Mamelodi Sundowns wako Overrated

Mamelodi Sundowns wako Overrated

Hakuna cha ku-edit mkuu, ndo uhalisia Mamelodi wako Overrated sana ukilinganisha na wanacho kionesha uwanjani, ni mara 10 ungeniambia Raja CA
Kama Simba atashinda game yake na Raja Casablanca ugenini nita amini huu uzi wako
 
Mimi ni Simba lialia ila kiukweli wale jamaa ukiwaangalia wanajua Kuna mtu anaitwa Maema ,Mailula na Peter wale jamaa ndo injini pale kwa huu mpira wanaocheza labda Raja kidogo msimu huu ndo wako sawa ila jamaa wako far beyond us.
Mkuu kama kwa mtazamo wako Mamelodi ni bora zaidi ya Raja, basi unahitaji kukaa chini ujifunze mpira
 
Al ahly ya mwaka huu umeiona au unaongea tu kwa historia ?
Kama hautaki tuongee history basi usijilete habari ya Mamelodi kuishia robo kila mwaka maana tunarudi kule kule kwenye history
 
A very lame comparison. Hapa tunawalinganisha Mamelodi na Simba, sio Mamelodi na Al Hilal.

Lakini pia hata tukiamua kufanya hivyo unavyotaka, kwani hukuona malalamiko kwamba Mamelodi wanafanya match fixing kwa kuwalegezea Al hilal makusudi ili Al Ahly atoke?

Ikitokea Mamelodi akapangiwa Simba, basi ni do or die kind of a match kwa Mamelodi. Usitegemee wacheze kama walivyocheza na Al Hilal kwenye makundi ambapo wao tayari walikua na uhakika wa kufuzu!

Inahitaji kiwango cha juu sana cha kujitoa fahamu kuwaweka Mamelodi hawa, na Hii simba kwenye level moja!

Mechi ya kwanza ya Mamelodi vs Al Hilal kule south africa nayo ilikuwa mechi fixing ili Al Ahly atoke ? Ndio ilikuwa mechi ya kwanza ya group kwa timu zote zina 0 point.

Kumbe unalijua hilo kuhusu comparison haitakiwi

Why useme simba atafungwa nyingi na mamelodi ?

Huku hujawai kuona simba na mamelodi wakicheza hata siku moja ?
 
Itoshe kusema waarabu wataendelea kubeba sana ubingwa wa champions league. Simba na huyo Mamelodi ni wasindikizi tu. Mabingwa wanajulikana.

Tatizo kubwa la Simba ni jinsi ya kucheza ama kushinda au kuzuia kufungwa michezo ya ugenini kwa margin kubwa ya magoli kwenye mechi za mtoano. Siku tiba ikipatikana tutafika mbali.
 
Anakuja mtu, anakuambia Mamelodi ni wa kawaida. Ukimuuliza sababu, anakuambia habari za misimu iliyopita. Sijui mnatumia viungo gani kufikiri!

Mamelodi anaeongelewa hapa ni wa msimu huu. Mamelodi ambae yuko kwenye ubora wa hali ya juu. Kabisa mnategemea akina Onyango wawavushe kwa Mamelodi aliemtandika Al Ahly tano? Hamko serious!
Hata wewe mwenyewe unapomtaja al ahly ni kama una m-picture Al ahly wa misimu iliyopita, wale jamaa msimu huu wabovu, angekula 7 kwa mkapa kama angepangwa na Simba.
 
Kama Simba atashinda game yake na Raja Casablanca ugenini nita amini huu uzi wako
Hata wewe mwenyewe unapomtaja al ahly ni kama una m-picture Al ahly wa misimu iliyopita, wale jamaa msimu huu wabovu, angekula 7 kwa mkapa kama angepangwa na Simba.

Pia Mamelodi vs Al ahly south africa mechi imeanza kuchezwa saa 9. Jua bado kali. AL Ahly na jua wapi na wapi.

Hizo 5 angekuwa amemfungia misri ingekuwa na nguvu. Ama angemfunga muda wa usiku.

Hata Simba angecheza na Raja casablanca saa 9 kwa jua la dar. Raja casablanca hasingeshinda mbele ya mnyama kwa mkapa
 
Simba angekua anacheza huo mpira unao usema angekua kafika final hata moja kumbuka mara mbili katolewa ni timu za SA (Orlando pirates na Kaizer Chiefs) wala sio Northern huko kabla ya kujigamba kumtoa Mamelodi ungejiuliza kwanini Simba hua anaishia robo?
Kwani Simba huo mpira wa matokeo kaanza lini ?
 
