Mamlaka ya chakula(TMDA) ingieni kazini kukagua samaki na nyama nchi nzima, tena kwa uwazi, tamko ya Makamu wa Rais linatutia hofu

Mamlaka ya chakula(TMDA) ingieni kazini kukagua samaki na nyama nchi nzima, tena kwa uwazi, tamko ya Makamu wa Rais linatutia hofu

Siwaelewi kabisa viongozi wetu.

Wanafanya mambo kwa kutukomoa.
 
Maji ya sumu kutoka mgodi wa north mara yalikuwa yanatiririka kwenye mto mara na samaki na viumbe vingine vilikufa
Wananchi walipaza sauti na serikali ikaunda tume mchongo, na tume mchongo ikatupa majibu haya....samaki wa mto mara na viumbe wengine wamekufa sababu mazingira na hali ya hewa hubadilika ndani ya maji yanayosababishwa biological reasons [emoji375][emoji375][emoji375][emoji375][emoji1732]
 
Tamko la makamu wa Rais kwamba samaki, na pengine nyama zinazouzwa zinaleta kansa, kwa kweli linaleta ukakasi.

Mamlaka ya chakula, tunahitaji ukaguzi wa kina nchi nzima, na taarifa za Kila siku au mwezi au wiki zitolewe
Tangu lini TMDA imekuwa Mamlaka ya chakula?
 
Juzi kuku wa shekilango, Mara samaki wa mwanza ,Mara mafuta Singida..vyakula vingi vimeharibiwa Sana..maisha yetu yako hatarini sana...hizi cancer zimekuwa nyingi

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kwahyo mkuu Hawa niliowaletea kutoka mwanza mwezi wa Saba Ni sawa niwatumie au niwatupe tuView attachment 2359739View attachment 2359740
IMG_20220917_132930_5.jpg


Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Tamko la makamu wa Rais kwamba samaki, na pengine nyama zinazouzwa zinaleta kansa, kwa kweli linaleta ukakasi.

Mamlaka ya chakula, tunahitaji ukaguzi wa kina nchi nzima, na taarifa za Kila siku au mwezi au wiki zitolewe
Linalonitatiza mimi ni kwamba itakuwaje Makamu wa Rais afikie hatua ya kutamka jambo zito namna hii bila ya kuwasiliana na wizara husika na taasisi zenye wajibu wa kusimamia ubora wa chakula?

Hili linawezekana vipi hasa?
 
Mi sijalelewa, kuna kauli mbili nilizosikia

1.Samaki kuhifandhiwa kwa kutumia maji ya yaliyo oshea maiti.

2. Samaki kuhifadhiwa kwa kutumia dawa za kuoshea maiti.

Lipi linalosemwa hapo ?
 
lakini kama hao samaki wenye dawa za maiti wanaliwa nchi nzima kulikoni hiyo Kansa iwe kanda ya ziwa tu ?
Kinyume chake kingekuwa sahihi zaidi; yaani kanda ya ziwa isingekuwa na tatizo hilo kabisa kwa vile wao wanakula samaki 'fresh' ambaye bado hajawekwa kwenye hayo maji; ila huko kwingine ndiko kungekuwa na matatizo zaidi kwa vile hayo maji ni kuhifadhi samaki wasiharibike.

Lakini pia tatizo linaweza kuwa kubwa kanda ya ziawa kuliko kwingineko, kwa sababu wakazi wa kanda hiyo wanatumia samaki mara nyingi zaidi kila wiki kuliko watu waliopo maeneo mengine ambao wao utumiaji wao ni wa mara moja kwa wiki. Hili linawezekana kama madhara yanatokana na chembechembe zilizomo kwenye samaki wenyewe, kama vile 'mercury'.
Ni kama mvuta sigara anayetumia paketi moja kwa siku, na mwingine anayetumia paketi hiyo hiyo mara moja kwa wiki. Mategemeo ya kawaida ni kwamba mvuta paketi kwa siku atadhurika mapema kabla ya yule mwingine.

Formaldehyde, bila shaka ndiyo inayosemwa kuwa maji (dawa) za maiti! Aiseee, waswahili wanajua kupindisha jambo na kulifanya la kutisha kabisa.
Hii haina maana kwamba 'formaldehde' haina madhara, lakini "siyo maji ya kusafishia maiti" kivile!
 
lakini kama hao samaki wenye dawa za maiti wanaliwa nchi nzima kulikoni hiyo Kansa iwe kanda ya ziwa tu ?
Alichosema Makamu wa Rais, ni kuwa kuna ongezeko la wagonjwa wa kansa, Kanda ya ziwa, akimaanisha kuwa walaji wakubwa wa Sato na Sangara, kutoka ziwa Victoria, ni wakazi wa ukanda huo
 
KAULI YA MWANASIASA AU KAULI YA MTAALAMU?
Sasa imekuwa ni mazoea ya WANASIASA kuingia kazi za wataalamu,madhara yake imekuwa kwa kila jambo linafanyiwa siasa.

