Mamlaka husika watazame vivuko kwa ukaribu zaidi

Mamlaka husika watazame vivuko kwa ukaribu zaidi

Siri ya sifuri

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2018
Posts
2,335
Reaction score
1,967
Salaam wakuu;

Wahenga walisema"Kuhangaika bure sio sawa na kukaa bure,tena wakasema tembea uyaone.

Naam, leo nilikuwa na vijisent vyangu vilivyotosha kwa nauli ya kwenda mahala fulani na kunirudisha nilipotoka, huyoo kwenye daladala za kigamboni kutokea Tandika safari ikaanza,Daresalaam nzuri bwana asikwambie mtu kitu!

Kwasisi ambao tunatokea mikoani tunapotembea ndani ya jiji ndio kwanza tunajihisi tupo duniani!

lakini kama kawaida vizuri navyo havikosi kasoro,nilipofika kigamboni kwa namna jiji linavyopendeza na kuvutia nikaona bora nivuke kuliko kurudi Tandika kwa njia niliokujia ili niendelee kushangaashangaa na kupunguza ushamba! Ilishakuwa usiku na giza lilishatanda.

Mara pap! Moyo ukaanza kudunda, taratiiibu na kwatahadhari nikaelekea kudandia Panton (ferry)sio yale makubwa, mv magogoni niliyoyazoea, kuna mengine mawili madogo madogo na lile nililopanda lilishajaa watu kwenye viti vyote lakini bado kuna umati wa watu wengine wanatiririka kulipanda hilohilo!tukajaa top, chombo kikang'oa nanga.

Roho mkononi lakini kama watalii vile! Hofu yangu ikarudi tena pale tulipokaribia kufika kwenye upande wa pili, kabla lile pantoni halijapaki vizuri darajani abiria wale waliosimama wakaanza kusukumana kusogea mbele na wale tuliokaa tukaanza kusimama,sasa wote tukawa kwenye hekaheka kila mmoja anataka kuwahi kushuka yeye, mbaya zaidi yule baharia anaesimamia abiria bado hajaruhusu watu washuke kwasababu Pantoni halijakaa sawa darajani.

Ni hatari,hatari sana. Lakini kama ilivyo ada kwa mamlaka zinazohusika kukaa kimya mpaka maafa yatokee,kama hali itaendelea vile basi tujiandae kwa vilio.

(Tenda wema uondoke,malipo kwa Mungu)
 
sijaona maana ya "mkaa bure sio sawa na mtembea bure"

economically ume gain nini katika safari yako?
Sikuzalisha chochote lakini nimepata faida kiafya,nimeongeza ufahamu,nimeburudika na nimetenda wema (ihsan)kwa kugundua mazingira hatarishi kwa jamii na kuyazungumzia.
Vipi mkuu, unazichukuliaje faida hizi nilizozipata!?
 
kwani linapaki darajani au linafunga ghati ? Nisaidieni nijue secretarybird Dr hyperkid Kiranga
Nimetumia neno "kupaki"ili nieleweke kwa urahisi, halafu yayofunga gati ni zile Panton kubwa kwasababu zinasubiri kwa muda mrefu kupakia magari na watu, lakini zile Panton ndogo hazibebi magari, ni watu tu. Kwahiyo likisoza tu, watu wanashuka na hapo hapo wengine wanapakia linaondoka,sijaona likifungwa!.
 
Watanzania kuelekezeka nayo ni ngumu sana, watu kusogelea karibu na kujazana wakati wa kushuka ni kawaida sana kwenye panton.

Ni hatari sio kwamba watu hawajui ila ni vile huko dasalama kila mtu ana haraka.
 
Ooh kumbe Haina ttzo nimekupata vyema
 
Watanzania kuelekezeka nayo ni ngumu sana, watu kusogelea karibu na kujazana wakati wa kushuka ni kawaida sana kwenye panton.

Ni hatari sio kwamba watu hawajui ila ni vile huko dasalama kila mtu ana haraka.
Haraka ya nini!? wakati wengi wanaoenda maeneo hayo wapo matembezini kupoteza muda. Ni kutokujali tu, na wengine kudhani wanachofanya ndio salama.
 
Back
Top Bottom