KERO Mamlaka Shehia ya Kwahani, Mjini Unguja zishughulikie Maji Taka na Mitaro inayotoa maji machafu na kusambaa Mtaani

KERO Mamlaka Shehia ya Kwahani, Mjini Unguja zishughulikie Maji Taka na Mitaro inayotoa maji machafu na kusambaa Mtaani

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni Mwananchi ninayeishi Shehia ya Kwahani, Wilaya ya Mjini Unguja Zanzibar, naomba mamlaka husika pamoja na baraza la Manispaa Unguja kushughulikia kero ya Maji Taka na mitaro inayotoa maji machafu mtaani kwetu.

Uchafu huo unatoka kwenye nyumba mpya za Kwahani na hivyo kuwa kero kwa muda mrefu, kinachosikitisha zaidi ni kuwa Watu wazima kwa wadogo wanapita na kuyakanyaga kama maji ya kawaida.

Watoto nao kuna muda wanapita na kucheza kabisa maeneo hayo, jamani hii hali si inaweza kusababisha maradhi ya mlipuko?

Viongozi wetu washughulikie hii hali inatutesa.

IMG_20250320_084343.jpg
IMG_20250320_084411.jpg
IMG_20250320_084038.jpg
 

Attachments

  • IMG_20250320_084209.jpg
    IMG_20250320_084209.jpg
    253.6 KB · Views: 34
Back
Top Bottom