Frank Wanjiru
JF-Expert Member
- Apr 12, 2012
- 22,719
- 40,739
Pichani ni mchezaji wa Cape Town spurs akimchezea rafu mshambuliaji wa Mamelodi Sundowns Peter Shalulile nje ya box ambapo jambo lililostua wengi na kuzua taharuki ni kwamba mwamuzi wa mchezo huo aliamuru penalti iliyowapa ushindi wa goli 1 Mamelodi Sundowns.
Penalti hiyo imekuwa gumzo kubwa mitandaoni nchini Afrika Kusini mashabiki wa soka wanasema Mamelodi Sundowns inaua soka la Afrika kwa kutumia waamuzi kushinda mechi zake. Huu ni ushahidi mwingine kwamba kukataliwa goli halali la Aziz Ki haikuwa bahati mbaya, ulikua mpango wa makusudi kabisa na klabu ya Mamelodi Sundowns imehusika.
Tukio la jana limeibua hasira kali huku mashabiki wengi wakitaka shirikisho la soka Afrika CAF kufanya uchunguzi mkali dhidi ya klabu ya Mamelodi Sundowns pia wakitaka mmiliki wa klabu hiyo ambaye pia ndio rais wa CAF bilionea Patrick Motsepe kuachia ngazi mara moja kwakua inawezekana ndio mastermind wa matukio haya ya upangaji matokeo ya Mamelodi Sundowns
Ni dhahiri sasa kibaka Mamelodi Sundowns amedakwa hadharani tena akiiba msikitini awamu hii hachomoi, hii unaitaje penalti mdau?