Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
KUSITISHWA KWA MUDA LESENI ZA HUDUMA ZA MAUDHUI MTANDAONI ZILIZOTOLEWA KWA MWANANCHI COMMUNICATIONS LIMITED
Kwa nyakati tofauti kati ya mwaka 2023 na 2024, TCRA ilitoa leseni za huduma za maudhui mtandaoni (online media services licences) kwa kampuni ya Mwananchi Communications Limited kutoa huduma kwa majina ya The Citizen, Mwananchi Digital, Mwananchi na Mwanaspoti kwa ajili ya utoaji wa huduma za maudhui mtandaoni nchini. Katika utoaji wa huduma na kwa mujibu wa Kanuni ya 16 ya Kanuni za Maudhui Mtandao (the Online Content Regulations) za mwaka 2020, Mwananchi Communications Limited anatakiwa kutokutangaza au kuchapisha kwa Umma maudhui yaliyozuiwa ikiwa ni pamoja na maudhui yanayolenga kudhihaki au kuharibu taswira ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tarehe 01 Oktoba 2024 Mwananchi Communications Limited ilichapisha maudhui mjongeo na sauti (audio-visual content) kwenye mitandao yake ya kijamii, maudhui yaliyozuiwa kwa mujibu wa Kanuni ya 16 ya Kanuni za Maudhui Mtandaoni zilizorejewa hapo juu. Aidha, maudhui hayo yameleta tafsiri hasi kwa Taifa, jambo ambalo linaathiri na kuharibu umoja, amani na mshikamano wa kitaifa.
UMMA UNATAARIFIWA KUWA, kufuatia kuchapishwa kwa maudhui yaliyokatazwa na yanayopingana na sheria, TCRA imesitisha kwa muda leseni za huduma za maudhui mtandaoni (online media services licences) za Mwananchi Communications Limited (The Citizen, Mwananchi Digital, Mwananchi na Mwanaspoti) kutoa huduma za maudhui mtandaoni nchini Tanzania kwa muda wa siku thelathini (30) tangu tarehe ya kutolewa kwa taarifa hii, wakati masuala mengine ya kiusimamizi yanafanyiwa kazi.
Imetolewa tarehe 02 Oktoba, 2024
PIA SOMA
- Siku ya Uhuru wa Habari: Hakuna Uhuru wa Habari, Bila Uhuru wa Kiuchumi wa Media/Waandishi wa Habari!. Media Njaa Inaweza Kuwa Huru?!
UPDATE:
- Gazeti la Mwananchi larejea hewani baada ya zuio la mwezi kuisha. Ni zile video tu au kuna la zaidi?