Matatizo ya Tanesco utasikia anaongea mwanasiasa,mlipuko wa magonjwa utasikia anaongea mwanasiasa.

Wanasiasa,tuache maeneo yenye kuruhusu utaalamu waongee wataalamu.

Mfano huu:Siasa imeingia kwenye elimu,mmeua elimu,sasa mnamtafuta mchawi. :wanasiasa,tena viongozi wamekuwa wanawatishia walimu kwa kauli,tena hadharani "nisisikie wanafunzi wamefeli","walimu wote ambao shule zao wanafunzi wamefeli washushwe cheo","msihoji wanafunzi waliofaulu na hawajui kusoma na kuandika, wapokeeni na muwafundishe".Sasa wanaachwa watoto wanaenda sekondari bila kujua kusoma na kuandika,na kufanya taifa kuzalisha idadi kubwa ya wanafunzi waliofeli kuingia mtaani.
 
Mi sijalelewa, kuna kauli mbili nilizosikia

1.Samaki kuhifandhiwa kwa kutumia maji ya yaliyo oshea maiti.

2. Samaki kuhifadhiwa kwa kutumia dawa za kuoshea maiti.

Lipi linalosemwa hapo ?
Namba mbili ndiyo sahihi.
Kuna dawa zinazotumika kuhifadhi vyakula au kitu chochote kinachooza ili kisiharibike.

Maiti isipowekewa dawa itaharibika. Samaki isipowekwa dawa/au kuhifadhiwa kwenye jokofu itaharibika.

formaldehyde ni aina ya dawa inayochanganywa na maji ili kuhifadhi maiti isiharibike.

Wapumbavu wakaona waitumie kuhifadhi samaki na wao wasiharibike. Haya matumizi kwenye chakula hayaruhusiwi kwa sababu hiyo dawa ina madhara kwa viumbe hai wanaokula vitu vilivyohifadhiwa na hiyo dawa..

Namba moja ni upotoshaji wa moja kwa moja wa kutia vitisho kwa watu.
 
Alichosema Makamu wa Rais, ni kuwa kuna ongezeko la wagonjwa wa kansa, Kanda ya ziwa, akimaanisha kuwa walaji wakubwa wa Sato na Sangara, kutoka ziwa Victoria, ni wakazi wa ukanda huo
Lakini hata hili haliwezi kuwa sahihi, kwa maana hiyo kansa inaweza ikawa inasababishwa na vitu vingine bila kupitia kwenye samaki, pamoja na kwamba inawezekana kwa vile samaki wanapata chembe chembe hizo ndani ya maji, kama mercury, kwa mfano, inayotumika kwenye machimbo ya dhahabu.

Njia pekee ya kujua ukweli ni kufanya utafiti; kabla ya kutoa matamko kama haya.
 
lakini kama hao samaki wenye dawa za maiti wanaliwa nchi nzima kulikoni hiyo Kansa iwe kanda ya ziwa tu ?
Kiwango cha samaki kinacholiwa maeneo mengine, kinalinhana na kike kinacholiwa ndani ya kanda ya Ziwa ambako samaki huvuliwa? Unafahamu kuwa kuna asilimia kubwa sana ya wananchi kweenye kanda nyingine ambao hawajawahi kumgusa samaki wa Ziwa Victoria?

Mimi mwenyewe, namla samaki wa Ziwa Victoria nikiwa kanda ya Zuwa. Lakini siwezi kuwa Sumbawanga, Mbeya, Singea au Dar, nikaagiza samaki wa Ziwa Victoria. Nikiwa Dar napendelea king fish au changu, nikiwa kuke Sumbawanga napebdelea yule wabamwita kachinga (sijui kama nimepatia), kule Songea napendelea dagaa wa ziwa nyasa (ni dagaa watamu kuliko dagaa wengine wote wanaopatikana nchini).

Walaji wakuu wa samaki wa kanda ya Ziwa ni wakazi wa Kanda ya Ziwa, wakazi wa kanda nyingine ni kwa kiasi kidogo sana. Samaki wanaopeelekwa viwandani, hawawekwi hayo madawa ya ajabu kwa sababu wanagandishwa na wenye viwanda. Samaki wenye shida ni hao ambao wengi wanauzwa kwenye fukwe za Ziwa. Wakishavuliwa wanaletwa wakiwa fresh, wakikosa wateja wakiwa fresh, ndipo mbinu chafu za kuwahifadhi zinapoanza kutumika. Na hapo hutamwona nzi hata mmoja, pamoja na ukweli kuwa samaki wana harufu kali sana inayowavuta nzi.
 
Back
Top Bottom