Mamlaka simamieni vizuri huduma za usafiri, kuna 'uhuni' mwingi sana kule

Mamlaka simamieni vizuri huduma za usafiri, kuna 'uhuni' mwingi sana kule

May Day

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2018
Posts
6,311
Reaction score
9,027
Siku chache zilizopita nimetumia muda mwingi barabarani nikitumia usafiri wa Mabasi yanayofanya safari kati ya Dar Es Salaama na Arusha.

Hakika kuna mengi nimeshuhudia yanayokera mpaka unajiuliza ziko wapi Mamlaka zinazotakiwa kusimamia na kutoa miongozo, ina mana hawaoni haya?

Kati ya mambo niliyoyaona na kukerwa nayo ni pamoja na aina ya maudhui yanayooneshwa kwenye TV screen zilizopo kwenye Mabasi haya.

Hebu Mamlaka iwakumbushe hawa Watoa huduma/Wamiliki kuwa wanawajibika kuwahudumia Watu wenye imani tofauti tofauti badala ya Watu kulazimika kuangalia na kusikiliza nyimbo za kuabudu zisizomuhusu na zilizoegemea upande mmoja tu wa imani, na sanasana ni ya mmiliki wa chombo.

Au la basi Kampuni husika ziweke wazi kuwa wao ni wa Mrengo wa Imani fulani na wanahitaji Abiria wa Imani hiyo tu...au walau basi wacheze maudhui hayo kwa uchache sana, Nyimbo moja au mbili sio mbaya.

Kama hiyo haitoshi nikakutana na kiroja kwenye moja ya Kampuni ambapo Muhudumu anafanya maombi ya kuombea safari...tatizo ni lile lile la kulazimishana Watu kutumia zaidi ya dakika 5 au 6 kusikiliza kero zisizokuhusu. Yaani kwa kuwa tu Muhudumu yeye ni Muumini wa kwa Wazee wa upako basi ataangusha maombi hapo bila kujali kuwa anachokifanya ni kero tu kwa Abiria wengine.

Ifike mahali kuwe na muongozo wa Mtu kusema maneno machache tu yanayotosha kubeba uzito...kwa mfano "Mungu ibariki Safari yetu" au "Mungu tuongoze kwenye hii Safari yetu" n.k badala ya kukera Watu na sala zao ndefu ambazo kama kuna Abiria wa Kihindi ndani ya Basi nyie mmemtenga kwa hizo sala zenu.

Kero nyingine kubwa ni maudhui ya Video za Muziki na Movie...Huwa najiuliza hawa Watu wanatumia vigezo gani kuchagua haya Maudhui, au wao hunufaika na nini kwa hayo Maudhui wanayoonesha kwenye Vyombo vyao hivyo vya usafiri?.

Mara kadhaa utakuta kuna Watoto wengi tu ndani ya Gari na matokeo yake kile wanchodhani kinatuburudisha huishia kuwa Kero kwa Wazazi walioongozana na Watoto wao ndani ya Basi, Hivi mbona zipo nyimbo nyingi tu zisizohusisha watu wanaoshikana shikana au wakiwa wamevaa chupi tu n.k..kwa mfano walicheza Wimbo wa Msanii Mbosso ambapo anashikana shikana na Mwanamke, baadae wakacheza wimbo wa Julio Iglicious ambapo Watu wananyonyana ndimi na nyingine kadhaa.

Nilimshuhudia Mama au Dada yake aliyekuwa amempakata Mtoto wa miaka kama 7 au 8 hivi akiwa anahangaika kumgeuza Mtoto kichwa asiangalie kule kwenye screen, na kama tunavyowajua Watoto basi ilikuwa ni kama wanashindana.

Baadae wakacheza Movie ya Rambo (Rambo 3 ile kama sikosei)Movie imejaa mauaji ya kinyama sana ile, na hata baadhi ya hao Watu wazima walishindwa kuiangalia, cha ajabu huyo Muhudumu na Dereva wake wao wapo mbele kule wala hawaangalii.

Hivi mbona wanazo comedy nyingi tu mule za kina Mkojani na Watu walikuwa wanafurahia? Nilitamani kuwaita kuwalalamikia lakini sidhani hata kama watajali Wabongo hawa na siku inayofuata kila kitu kinaendelea kama kawaida.

Ni lazima kuwe na Miongozo rasmi la sivyo ni tabu sana kwa Abiria.

Chama cha kutetea Abiria na LATRA amkeni, safari inapaswa kuwa sehemu ya burudani sio kero.
 
Kwenye maombi mhudumu akiombea safari sioni tatizo, au kama wewe huamini uwepo wa Mungu ndio ukerwe, vinginevyo nakuona kama mtu uliyejaa roho ya hasira zisizo na sababu, maombi ha dakika tano au sita ni muda mfupi sana.

Kuhusu maudhui ya hizo video nakuelewa, hapo kweli hazifai hasa kama abiria anasafiri na watoto, au akiwa na mtu mzima pembeni yake huwa mtihani haswa.
 
Huna neno lolote kuhusu wabrashi viatu, kupanda kwa madai ya rushwa, faini, kodi za stendi nk?

Vipi zile lazima za kuingia mabasi stendi njiani hata kama hakuna cha kufanya huko?

