Analogia Malenga
Platinum Member
- Feb 24, 2012
- 5,292
- 10,842
Shirika la Umeme nchini (Tanesco) mkoa Mwanza limesitisha huduma ya umeme kwenye chanzo cha maji cha Nyamazugo kinachosambaza maji wilayani ya Sengerema mkoani hapa.
Meneja wa shirika hilo wilayani Sengerema, James Kabasa amesema wamesitisha huduma hiyo kutokana na Mamlaka ya Maji Safi ya Mji wa Sengerema (Seuwasa) kudaiwa Sh40 milioni kama malimbikizo ya ankara ya miezi miwili.
Amesema Seuwasa wanadaiwa ankara ya miezi miwili ya Desemba na Januari ambapo Februari 27 wamelipa Sh19 milioni, hivyo, bado wanadaiwa Sh21 milioni.
“Hatuta lejesha huduma ya umeme hadi walipe deni hilo licha ya Wananchi kuteseka kwa kusomba maji kwenye mito,” amesema Kibasa.
Meneja wa Seuwasa, Robert Lupoja amekiri kusitishwa kwa huduma ya umeme kwenye chanzo cha maji cha Nyamazugo kutokana na kudaiwa ankara hiyo.
“Tuko kwenye meza ya mazungumuzo, tumekwisha lipa Sh19 milioni bado tunadaiwa Sh21milioni kukamilisha ankara hiyo. Tunawaomba waturejeshe huduma ili tuendelee kulipa,” amesema Lupoja.
Akizungumzia suala hilo, mkuu wa wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole amesema wamepata taarifa ya Tanesco kusitishwa huduma ya umeme chanzo cha maji Cha Nyamazugo na analifanyia kazi.
CHANZO: Mwananchi