JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Wakati Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) ikiendelea kutoa vibali vya daladala kutoka maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam kuelekea eneo la Kawe lililopo ndani ya Jiji hilo lakini katika hali ambayo inaleta mtanzuko sehemu hiyo ni muda sasa imeendelea kukosa stendi yenye hadhi ambayo inaweza kuwa rafiki kwa abiria pamoja na madereva.
Kwa udadisi kutoka kwa wenyeji wa eneo la Kawe ikiwemo wapiga debe na madereva ni kwamba kwa jumla kwa siku daladala takribani 100 utoa huduma kwenye eneo hilo, kwa kuingia na kutoka.
Daladala zinatoa huduma kwenye eneo hilo zimekuwa zikipaki kwenye maeneo 'bubu' ambayo kimazingira sio maeneo rafiki yanayoweza kutambuliwa moja kwa moja kama stendi.
Daladala hizo utokea njia ya njia ya Mwenge na Tegeta maarufu 'Bagamoyo road' ambayo upaki kwenye stendi Bubu ambayo ipo eneo linalotanbulika kama kwa Mwamposa mkabala na Kituo cha mafuta cha Lake, lakini daladala zinazotokea barabara ya Mwai Kibaki upaki barabarani eneo la Kawe Ukwamani.
Maeneo hayo yote sio rafiki, ambapo katika eneo la Kawe Ukwamani daladala hizo zimekuwa chanzo cha foleni kutokana na kupaki eneo la barabara pamoja na kugeuzia eneo hilo ambalo kiuhalisia madereva wanadai kuwa ni finyu hususani kwa magari makubwa yanatoa huduma kwenda Mbagala.
Licha ya hivyo abiria na watu wanaofika eneo hilo wanajikuta katika mazingira yasiyo rafiki kutokana na magari ambayo ujazana kwenye maeneo ya barabara bila mpangilio huku waendeshaji wa magari binafsi wakidai kukubana na changamoto eneo hilo, lakini ikizingatiwa eneo katika eneo hilo kuna maduka ambayo yapo pembezoni mwa barabara ambapo wahusika nao upata changamoto wanapotaka kushusha au kupakia bidhaa zao.
Eneo la Kawe kwa Mwamposa limekuwa kero kubwa sana hasa kipindi cha mvua huku abiria wakipata changamoto ya kukosa maeneo rafiki ya kungojea usafiri hasa wakati mvua zikiwa zinanyesha au kipindi cha jua kali.Katika eneo hilo kuna mashimo ambayo yamejaa maji machafu ambayo upelekea abiria kupata kadhia kubwa.
Kadhia hiyo kwa sasa imedumu kwa muda mrefu, ambapo kwa mara kadhaa wananchi wamepaza sauti zao kwa mamlaka lakini mpaka sasa hakuna jitihada za wazi ambazo zinaonekana kufanyika kutatua kero hiyo.
Hoja inayobeba andiko hili ni kwamba Serikali kupitia mamlaka zake zimeshindwa kupata eneo la kujenga stendi ya daladala ikizingatiwa eneo hilo linaonekana kuwa na abiria wengi pamoja na mwingiliano wa Watu.
Wito wangu ni vyema mamlaka zikaeleza wazi juu jitihada zinazofanyika kuhusu utekelezwaji wa ombi la Wananchi ambalo limekuwa likitolewa mara kwa mara, ukimya bila utekelezaji unaibua maswali yasiyo na majawabu rasmi kuhusu uwajibikaji.