Pre GE2025 Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) yasitisha Leseni ya Mwananchi kutoa maudhui mtandaoni kwa siku 30

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Safi sana.

Ingependeza,kama Jamiiforums kuwa wanatoa sababu za kupigwa ban watu hapa kama inavyosomeka kwenye taarifa hii ya TCRA kwa Umma.

Hakika tungewajua wapotoshaji na wale wote wenye "kudhihaki au kuharivu Taswira ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hatahivyo, hii ni safi sana. Tuende na wakati.
Kuharivu ndiyo Kiswahili gani na cha wapi?
 
Safi saaaaaaaaaaaaana.

Hawa Mwananchi wanafanya uchochezi. Wametengeneza kibonzo kuonesha kuwa Tz kuna kutekana na kuuana jambo ambalo sio la kweli. Nchi yetu ni ya amani hakuna anayetekwa wala kuuawa.

Nikiripoti kutoka makao makuu ya tisiaraei ni mimi msemaji wa sisimizi.
Hujisikii hata Aibu tu Kuandika huu Upuuzi?
 
Hiyo sheria ya kuwafungia mwananchi online ni sheria ya kipumbavu kwa 100%.
Haiwezekani anayeituhumu Mwananchi online na anayetoa hukumu dhidi ya mwananchi online ni mtu huyo huyo mmoja (TCRA).
 
That is Tanzania.
 
View attachment 3113606

KUSITISHWA KWA MUDA LESENI ZA HUDUMA ZA MAUDHUI MTANDAONI ZILIZOTOLEWA KWA MWANANCHI COMMUNICATIONS LIMITED
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa kwa Sheria ya Mamlaka ya Usimamizi wa Mawasiliano Tanzania, Sheria Na. 12 ya mwaka 2003, kusimamia huduma za mawasiliano ya Kielektroniki na Posta katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa nyakati tofauti kati ya mwaka 2023 na 2024, TCRA ilitoa leseni za huduma za maudhui mtandaoni (online media services licences) kwa kampuni ya Mwananchi Communications Limited kutoa huduma kwa majina ya The Citizen, Mwananchi Digital, Mwananchi na Mwanaspoti kwa ajili ya utoaji wa huduma za maudhui mtandaoni nchini. Katika utoaji wa huduma na kwa mujibu wa Kanuni ya 16 ya Kanuni za Maudhui Mtandao (the Online Content Regulations) za mwaka 2020, Mwananchi Communications Limited anatakiwa kutokutangaza au kuchapisha kwa Umma maudhui yaliyozuiwa ikiwa ni pamoja na maudhui yanayolenga kudhihaki au kuharibu taswira ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tarehe 01 Oktoba 2024 Mwananchi Communications Limited ilichapisha maudhui mjongeo na sauti (audio-visual content) kwenye mitandao yake ya kijamii, maudhui yaliyozuiwa kwa mujibu wa Kanuni ya 16 ya Kanuni za Maudhui Mtandaoni zilizorejewa hapo juu. Aidha, maudhui hayo yameleta tafsiri hasi kwa Taifa, jambo ambalo linaathiri na kuharibu umoja, amani na mshikamano wa kitaifa.

UMMA UNATAARIFIWA KUWA, kufuatia kuchapishwa kwa maudhui yaliyokatazwa na yanayopingana na sheria, TCRA imesitisha kwa muda leseni za huduma za maudhui mtandaoni (online media services licences) za Mwananchi Communications Limited (The Citizen, Mwananchi Digital, Mwananchi na Mwanaspoti) kutoa huduma za maudhui mtandaoni nchini Tanzania kwa muda wa siku thelathini (30) tangu tarehe ya kutolewa kwa taarifa hii, wakati masuala mengine ya kiusimamizi yanafanyiwa kazi.

Imetolewa tarehe 02 Oktoba, 2024

PIA SOMA
- Siku ya Uhuru wa Habari: Hakuna Uhuru wa Habari, Bila Uhuru wa Kiuchumi wa Media/Waandishi wa Habari!. Media Njaa Inaweza Kuwa Huru?!
Aliyesema wanaenda mstuni kufanya mambo heye hakuhatarisha umoja na mshikamano.
 
Yaleyale ya kukimbia hoja kwa kumuaduisha mwenye hoja kinzani, sijui hawa madoktori wa kitanzanzania wanapataje hizi phd's kwa kweli. Daktari mzima unasign ban kwa vitu dhaifu namna hii??? Pathetic. Hivi hawa wangekutana na challenge kama za hurricanes, vita, mafuriko wangepambana nazo kweli?? Inasikitisha sana kuona pesa za umma kwa kuuza ng'ombe ili kusomesha ng'ombe na zinabaki kuwa ng'ombe vilevile ndani ya VX. wanajua kutumbua tu pesa za umma
 
Tarehe 01 Oktoba 2024 Mwananchi Communications Limited ilichapisha maudhui mjongeo na sauti (audio-visual content) kwenye mitandao yake ya kijamii, maudhui yaliyozuiwa kwa mujibu wa Kanuni ya 16 ya Kanuni za Maudhui Mtandaoni zilizorejewa hapo juu. Aidha, maudhui hayo yameleta tafsiri hasi kwa Taifa, jambo ambalo linaathiri na kuharibu umoja, amani na mshikamano wa kitaifa.
Yanasemaje hebu tupeni tuyasikie
 
Safi sana.

