KERO Mamlaka husika zichukue hatua za haraka kuhusu usafirishaji abiria halmashauri ya Wilaya ya Rombo

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Bhn bhn

Rombo kabla ya Noah kuja kulikuwa na coaster za rombo to Moshi mjini, nakumbuka moja ya ndeng'aso

Baadae Noah zikaanza kuingia road, zilikuwa sio nyingi, kadri siku zinaenda Noah zikawa nyingi mpka coaster kutoka barabarani,

Noah me nimezipanda sana, hazikuwa na shida maake ilikuwa nyuma mnakaa wanne, katikati wanne mbele kwa wadogo wadg wawili mnafiti fresh,

Ishu inakuja kule watu wana miili mikubwa mikubwa mkiekwa na sisi wenye miili midogo naona kama nabanwa plus zile Kona kulaliana

Baadae zikaja shuttle nazo sii nyingi nika opt kutoka Noah to shuttle, shuttle unakuwa comfortable zaidi,

Ajali ya Noah na bus la ngasere ni ajali tuu sio sababu ya Noah, Noah zimekaa barabarani muda mrefu na ajali utazosikia ni chache Tena chache sana,,

Kutozwa nauli ghali ni kuwa watu ni wachache aseeh unaokuta wanatumia usafiri huo huwezi kuwa sawa na mjini,

Huyo alosema mashati to Tarakea 5k jamaa alimpiga pale nakumbuka las time ni buku mbili, Ila ndo hivyo bhn,

Noah zinawah kwa kiasi chake,
 
kinacholalamikiwa kwenye Noah;
1. Kujaza kupita idadi inayotakiwa
2. Uchakavu wa hizo Noah - angalia hasa seat za abiria. Trafic anakagua bodi na tairi basi!
3. Overspending wakati ni chakavu
4. Kutoza nauli zaidi ya inayokubalika
5. Lugha chafu za madereva
6. Uchache wa hizo Noah

Solution: wafunge kamera kwenye hizo Noah kwakuwa wameshindwa kuwa waaminifu ili abiria akiripoti tatizo ushahidi upatikane
 
Weka coaster yako
 
Inawezkn kwa sasa kwa kipindi Cha nyuma kidg walikuwa vzr, though uliyosema ni sahihi
 
Hii ni kweli kabisa Rombo usafiri ndani ya wilaya nichangamoto sana , pia kutoka Rombo kwenda moshi mjini ndo balaaa ...
Hii adha ya usafiri nadhani pia inachangiwa na uchache wa abiria ndio maana unaona hakuna coaster. Noah wanatoza gharama kubwa sana, hapa ndipo mamlaka zinatakiwa kuingilia kati tuu nadhani mambo yatakua sawa.
 
Rombo jeuri yenu ndio imewafikisha hapo, zamani yalikuwepi ma Bus kama Ndengaso, Tilisho, Manguku, Maktaba Charter na Sun City lakini zilivoanza kuja noah watu wakaona hawana haja ya kusubiri Bus lijae zaidi ya Lisaa wakati Noah dkk 10 imejaa, basi ndio Mwanzo wa ma bus kukosa abiria na wakaamua kutoa mabus yao kupeleka route zenye shida ya usafiri, unaambiwa paka akitoka panya utawala, sasa vinoah na vimini bus maarufu kama shuttle vinafanya vinavyotaka, kutoka Moshi hadi Rombo Km 60 lakini unaweza kufaulishwa kwenye gari hata sita maana kimesusa kuendelea na safari baada ya kuona abiria wengi wakurudi 😂😂.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…