Sawa nitawajengea sehemu ya kuhuisha akili zenu Wananchi wangu.Wakuu,
Ni ajabu sana kuona miji midogo ndani ya majiji haina sehemu zenye utulivu kwa ajili ya watu kupumzika na kutembea, huku wakicheza na watoto wao, wakinywa soft drinks na bites, wakipiga picha na kupumzisha mafuvu yao.
Mji mdogo kama Mbezi-Kimara, kutwa ni shughuli za kiuchumi zinaendelea, kuanzia maduka makubwa hadi wanaopanga nyanya stand, huduma za usafirishaji hadi huduma zetu pendwa usiku wa manane maeneo tofauti kama kwa Gody, kwa Robert(Ngao Pub) na njia ya Kinyerezi.
Sasa kwa nini kusiwe na maeneo ya watu kupumzika, yatengenezwe vizuri, yahudumiwe kwa usafi yavutie wenyeji na wageni? Hizi open spaces nyingi zimegeuzwa maeneo ya biashara ndogondogo.
Watanzania nadhani hatuna huu utamaduni, tukitaka kutoka basi it's either tukutane bar, beach na wengine wetu guest[emoji3], sio kila mtu anapenda kukutana bar. Lakini kuna namna tunaweza kujenga na kutengeneza maeneo mahususi watu wakakaa na kupumzika, kuongea, kupanga na kupangua mambo yao. Mbona hapo Zanzibar kuna sehemu zimejengwa vizuri tu, huku bara sisi tunashindwa nini?
Napendekeza eneo linalotizamana na Magufuli Stand, katikati ya barabara kuu na Stand kuu kuwe na recreation space, ijengwe vizuri, ivutie wageni na wenyeji, yaani sisi tunakuwa wala vumbi tu mda wote kweli?
Sio Mbezi tu, sehemu zote za miji yetu zinahitaji kuwa na mandhari za kuvutia wageni na wenyeji, tuache uchafu jamani, miji yetu ni michafu sana, haivutii, inaongezea watu stress.
Kwani wenye nchi huwa hawasafiri wakaona wenzetu wanafanyaje huko kwao?
Boss pugu forest natamanigi kwenda sijajua kupojeTembelea pugu forest, kuna bamboo trees za maana na camping pia, ukikaa kule akili inajifomati kabisa.....usiache kuja kunishukuru 😉
Kwani wenye nchi huwa hawasafiri wakaona wenzetu wanafanyaje huko kwao?
Pazuri kwakweli, mi nimepapenda sana na gharama ni za kitz kabisa bila tozo.....kulala kwenye tent chini ya bamboo trees imenipa tibaBoss pugu forest natamanigi kwenda sijajua kupoje
Weekend moj nimtoe mtot wa mtu sasaPazuri kwakweli, mi nimepapenda sana na gharama ni za kitz kabisa bila tozo.....kulala kwenye tent chini ya bamboo trees imenipa tiba
Kwa hiyo kumbe shida yetu kubwa ni ustaarabu? Tumekuwa watu wa hovyo kiasi hiki, au ni muendelezo wa watu masikini hawawezi kutunza hata mazingira yao?parks zipo lakin zinapotea kwasababu ya ustaarabu duni wa watanzania, sanasana uchafu
Mkuu, hapa sasa ndio naanza kuelewa. Kumbe pamoja na yote shida yetu kubwa ni kukosa ustaarabu? Hili linaumiza, mbona miaka hiyo Zanzibar(sijui siku hizi) kulikuwa na maeneo mazuri watu wanakaa na kupiga story, wanaenjoy. Tumekuwaje watu wa hovyo namna hii?Halafu sisi swala la ustaarabu ni sifuri hatujastaarabika kabisa, sehemu kama hizo tukijengewa itakua ndio sehemu ya kuvutia bangi, kutupa taka watu watakaa hapo wale watupe mabaki ya vyakula na machupa ya plastic, asubuhi utakuta condom zilizotumika, watu watakojoa watapupu hapo hadi basi...hizi vurugu ndio tumezizoea [emoji16]
NA HILI NALO MKALITAZAMEWakuu,
Ni ajabu sana kuona miji midogo ndani ya majiji haina sehemu zenye utulivu kwa ajili ya watu kupumzika na kutembea, huku wakicheza na watoto wao, wakinywa soft drinks na bites, wakipiga picha na kupumzisha mafuvu yao.
Mji mdogo kama Mbezi-Kimara, kutwa ni shughuli za kiuchumi zinaendelea, kuanzia maduka makubwa hadi wanaopanga nyanya stand, huduma za usafirishaji hadi huduma zetu pendwa usiku wa manane maeneo tofauti kama kwa Gody, kwa Robert(Ngao Pub) na njia ya Kinyerezi.
Sasa kwa nini kusiwe na maeneo ya watu kupumzika, yatengenezwe vizuri, yahudumiwe kwa usafi yavutie wenyeji na wageni? Hizi open spaces nyingi zimegeuzwa maeneo ya biashara ndogondogo.
Watanzania nadhani hatuna huu utamaduni, tukitaka kutoka basi it's either tukutane bar, beach na wengine wetu guest😀, sio kila mtu anapenda kukutana bar. Lakini kuna namna tunaweza kujenga na kutengeneza maeneo mahususi watu wakakaa na kupumzika, kuongea, kupanga na kupangua mambo yao. Mbona hapo Zanzibar kuna sehemu zimejengwa vizuri tu, huku bara sisi tunashindwa nini?
Napendekeza eneo linalotizamana na Magufuli Stand, katikati ya barabara kuu na Stand kuu kuwe na recreation space, ijengwe vizuri, ivutie wageni na wenyeji, yaani sisi tunakuwa wala vumbi tu mda wote kweli?
Sio Mbezi tu, sehemu zote za miji yetu zinahitaji kuwa na mandhari za kuvutia wageni na wenyeji, tuache uchafu jamani, miji yetu ni michafu sana, haivutii, inaongezea watu stress.
Kwani wenye nchi huwa hawasafiri wakaona wenzetu wanafanyaje huko kwao?
View attachment 2392589
Pugu kazimzumbwi forest.....ipo wilaya ya kisarawe ila ni jirani kabisa na pugu Jokate aliitangaza sana akiwa dc kule, ni pazuri kwakweliNi wapi huko?