Mamlaka ya Bandari (TPA) yatoa ufafanuzi kuhusu hali ya ajira za Watumishi wa Bandari ya Dar es Salaam

Mamlaka ya Bandari (TPA) yatoa ufafanuzi kuhusu hali ya ajira za Watumishi wa Bandari ya Dar es Salaam

Hapa ni janja ya TPA. Wafanyakazi watakaochagua kubaki TPA ina maana wengi watasambazwa Mikoani mfano Musoma, Mbaba Bay, Kyela, Mwanza, Ukerewe, Kemondo n.k na kama maisha yako yote ni Dar basi uchaguzi wako ni kuacha kazi. Watakaopenda kufanya kazi na DP World hata hawa DP World watakuwa na hiari ya kuendelea nao au kuachana nao.
Ahahahahha eti Kemondo...hii ipo Mwanza au Musoma?

Yaani ukithubutu kuchagua DP World ndo umejiua hapohapo...

Bora upelekwe Chonyonyo...

SEMA hii inatupa nguvi sisi tuliochagua biashara
 
Hawa wafanyakazi hawakupaswa kupewa jukumu la kuchagua TPA au DP World. Nionavyo mimi ilitakiwa TPA kukabidhi wafanya kazi wote waliokuwa chini ya TPA kwa DP world, Muundo wa TPA uvunjwe na ubaki uongozi wa TPA kusimamia tu uendeshaji wa DP world na kuhakikisha hawa DP World hawatanyanyasa wafanyakazi na kuhakikisha malipo yao yanfuata makubaliano ya mkataba, na kuhakikisha mkataba wenyewe unaenda kama ulivyopangwa.

Sasa TPA inabaki kufanya nini ilkiwa DP World anapewa Bandari ya Dar es Salaam na zingine na za maziwa yote, kama sikukosea mkataba ulikuwa unasemaje.

TPH iji disolve yenyewe, wafanyakazi wote waende kule DP World kwa mama Kizimkazi.
Kimsingi TPA hana mamlaka kwenye bandari kwa sasa na kama angekuwa ana mamlaka kama tulivyo ambiwa hawa wafanyakazi walitakiwa kukabidhiwa kwa DPW! Lakini kimsingi hawa wafanyakazi ni kama wamefukuzwa kazi TPA na ndio maana wanapewa option ya kinachoitwa kuajiriwa maana yake watapewa mikataba mipya na yenye masharti mapya na watapimwa kwa vigezo na hakutakuwa na kufanya kazi bila kufukuzwa kazi hivyo wale watakao ajiriwa na DPW wajiandae kuchapa kazi kweli kweli ……!

Kiufupi watakao baki TPA wengi wao watahamishiwa kwenye ofisi za serikali na mashirika mengine na pia watapelekwa kwenye vibandari vidogo vidogo…..!

Kwa watanzania walivyo na mambo ya hovyo,uvivu ,ujinga nawashauri wabaki TPA….
 
Translation.... Tuma maombi kufanya kazi na TPA Bandarini AU endelea kubaki na sisi tukutafutie nafasi katika bandari nyingine nchini...., Swali linakuja huko pengine kuna uhaba au ndio kupewa contract ambayo mwisho wa siku haiwi renewed / terminated ?

Kwa waliodhani DP watakuja na kuwekeza machinery alafu ajira ziongezeke walikuwa wanota (au wanaendelea kuoata Ndoto za Alinacha)
 
Hawa wafanyakazi hawakupaswa kupewa jukumu la kuchagua TPA au DP World. Nionavyo mimi ilitakiwa TPA kukabidhi wafanya kazi wote waliokuwa chini ya TPA kwa DP world, Muundo wa TPA uvunjwe na ubaki uongozi wa TPA kusimamia tu uendeshaji wa DP world na kuhakikisha hawa DP World hawatanyanyasa wafanyakazi na kuhakikisha malipo yao yanfuata makubaliano ya mkataba, na kuhakikisha mkataba wenyewe unaenda kama ulivyopangwa.