Vipi zile nauli pendekezwa kuanza kutumika May 15 wakati bei za mafuta zimepanda tena tokea kwenye hiyo iliyokuwa benchi mark?

Acheni kufanya wasio husika:

Awamu ya sita mnajiwakilisha walamba asali
 
Chama Chakutetea Abiria ni Mzigo kwa Abiria maana wao kwa sehemu kubwa wanakagua nauli za ubungo kipindi cha mwisho wa mwaka.

Miongozo ni muhimu na ni haki ya Mteja na Mtoa huduma.. kwa mfano Kuna miongozo ya Kupanga Nauli za Safari kwa Aina za Mabasi na Wameyagawanya katika makundi Matatu, Luxury, SemiLuxury na Ya Kawaida. Hivi abiria anawezaje kiyatofautisha au kuna muongozo gani wa kuhakikisha ili abiria ujue umepanda Basi la kiwango gani Itategemea na umepata huduma gani..

Huko kwenye Burudani ndio tatizo kabisa kuna uwezekano hata dereva na muhudumu wasijue abiria wanaangalia kitu gani muda huu.
 
Maombi ni lazima, bila maombi Leo usingekuwepo. Yesu anatupenda
Huyo Yesu unamjua wewe sio kila Mtu, Muhindu hajui hata Yesu ni nini.

Maombi ya kinafiki hatuyahitaji...hao hao wanaoomba wanatuwekea Video za maudhui machafu sasa si unafiki tu huo.

Aseme MUNGU IBARIKI SAFARI YETU inatosha sana tu.
 
Kwenye maombi mhudumu akiombea safari sioni tatizo, au kama wewe huamini uwepo wa Mungu ndio ukerwe, vinginevyo nakuona kama mtu uliyejaa roho ya hasira zisizo na sababu, maombi ha dakika tano au sita ni muda mfupi sana.

Kuhusu maudhui ya hizo video nakuelewa, hapo kweli hazifai hasa kama abiria anasafiri na watoto, au akiwa na mtu mzima pembeni yake huwa mtihani haswa.
Siungi mkono maombi ya kinafiki mimi.

Wewe Abiria kama unaona umuhimu wa maombi si usali nani anakuzuia, mpaka Muhudumu akuongoze na janaba lake.
 
Chama Chakutetea Abiria ni Mzigo kwa Abiria maana wao kwa sehemu kubwa wanakagua nauli za ubungo kipindi cha mwisho wa mwaka.

Miongozo ni muhimu na ni haki ya Mteja na Mtoa huduma.. kwa mfano Kuna miongozo ya Kupanga Nauli za Safari kwa Aina za Mabasi na Wameyagawanya katika makundi Matatu, Luxury, SemiLuxury na Ya Kawaida. Hivi abiria anawezaje kiyatofautisha au kuna muongozo gani wa kuhakikisha ili abiria ujue umepanda Basi la kiwango gani Itategemea na umepata huduma gani..

Huko kwenye Burudani ndio tatizo kabisa kuna uwezekano hata dereva na muhudumu wasijue abiria wanaangalia kitu gani muda huu.
Umeongea jambo lingine la muhimu sana Mkuu.

Nadhani niliwahi ku comment kuhusu hili kwenye moja ya nyui humu.

Kuna Wakati nimekata tiketi ya luxury, yale Mabasi yao nayajua ni mazuri...kufika alfajiri naona naelekezwa kwenye Basi lilokaa kiana...aliyeniuzia tiketi hayupo muda huo, sikuwa na namna ilibidi nisafiri tu...kule ndani niliwaangalia Abiria Wenzangu na nikajua kabisa karibia nusu kama sio asilimia 90 mule wamepigwa kama mimi.

Basi halikuwa na sifa za Luxury lile na wala hakukuwa na Mtu wa kuomba msamaha kama kuna tatizo lilitokea wakabadili Basi, yaani ni kupelekwa pelekwa tu.

Na hili la tiketi Mtandao ndio mtawarahisishia kupiga sana Watu maana mnakutana saa kumi na moja alfajiri na huna tena choice....kuna uhuni sana hii sekta ya usafirishaji.
 
Tatizo watu hawajui kiarabu. Ukitaka mtoa maombi kwa upande wa waislamu itabidi umkodi ustadhi utaweza kumlipa kila siku?
Ila huo upande mwingine mtu yeyote anaweza kuomba. Badilisheni lugha kwanza
 
Tatizo watu hawajui kiarabu. Ukitaka mtoa maombi kwa upande wa waislamu itabidi umkodi ustadhi utaweza kumlipa kila siku?
Ila huo upande mwingine mtu yeyote anaweza kuomba. Badilisheni lugha kwanza
Ila si wanajua kiswahili?..basi waseme tu "MUNGU IBARIKI SAFARI YETU" maneno yanatosha sana haya anayetaka ziada asali kwa wakati wake.
 
Nikiwa na kampuni ya bus, ntakuwa naweka series zinazo-trend kwa wakati huo.

Ili wale wanaozifuatilia wawe wanakimbilia kupanda bus langu.

Miaka ya nyuma niliwahi kupanda Shabiby toka Dodoma, katikati ya safari wakaweka zile movies za kutafsiriwa kwa kiswahili. Nilichoka.
 
Back
Top Bottom