Habari wana bodi,
Tanzania nzima hakuna wananchi wanapata shida ya usafiri kama wananchi wa Rombo! Kuna ukiritimba gani uliopo kwenye vyombo vya usafiri Rombo? Kwanini wananchi wanateseka hivi na usafiri? Vijana wengine wameamua kutumia pikipiki zao kusafiri kutoka Moshi mjini hadi Rombo kwasababu ya kero ya usafiri. Hivi Rombo hizo Noah pekee ndizo zinafaa kwa safari za Rombo? Usumbufu wao ni mkubwa, maringo mengi, wanavunja sheria za barabarani, nauli wanatoza wanavyotaka,
Mfano January mwaka huu nimetoka Useri kuja Moshi nauli nimelipa shs 7,000 lakini hiyo Noah ilibeba abiria mpaka kwenye buti na mbele wamekaa abiria wawili badala ya mmoja na imesimamishwa na askari kama mara tatu! Kilacha, njia panda sikumbuki na wapi lakini askari hawakuchukua hatua yoyote! Tumekuja hivo hivo mpaka tumefika Moshi! Hivi leseni za usafirishaji LATRA zinaruhusu Noah kwenda umbali mrefu kama huo wa Tarakea mpaka Moshi zaidi ya kilomita 90? Hivi ni serikali imelala ama hizo Noah ni mradi wa viongozi? Kwanini muwatese wananchi? Hili jambo siyo kwamba RTO, RPC, RC wa Kilimanjaro hawajui, siyo kweli DC, DED, na vyombo vya usalama vya Rombo havijui kuna maslahi ya watu yanalindwa lakini wananchi wanateseka.
Hata ajali mbaya sana ya Noah na basi la kampuni ya Ngassere imetokea mwaka jana Tarakea tu lakini bado wenye hizo Noah hata hawajirekebeshi! Kwanini mabasi na Coaster zisitumike kusafirisha abiria route ya Rombo? Mbona Arusha to Moshi is the same distance lakini hakuna hizo Noah? Hivi Noah zilitengenezwa kama chombo cha usafiri wa umma? Kwanini Rombo zisajiliwe kama usafiri mkubwa kwa maelfu ya wananchi wa Rombo? Mahali pa kilometa moja tu mtu analipa elfu moja! Kweli hata kama ni kuwafanya warombo wajinga siyo hivyo. Nitalisemea hili hata kwa Rais Samia hizo Noah kama ni za viongozi ziondolewe ziletwe Moshi to Arusha. Viongozi chukueni hatua. Hasa kipindi cha sikukuu wananchi wanateseka sana lakini serikali ipo, wananchi wanatozwa nauli kubwa na nina imani wapo viongozi wanapelekewa fungu ndiyo maana wanaacha hilo liendelee.
Miaka kama mitatu iliyopita nilisikia mamlaka ilisitisha kusajili Noah zingine ndiyo maana hakuna Noah yenye namba E barabarani hadi hizi za zamani zichakae ziondolewe kwa uchakavu! Hii sijui ni akili gani?! Ni sawa na mchezo wa kurushiana mahindi na nyani shambani kwako! Hizi Noah haziachwi zichakae badala yake zinakarabatiwa kila mara ilimradi plate namba inasoma 'ilisajiliwa' na kwa uchache wake huku hakuna vyombo vingine ndiyo manyanyaso huongezeka na kujipangia nauli, unyanyasaji wa abiria, saa moja wamepark abiria wanaingia gharama za kulala gesti, usumbufu ni mwingi kwa wasafiri wa Rombo hivyo mamlaka husika zichukue hatua ya kuziondoa barabarani kwa vitendo.