Sasa TPA inabaki kufanya nini ilkiwa DP World anapewa Bandari ya Dar es Salaam na zingine na za maziwa yote, kama sikukosea mkataba ulikuwa unasemaje.

TPH iji disolve yenyewe, wafanyakazi wote waende kule DP World kwa mama Kizimkazi.
Wamepewa gati nane (8) tu katika Bandari ya Dar es Salaam. Gatio namba 0-7.
TPA bado inaendelea kusimamia gati zingine na bandari zingine.
 

UFAFANUZI KUHUSU HALI YA AJIRA ZA WATUMISHI KAΤΙΚΑ BANDARI YA DAR ES SALAAM
Ijumaa 22 Machi, 2024 DAR ES SALAAM

Jumatano tarehe 20 Machi, 2024 Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) ilitoa taarifa kwa Watumishi wake kuhusiana na mabadiliko ya uendeshaji wa Bandari ya Dar es Salaam, Gati namba sifuri (RoRo) hadi Gati namba saba.

Mabadiliko hayo yanatokana na Mkataba kati ya TPA na Kampuni ya DP World ya Dubai kuhusu uendeshaji na uendelezaji wa Gati namba 0-7 za Bandari ya Dar es Salaam kwa kipindi cha miaka thelathini (30) kuanzia tarehe 22 Oktoba 2023.

Kutokana na mabadiliko hayo katika usimamizi na uendeshaji wa maeneo tajwa, Watumishi wa Bandari ya Dar es Salaam walitakiwa kuchagua ama kubaki TPA au kusitisha mkataba wa ajira na TPA na kuajiriwa na DP World papo hapo.

Menejimenti ya TPA ilitoa taarifa hiyo kwa Watumishi baada ya kukamilisha pro- gramu maalum ya kuwaelimisha na kutoa ufafanuzi wa kina na taarifa sahihi kuhusiana na mabadiliko tajwa kwa Watumishi wake.

Katika taarifa ya Menejimenti, Watumishi watakaoridhia kujiunga na DPW kwa hiyari walielekezwa kuwasilisha taarifa zao (Notice) katika Ofisi zilizopo ghorofa ya 32 katika Jengo la Makao Makuu ya TPA (One Stop Centre) kabla au ifikapo tarehe 29 Machi, 2024. Aidha, Watumishi ambao hawatapenda kujiunga na DP World watabaki TPA kwa kuwa Mamlaka itaendelea kuhitaji Watumishi watakaotoa huduma katika Bandari zake zinazoendelea kuboreshwa katika maeneo mbalimbali Nchini.

Kwa kuzingatia ufafanuzi hapo juu, Menejimenti ya TPA inapenda kuujulisha Umma kwamba, taarifa inayosambaa ilitolewa kwa ajili ya Watumishi na TPA ilifanya hivyo ili kukamilisha taratibu za kuhamisha huduma kwa DP World.

TPA inauhakikishia Umma kwamba, itaendelea kuwathamini Watumishi wake ambao ni rasilimali muhimu zaidi katika Mamlaka na katika utekelezaji wa zoezi hili, maslahi ya pande zote husika yatazingatiwa kikamilifu kwa mujibu wa Sheria za Nchi yetu.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Masoko na Uhusiano,
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (ΤΡΑ)

Pia soma:
- DP World wadaiwa kuanza mchakato wa kuajiri, Wafanyakazi wa TPA wadaiwa kutakiwa kuchagua kwenda DWP au kubaki TPA
Akili kumkichwa Hao watakaohamia DP world watakua wamemake risk decision watakaokua wamebaki TPA watakua safe Na security ya kazi
 
Wamepewa gati nane (8) tu katika Bandari ya Dar es Salaam. Gatio namba 0-7.
TPA bado inaendelea kusimamia gati zingine na bandari zingine.
Unajua kuna gati ngapi pale bandarini!?
Sehemu iliyo baki ni ya wavuvi tu, hata ile aliyo kuwa nayo tics ambayo ilipewa kampuni haileweki ni janja tu za kumshikia dp word.
Hakuna gati inayo baki, na sgr ikikamilika mpaka mwanza na kigoma nazo atachukua
 
Back
Top Bottom