Ingependeza,kama Jamiiforums kuwa wanatoa sababu za kupigwa ban watu hapa kama inavyosomeka kwenye taarifa hii ya TCRA kwa Umma.

Hakika tungewajua wapotoshaji na wale wote wenye "kudhihaki au kuharivu Taswira ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hatahivyo, hii ni safi sana. Tuende na wakati.
Nakubaliana na ww pia wawe wanatuambia sababu za kufuta nyuzi zetu kimya kimya. Tuma hata taarifa privately
 
Bwana Yule alibinya uhuru wa vyombo vya habari, ila Mama kafungua nchi, uhuru wa kujieleza umeimarika, miatno tena kwa mama!
 
Nakubaliana na ww pia wawe wanatuambia sababu za kufuta nyuzi zetu kimya kimya. Tuma hata taarifa privately
Na Uhakika itakuwa ni jambo zuri tu.
Yaani, mtu akileta maudhui ya Uongo, wamwanike tu, ni muongo. Waweke pia na Uwongo wake.

Hatahivyo, natambua mchango mkubwa na hata changamoto wanazozipitia moderators, hawafanyi kazi ndogo hata na wapewe maua yao, ila nadhani wanaweza boresha huu mtandao ambao kwa sasa umejaa disinformation.
 
View attachment 3113606

KUSITISHWA KWA MUDA LESENI ZA HUDUMA ZA MAUDHUI MTANDAONI ZILIZOTOLEWA KWA MWANANCHI COMMUNICATIONS LIMITED
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa kwa Sheria ya Mamlaka ya Usimamizi wa Mawasiliano Tanzania, Sheria Na. 12 ya mwaka 2003, kusimamia huduma za mawasiliano ya Kielektroniki na Posta katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa nyakati tofauti kati ya mwaka 2023 na 2024, TCRA ilitoa leseni za huduma za maudhui mtandaoni (online media services licences) kwa kampuni ya Mwananchi Communications Limited kutoa huduma kwa majina ya The Citizen, Mwananchi Digital, Mwananchi na Mwanaspoti kwa ajili ya utoaji wa huduma za maudhui mtandaoni nchini. Katika utoaji wa huduma na kwa mujibu wa Kanuni ya 16 ya Kanuni za Maudhui Mtandao (the Online Content Regulations) za mwaka 2020, Mwananchi Communications Limited anatakiwa kutokutangaza au kuchapisha kwa Umma maudhui yaliyozuiwa ikiwa ni pamoja na maudhui yanayolenga kudhihaki au kuharibu taswira ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tarehe 01 Oktoba 2024 Mwananchi Communications Limited ilichapisha maudhui mjongeo na sauti (audio-visual content) kwenye mitandao yake ya kijamii, maudhui yaliyozuiwa kwa mujibu wa Kanuni ya 16 ya Kanuni za Maudhui Mtandaoni zilizorejewa hapo juu. Aidha, maudhui hayo yameleta tafsiri hasi kwa Taifa, jambo ambalo linaathiri na kuharibu umoja, amani na mshikamano wa kitaifa.

UMMA UNATAARIFIWA KUWA, kufuatia kuchapishwa kwa maudhui yaliyokatazwa na yanayopingana na sheria, TCRA imesitisha kwa muda leseni za huduma za maudhui mtandaoni (online media services licences) za Mwananchi Communications Limited (The Citizen, Mwananchi Digital, Mwananchi na Mwanaspoti) kutoa huduma za maudhui mtandaoni nchini Tanzania kwa muda wa siku thelathini (30) tangu tarehe ya kutolewa kwa taarifa hii, wakati masuala mengine ya kiusimamizi yanafanyiwa kazi.

Imetolewa tarehe 02 Oktoba, 2024

PIA SOMA
- Siku ya Uhuru wa Habari: Hakuna Uhuru wa Habari, Bila Uhuru wa Kiuchumi wa Media/Waandishi wa Habari!. Media Njaa Inaweza Kuwa Huru?!
Freedom of press attacked
Pascal Mayalla
 
Mwananchi online,niliishawaambia kwenye comment zangu kwamba,kwakuwa wamejitolea kuwashambulia watumishi wa MUNGU kwenye makala zao,basi anguko lao Mwananchi linakuja .
 
Back
Top Bottom