Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mnaua biashara na mzunguko pia wa pesa

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mnaua biashara na mzunguko pia wa pesa

TumainiEl

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
6,782
Reaction score
12,716
Ndugu zangu TRA mimi naomba niwaambie ukweli mnauwa biashara siwafichi nasema ukweli ukweli mtupu.

Mnauwa biashara na mnaenda kuuwa secta ya fedha kabisa. Hivi mnajuwa watu wanatoa pesa bank na hawataki kusikia akaunti?

Hivi mnajuwa hizi estimate mnawapa watu zinawafanya kufunga biashara na kuachana kabisa na biashara nina andika haya kama BOT wangefanya tahimini ya mabank akaunti zinavo fungwa walai mngeacha hii aina ya ukusanyaji kodi..

Hali sio nzuri naongea juu juu tu ila mambo yanaendelea kiukweli yanatisha na waambia ynatisha.

Wafanyeni watu wapende kulipa kodi na sio kuwa chukia. Kuna watu wanapesa na hawatumii bank na wala hawataki bank why?

TRA hili mnalifanya sio faida kwa uchumi wetu na mwisho itakuwa huzuni sana.

Nawasilisha maoni yangu kwa BOT fanyeni tathimini ya watu kuacha tumia huduma za ki bank pamoja na akaunti zilizo fugwa kwa sababu za kikodi au hofia kodi
 
Badala Yakuwapunguzia wafanyabiashara Kodi katika kipindi cha corona wao ndio kwanza wanawanyanyasasa watz
 
TRA nishida jamani, hebu waangalie namna yakufanya biashara ziishi na sio kuziua.

Mtu ndani ya mwez mmoja unakuwa examined mara mbili halafu zinatafautiana.

Halafu na hili swala la clearance mbona linageuka kuwa tatizo tena.

sio kwamba hatutaki kulipa kodi, tunaomba tulipe kutokana na hali halisi yakibiashara.

Makadirio nayo mnafanya makubwa sana hadi tunakata tamaaa.

Tafadhalini
 
Hivi nasikia kuna pesa unapaswa utoe ya service levy, hii pesa inakuwa ya nini na mtu anailipaje.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
TRA nishida jamani, hebu waangalie namna yakufanya biashara ziishi na sio kuziua.

Mtu ndani ya mwez mmoja unakuwa examined mara mbili halafu zinatafautiana.

Halafu na hili swala la clearance mbona linageuka kuwa tatizo tena.

sio kwamba hatutaki kulipa kodi, tunaomba tulipe kutokana na hali halisi yakibiashara.

Makadirio nayo mnafanya makubwa sana hadi tunakata tamaaa.

Tafadhalini

Kwa kipindi hicho hicho au miaka tofauti?

Kwanini usingeandika barua ya kuomba extension ukieleza sababu zako kama zinamsingi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimepeleka barua ya kuomba kupunguziwa kodi
 
Back
Top Bottom