Kama Simba atashinda game yake na Raja Casablanca ugenini nita amini huu uzi wako
Hakuna simba anachohitaji kwenye hii game kwani tayari ameshafuzu, hivyo anakwenda kukamilisha ratiba tu, na hata ikitokea simba ameshinda au draw bado mtakuja na vijisababu kuwa Raja amechia kwakuwa hakuna anacho hitaji
 
Kama hautaki tuongee history basi usijilete habari ya Mamelodi kuishia robo kila mwaka maana tunarudi kule kule kwenye history
Kama ulisoma vizuri uzi wangu, nilisema nimewaona mamelodi kwenye game zao kadhaa za makundi msimu huu,, sijazungumzia miaka fulani iliyopita..
 
Kwani Simba huo mpira wa matokeo kaanza lini ?
Kwanza huo mpira wa matokeo ni wa aina gani? sababu me nnacho fahamu kwenye makundi panahitaji matokeo ili upite kwenda next round sasa hayo matokeo unayosema sijui ni yapi
 
Kwanza huo mpira wa matokeo ni wa aina gani? sababu me nnacho fahamu kwenye makundi panahitaji matokeo ili upite kwenda next round sasa hayo matokeo unayosema sijui ni yapi
Ni direct football ambayo tumeanza kucheza msimu huu
 

Habari wakuu

Awali ya yote ningependa ku-declare interest kuwa nawataka Masandawana. Twende kwenye mada, imezuka mijadala mingi sana mitandaoni hususani kwa baadhi ya wachambuzi wakisema kuwa Mamelodi sundowns sio timu ya kuomba kukutana nayo. Wengine wakaenda mbali zaidi kusema kuwa ndio timu hatari zaidi.

Binafsi naheshimu ubora wa Mamelodi, nilipata wasaa wa kutizama game zao mbili tatu hususani ile game yao ambayo walimpiga Al ahly hamsa pale Africa kusini. Naomba niseme tu kwamba Mamelodi wako Overrated mno.

Nadhani ni kwa sababu ya kumnyanyapaa Al ahly ndicho kinachofanya watu wamzungumzie kiutofauti, ambapo obviously hajaanza leo toka kitambo al ahly anapotua Johannesburg basi Hamsa zina muhusu.

Lakini ni ukweli usiopingika kuwa al ahly pia msimu huu hayupo vizuri, kinacho mbeba ni uzoefu tu ila hana timu, nisingeshangaa angepigwa nje ndani na mnyama simba kama angepangwa group moja.

Turudi sasa kwenye mada yetu, Mamelodi sundowns pamoja na kuwa Overrated sana bado hana mpira wa kutisha, nachelea kusema kuwa hata Raja CA ni maji marefu kwa Mamelodi. Kingine nilichokiona kwa Mamelodi ni aina yao ya uchezaji ambao uko very identical na uchezaji wa simba yani pira biriani a.k.a Sambaloketo.

Hivyo ikitokea timu hizi mbili zikakutana, basi Africa na Dunia kiujumla itashuhudia mechi ya karne, yani historical match, hivyo niwatoe hofu wanasimba wenzangu ambao mmeanza kutishika na maneno ya waganga njaa kuhusu Mamelodi sundowns.

Binafsi sintoshangaa kabisa kama simba akimtoa Sundowns kwenye hatua ya Robo fainali au hatua yoyote tutakayo kutana nae.

Nguvu moja [emoji881]
Kuhusu kuwa overated Sawa, Ila hayo mengine Baki nayo.
 
Ilikuwaje wakawa wanaishi robo fainali kwa misimu mitano mfululizo?

Haohao mwaka jana walitolewa na Petroleos, ilikuwaje?
Kawaida Kwenye michezo hutokea kama unawaangalia Sundowns unaeza fananisha quality ya wachezaji wako nao past 3 season na hii ya msimu huu?
 
Mkuu kama kwa mtazamo wako Mamelodi ni bora zaidi ya Raja, basi unahitaji kukaa chini ujifunze mpira
Naona wewe umekua ndo mtoa degree ya Kipimo cha kufahamu mpira si ndio ?
Soma vizuri nilichoandika ,nimekwambia kwa msimu huu team yenye quality ya kuperform zaidi ya Mamelodi ni Raja..
Halafu huyu Raja ndio huyu aliecheza na Horoya ,vipers na Hii simba ?
 
Back
Top Bottom