Mamlaka husika chunguzeni hili la Ziwa Nyasa

Mamlaka husika chunguzeni hili la Ziwa Nyasa

Shida ni jina au mpaka mahali ulipo?
Vyote viwili! Jina la ziwa siyo haki miliki ya Malawi, mabadiliko yo yote lazima yashirikishe nchi zote.

Mpaka upo katikati ya ziwa na siyo huo mpaka fake uliowekwa hapo. Ndiyo sababu Malawi imefungua kesi mahakama ya kimataifa kutaka kuuhamisha na kuuweka pembeni!
 
Lakini kwanini mpaka uonekane kulimega ziwa lilopo upande wa Tz, mbona kwa wenzetu Msumbiji mpaka wa ziwa upo sawa tu?
Huo ni mpaka fake! Ndiyo sababu Malawi imefungua kesi mahakama ya kimataifa kutaka kuuhalalisha!

Mpaka rasmi upo katikati ya ziwa.
 
View attachment 2109716


Katika kuperuzi peruzi kwenye google map nimeshtushwa kuona mpaka na jina la ziwa Nyasa vikionekana kama nilivyoattach hapo juu. Hii imekaaje wadau? Naomba mamlaka husika itupe ufafanuzi. Nawasilisha.
Ndivyo huwa inachorwa siku zote na hata hilo Ziwa linaitwa Ziwa Malawi.

Hiyo mipaka ilitumiwa na wakoloni ila baada ya Uhuru Mwl.Nyerere ndio alibadili ikawa kama unavyoona kwenye ramani zinazochapishwa na Tzn.
 
hichi kitu kina nishangaza sana
Ingawaje ziwa ni letu pia......ila hata kama lisingekuwa letu yaani nimepakana nalo halafu nisilitumie??

Hapo cha kufanya majeshi yote Tz hadi ya zimamoto ikiwezekana yatumwe malawi washikishwe adabu vizuri
Lenu na nani? Mgogoro upo miaka yote na Malawi Kuhusu mipaka.
 
Vyote viwili! Jina la ziwa siyo haki miliki ya Malawi, mabadiliko yo yote lazima yashirikishe nchi zote.

Mpaka upo katikati ya ziwa na siyo huo mpaka fake uliowekwa hapo. Ndiyo sababu Malawi imefungua kesi mahakama ya kimataifa kutaka kuuhamisha na kuuweka pembeni!
Kwa nini hamkutokea mahakamani?😁😁
 
Lakini kwanini mpaka uonekane kulimega ziwa lilopo upande wa Tz, mbona kwa wenzetu Msumbiji mpaka wa ziwa upo sawa tu?
mipaka ya ziwa nyasa iliwekwa na wakoloni wa kijerumana na waingereza, kama inavyo onekana kwenye ya google map, wakati wa ukoloni wao waingereza wali iheshimu mpaka unao lipeleka ziwa nyasa loote kwa Malaw. Na sisi waTZ baada ya uhuru tulilala usingizi wa pono badala ya kuchukua hatua stahiki mapema, sasa hii blunder ya wakoloni inaanza kutu costs
 
Ukienda mahakama yoyote ya kimataifa ziwa Nyasa ni la Malawi. Hakuna nchi ya Afrika ilijigawia mipaka, mipaka iliyowekwa na wakoloni ndio tunatumia. Heligoland Treaty ya mwishoni mwa karne ya 19 inaonyesha hilo ziwa Malawi liko Malawi lote. Hata ukisoma ramani za Kijerumani wanajua walivyogawa Ziwa huwa wanaliweka Malawi lote.

Hata hivyo kuna treaty nyingine baina ya Waingereza na Wajerumani inayosema kila nchi inayopaka na chanzo cha maji haitakiwi kunyimwa sehemu ya chanzo hicho. Malawi wana documents zinazoonesha ni ziwa lao na sisi hatuna.

Waliotengeneza ramani sio Malawi ni Google ambao wanatumia ramani za kimataifa. Ni Tanzania tu tunaojua ziwa Nyasa lina kipande chetu
 
Bila hao watu kupigwa hawawezi elewa

Hizi ni dharau za wazi wazi

Inabidi TPDF wakajifanye kama wanafanya drill kule mbinga

Hao wanyasa wanatafuta kitu
 
Ziwa sio mlima ,maji ya ziwa huongezeka na kupungua.Kando kando mwa hilo ziwa kuna miundombinu ilihamishwa kutokana na eneo la maji ya ziwa kuongezeka.

Sasa wanaosema ziwa lote ni mali ya Malawi mnamaanisha yale maji au kuna eneo limeainishwa? Kama ni maji basi hao walioweka mipaka hawakuwa sawa kiakili maana muda wowote eneo la maji linaweza kuongezeka au kupungua.
 
Maji mengi yanayojaza hilo ziwa yanatoka Tanzania, cheki mto Ruhuhu n.k , tunajaza maji kibao hivyo tunaweza sababisha mgogoro mkubwa sana tukipunguza maji yanayoingia ziwani tukayatumia kwa shughuli nyingine.
Bifu la Ethiopia na Misri litakuwa cha mtoto. Hivyo sisi tumeshika kwenye mpini.
 
Back
Top Bottom