Kukosekana kwa huduma ya maji katika maeneo ya Nyegezi na viunga vyake kumegeuka kuwa tatizo sugu na la kudumu, linalojirudia kila mara bila ufumbuzi wa msingi. Tangu sikukuu ya Krismasi hakuna maji, hali ambayo imewaweka wananchi katika adha kubwa ya maisha ya kila siku.
Licha ya kurudiarudia kwa tatizo hili, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) wameendelea kukaa kimya bila kutoa taarifa rasmi, maelezo ya kina, wala ratiba ya kurejesha huduma. Ukimya huu unaonesha kukosa uwajibikaji kwa taasisi inayopaswa kuwahudumia wananchi.
Huduma ya maji ni haki ya msingi.
MWAUWASA wajibikeni sasa—toeni taarifa ya wazi na suluhisho la kudumu kwa tatizo hili sugu.