Mambosasa ajibu maswali ya Rais Magufuli kuhusu kutekwa Mo Dewji

Mambosasa ajibu maswali ya Rais Magufuli kuhusu kutekwa Mo Dewji

Yaelekea hata yeye amechoka. Atakuwa Mambojana
 
Mambo sasa alipaswa kusema "maneno yaliyosemwa na Mkuu ya nchi si ya kupuuzwa bali yanapasa kitutafakarisha kama kuna sehemu tumekosea au tulikosea tujisahihishe".

Mambosasa amwambie nani wajitafakarishe na wamekosea na wajisahihishe wakati ametajwa YEYE directly na ni YEYE ndie alikuwa msemaji na mratibu wa ule uchunguzi? We vipi wewe?
 
Hakya ngai hii sinema sijui ni ya jetlee au Rambo..daadekii
 
Kwetu sisi wataalam wa Lugha na itifaki za Kiserikali, kauli ya mambo sasa ni utovu wa nidhamu si tu kwa Mkuu wa nchi Bali kwa Amiri Jeshi Mkuu.

Mambo sasa alipaswa kusema "maneno yaliyosemwa na Mkuu ya nchi si ya kupuuzwa bali yanapasa kitutafakarisha kama kuna sehemu tumekosea au tulikosea tujisahihishe". Hiyo ingekuwa kauli ya Afisa wa Jeshi kwa amiri Jeshi Mkuu.

Otherwise Mambosasa anapaswa kuchukuliwa hatua stahiki, tusubiri tuone!

Sent using Jamii Forums mobile app
Unaongea sahihi lakini pia kwa upande mwingine inawezekana Mambosasa anajua kua yeye anashushiwa tu lawama. Ndo mana anasukumia mpira kwa viongozi wa juu. Mana inawezekana anajua vizr mchezo ulivyokua ila yeye alipewa tu asimamie. Ndo mana amejaribu kuyakwepa maswali kwa kuwatuma kwa mabosi wake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uchunguzi uliishia kwenye kunywa chai hats sinema za kihindi siyo hivyo?...Kuna jambazi tekaji tena linaloteka mtu mzima sio mtoto tena tajiri ajulikanae Afrika anaweza kushindwa kuchoma gari kweli zaidi linakuachia na silaha bila ambush yoyote?!!?
hahahahahaaaaaa dah.... mambokale!!
 
Kuna shida kubwa unaweza kuta kuna implications za watu wasiweza kushtakiwa wapo juu ya sharia.
 
Tumeelezwa juzijuzi kwamba inashangaza kuona Mo ametekwa halafu alipoonekana anakunywa chai na Mambosasa. na kwamba watanzania siyo wajinga.

Tafsiri nyingi ni kwamba huenda kitendo hicho kikamwajibisha mtu yeyote ndani ya polisi na ikibidi mtu kutumbuliwa katika jeshi la polisi.

Ninachotaka kusema nanieleweke ni hiki. Katika hili tumesikia Mambosasa akisema faili liko wapi. Lakini mpaka mkuu anasema vile hadharani ni wazi kutumbuliwa kuna uwezekano usipuuzika.

Sasa, inaonekana kama polisi inataka kupata au inaelekea kupata sympathy (huruma) ya wananchi.

Sisemi polisi hawana haki katika hili. Binafsi sijali kama wakuu wa polisi wana haki au hawana haki. Sijali kwa sababu polisi maeneo yoyote hata mtaani wamekuwa ni watu ambao hatutakiwi kuwaonea huruma.

Ukikaa kwenye maongezi mtaani akitokea polisi kazi yake inakuwa kutetea serikali hata kwenye uonevu ambao hutarajii itetewe. Kimsingi kazi ya polisi imekuwa kama ni kuvuruga mijadala na kukaa upande wa serikali.

KWa maana hiyo polisi wameudhi wananchi wengi ka miaka mingi. Wananchi wanaonewa, polisi inakingia.

Sasa polisi yanawafika kuhusu hili la Mo. Ninaweza kuamini kwamba jeshi la polisi linaonewa. Ninachogomba ni kwamba pamoja na kuonewa hatuna sababu ya kuwahurumia. Waache kiwakute cha kuwakuta.

KAma ni kutumbuliwa maafosa wa ngazi za juu wa polisi basi acha watumbuliwe warudi mtaani. Na huko mtaani waendeleze stori za kuitetea serikali hata katika kutumbuliwa kwao.

Sasa katika hili polisi watataka watetewe hata na CHADEMA, ACT. Kwa sababu ipi? Wapinzani wanapobanwa polisi wanakuwa upande gani.

Wito wangu ni kwamba tuacheni polisi waubebe msalaba wao. Sisi hawakuishia kutuacha kuubeba msalaba tunapoonewa, badala yake walitutwisha hata taji la miiba kichwani kuongezea mateso ya msalaba.

Mwisho waswahili wanasema mwosha maiti naye ikifika kifo chake huoshwa. Acha polisi watumbuliwe ikibidi na ikitokea hivyo tufanye sherehe kote.
 
Polisi wetu hawafanyi kazi zao kwa weledi tena, wamebaki kupokea maagizo na kutenda bila hata kutafakari!
 
Back
Top Bottom