Mamelodi Sundowns wako Overrated

kama Mamelodi Sundowns wapo overrated sijui Simba wapo over nini, Raja kapumzisha wachezaji 5 bado kafanya mabalaa let's be realistic
 
kama Mamelodi Sundowns wapo overrated sijui Simba wapo over nini, Raja kapumzisha wachezaji 5 bado kafanya mabalaa let's be realistic
Tutajie hao wachezaji watano waliopumzishwa na Raja
 
Watanzania huwa tuna tabia ya kutishana na kutiana unyonge lakini Mamelodi Sundowns kwa aina ya mpira wake anaocheza ni rahisi zaidi kwa Simba kumdhibiti kwani anatabirika zaidi. Simba wakiwa na tahadhari na nidhamu ya hali ya juu wanaweza kuwatoa.Muhimu ni kujipanga tu.

Waarabu huwa wanampatia kwenye hatua za mtoano kwa kumchezea compact football.Aina hii ya mpira humsumbua sana na mara zote ameangukia pua kwa aina hii ya mpira alipokutana na waarabu kuanzia msimu wa 2016/2017 hadi 2020/2021 na msimu wa 2021/2022 wale Waangola walimtoa kwa aina hii ya mpira.

Kumbuka katika misimu yote hii, ni msimu wa 2018/2019 pekee ndiyo aliweza kufanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali na msimu wa 2017/2018 hakuweza kuvuka hatua ya makundi. Katika misimu yote hii walikuwa na wanaendelea kuwa na kiwango bora.

Waarabu kwenye hatua za mtoano hucheza kwa nidhamu na tahadhari ya hali ya juu na wana uzoefu wa hatua hizi.Iwe nyumbani ama ugenini. Sisi timu zetu huwa tunapungukiwa vitu hivi. Tp Mazembe kwenye ubora wao alikuwa navyo hivi vitu na alifanikiwa kuwamudu haswa hawa waarabu.!!!!!!!!!!

Nb 1 : Aina yao ya mpira haipishani sana na Simba.

Nb 2: Mamelody wanafanana kwa mbali na Manchester city kwa aina yao ya uchezaji.

Nb 3: Compact ndiyo njia nzuri kwa aina ya hii ya mpira.Pep Guardiola ameweza kuja na suluhisho kwa kuweka watu ambao wanaweza kuivunja compact, hao watu Mamelodi hana.!!!!!!!!!!!!

Nb 4: Mpira ni sayansi na umeenea karibu maeneo yote, zama za kutishana zimepitwa na wakati.

Nb 5 : Hatua za mtoano zina aina ya uchezaji wake na hazifanani na hatua za makundi.

Nb 6 : Timu za kiarabu ndiyo wapinzani halisi wa hili kombe. Naamini mojawapo zitafanikiwa kuchukua ubingwa, ingawaje mpira una maajabu yake na ni sehemu yake.

Ni mtazamo tu!!!!!!!!!!!!!
 
Kongole mkuu, umemaliza kila kitu [emoji122]
 
Well said mkuu
 
Mamelodi kampiga mwarabu 4 kwao
 
Watu wa kutazama mechi moja halafu wanafikia hitimisho...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…