Mambosasa ajibu maswali ya Rais Magufuli kuhusu kutekwa Mo Dewji

Kiofisi ni vizuri boss au junior kuwasiliana kiofisi kulikoni kujibizana au kutuhumiana hadharani .Naona kuna kitu hakiko sawa.Public sio ofisi.Mafaili yapo boss aandike junior ajibu.Haya mambo ya kuanikana hadharani na kujibizana hadharani kati ya mabosi na ma subordinate wao ni ukosefu wa nidhamu za kiofisi na lazima ukataliwe usiote mizizi . Taratibu za mawasiliano ya kiofisi yaheshimiwe na yatumike kwa wote mabosi na juniors.Kitu haliko sawa uliza kiofisi ujibiwe na junior kama kuna kitu hukioni sawa kiekezee kiofisi.Ndio maana vyuo vyote hufundisha business communication kwa kozi zote za sayansi na Arts ili zitumike zaidi
Kwahiyo hapo mwenye kosa ni presder au mambo sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TUMBUA MAMBOSASA, HANA NIDHAMU, anawezaje kumjibu mkuu wa nchi hadharani hivyo halafu kihuni.. Protoka ilimtaka aende kwa bosi wake Sirro akamwambie alipoishia halafu akae kimya, TUMBUA MAMBOSASA HANA NIDHAMU..
Shida ni kwamba rais hakutakiwa kuuliza hilo swali pale angeenda kuwauliza baadae ila ndo hayo unamwaga mboga namwaga ugali ngoma inogile

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi wazungu ndio nasubiri aisee. Kwani waliomteka ni wazungu raia wa wapi tena!
 
Ame
Siku chache baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli kuibua maswali juu ya tukio la kutekwa Mfanyabiashara Mohamed Dewji Kamanda wa Polisi Dar es salaam Lazaro Mambosasa amejitokeza na kusema yeye alishamaliza kazi yake.

Mambosasa amesema baada ya yeye kumaliza kazi yake alikabidhi kwa viongozi wake wa juu na kwa sasa wanaojua kinachoendelea ni Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ambaye anatakiwa kutoa taarifa za uchunguzi zilizowasilishwa kwake.

Mambosasa amesema, “kuhusu maelekezo ya Rais aliyoyatoa kuhusu kutekwa kwa Mo, maadamu aliyatoa mbele ya Mkuu wetu wa Jeshi la Polisi na DCI ambao walikuwepo, jalada hilo lilishafika kwao, huko ndiko wanakojua kinachoendelea".

“Mimi jukumu langu lilishakwisha kwa hiyo ni suala la maamuzi ya juu kuhusu hatua zilizofikiwa kwenye jalada hilo", ameongeza Kamanda Mambosasa.

Mapema juzi Ikulu akiwaapisha Makamshna wa juu wa Jeshi la Polisi, Rais Magufuli alisema, "Jeshi la Polisi linatakiwa kuelewa kuwa Watanzania sio wajinga, kama suala la kutekwa kwa Mo Dewji linaacha maswali, tuliambiwa alitekwa na wazungu lakini lilipoisha haikueleweka, mwishoni aliyetekwa alionekana anakunywa chai na Mambosasa."
Amemjibu rais?

Pole yake
 
kuna afande alisema atahakikisha waliomteka mo wanakamatwa wakiwa hai au wamekufa sijui ameamua kuwapotezea
 
Kwetu sisi wataalam wa Lugha na itifaki za Kiserikali, kauli ya mambo sasa ni utovu wa nidhamu si tu kwa Mkuu wa nchi Bali kwa Amiri Jeshi Mkuu.

Mambo sasa alipaswa kusema "maneno yaliyosemwa na Mkuu ya nchi si ya kupuuzwa bali yanapasa kitutafakarisha kama kuna sehemu tumekosea au tulikosea tujisahihishe". Hiyo ingekuwa kauli ya Afisa wa Jeshi kwa amiri Jeshi Mkuu.

Otherwise Mambosasa anapaswa kuchukuliwa hatua stahiki, tusubiri tuone!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mpk hapa tunapoongea impact tayari mkuu
 
wale wahalalisha pombe, wanapenda sana kutumia hayo maneno.
bible ya vitabu 72 sijui ilitoka wapi, maana wakristo wengine wote wanatumia bible ina vitabu 66.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ungeuliza hivi, 'Biblia yenye vitabu 66 ilitoka wapi maana Biblia iliyotangulia ilikuwa na vitabu 72; je ni nani aliyevipunguza na kibali cha kuvipunguza alipewa na nani?

Ha ha huna utaalamu wowote ndugu. Hivi unajua maana ya official correspondences?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nadhan kuna kitu kinatokota nadhan kuna mvujo wa issue nzima mahali sasa watu wanaanza ku pre empty kwa kujaribu kuji distance!
ili mvujo ukidondoka halafu mtu aseme hata mm nilikuwa nataka majibu ya hili suala!muda utasema ila naamini kuna tundu sehemu wata wanajaribu kulimaintain na nina was was hilo tundu linaweza kuleta mazingira magumu 2019-2020 katika yale mambo yetu ya kuchaguana!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
huyu jamaa ndoa atakuwa chambo......soon ataenda kuwa katibu tawala namtumbo.....
 
Mimi hii nchi hainivutii kwa kweli😁😁😁
VIONGOZI Wana Matukio. Kwa hiyo ulikuwa wapi kutujulisha hayo,Na kwa Nini wajibu wenu mnataka Hadi Raisi awashtue
Cha Ajabu Kama Ni mwana siasa wa upinzani angeyasema Yale yaliyosemwa na Raisi kwa Sasa bila Shaka angekuwa chini ya ulinzi kwa kuwa lazima mngesema kuuliza habari za Kutekwa watu Ni uchochezi🤣🤣🤣🤣
 
Siku chache baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli kuibua maswali juu ya tukio la kutekwa Mfanyabiashara Mohamed Dewji Kamanda wa Polisi Dar es salaam Lazaro Mambosasa amejitokeza na kusema yeye alishamaliza kazi yake.

Mambosasa amesema baada ya yeye kumaliza kazi yake alikabidhi kwa viongozi wake wa juu na kwa sasa wanaojua kinachoendelea ni Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ambaye anatakiwa kutoa taarifa za uchunguzi zilizowasilishwa kwake.

Mambosasa amesema, “kuhusu maelekezo ya Rais aliyoyatoa kuhusu kutekwa kwa Mo, maadamu aliyatoa mbele ya Mkuu wetu wa Jeshi la Polisi na DCI ambao walikuwepo, jalada hilo lilishafika kwao, huko ndiko wanakojua kinachoendelea".

“Mimi jukumu langu lilishakwisha kwa hiyo ni suala la maamuzi ya juu kuhusu hatua zilizofikiwa kwenye jalada hilo", ameongeza Kamanda Mambosasa.

Mapema juzi Ikulu akiwaapisha Makamshna wa juu wa Jeshi la Polisi, Rais Magufuli alisema, "Jeshi la Polisi linatakiwa kuelewa kuwa Watanzania sio wajinga, kama suala la kutekwa kwa Mo Dewji linaacha maswali, tuliambiwa alitekwa na wazungu lakini lilipoisha haikueleweka, mwishoni aliyetekwa alionekana anakunywa chai na Mambosasa."
Aki ccm hawana akili timamu, wao ndio walimuteka MO kisha wanajiuliza maswali, acheni kutuona kaa sisi ni mazuzu kaa nyinyi
 
Asante kwa kunikumbusha, nasubiri hiyo part 2 nione kama starring atabaki huyo huyo au atauwawa
Huyu hawezi kuuawa mpaka mzee baba atakapotuliza akili....
 
Kiofisi ni vizuri boss au junior kuwasiliana kiofisi kulikoni kujibizana au kutuhumiana hadharani .Naona kuna kitu hakiko sawa.Public sio ofisi.Mafaili yapo boss aandike junior ajibu.Haya mambo ya kuanikana hadharani na kujibizana hadharani kati ya mabosi na ma subordinate wao ni ukosefu wa nidhamu za kiofisi na lazima ukataliwe usiote mizizi . Taratibu za mawasiliano ya kiofisi yaheshimiwe na yatumike kwa wote mabosi na juniors.Kitu haliko sawa uliza kiofisi ujibiwe na junior kama kuna kitu hukioni sawa kiekezee kiofisi.Ndio maana vyuo vyote hufundisha business communication kwa kozi zote za sayansi na Arts ili zitumike zaidi
Aisee, sikujua kama huwa una hoja za maana namna hii. Sasa yale madudu ya hovyo hovyo unayoandika wakati mwingine huwa umejitoa ufahamu au umezidisha mvinyo? Kilangila.
 
Siku hazifanani mkuu
 
Kwetu sisi wataalam wa Lugha na itifaki za Kiserikali, kauli ya mambo sasa ni utovu wa nidhamu si tu kwa Mkuu wa nchi Bali kwa Amiri Jeshi Mkuu.

Mambo sasa alipaswa kusema "maneno yaliyosemwa na Mkuu ya nchi si ya kupuuzwa bali yanapasa kitutafakarisha kama kuna sehemu tumekosea au tulikosea tujisahihishe". Hiyo ingekuwa kauli ya Afisa wa Jeshi kwa amiri Jeshi Mkuu.

Otherwise Mambosasa anapaswa kuchukuliwa hatua stahiki, tusubiri tuone!

Sent using Jamii Forums mobile app
Ashajua wazi hili halimuachi kwahiyo anatapika tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom