuata ratiba za ibada. Hii ni mikoani zaidi, unakaa zaidi ya nusu saa ibada haijatoka tofauti na ilivyoandikwa kwenye time table.

Nawatakia kwaresma njema.
Hata wakukere kiasi gani utaendelea kwenda tu. Kuna minyonyoro wanaitumia kuwafungia watu ili wawe waumini wao wa kudumu.

Utalalamika wee lakini utaenda tu.

Sent from my VF-795 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom