LUTULWITU
JF-Expert Member
- Sep 9, 2024
- 584
- 983
Kuna katuni flani, Angalia kwa MdudechadematzWalipost nn
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuna katuni flani, Angalia kwa MdudechadematzWalipost nn
Hiyo pia part and parcel of freedom of the press, media iko huru kusema chochote, anayesifu, yuko huru kusifu, anayetaka kuzungumzia uhuru wa habari yuko huru na hata kumsifu mama anaupiga mwingi, rukhsa.Na nyie media pia ni sehemu ya haya, hasa zile media ambazo kutwa kucha hazizungumzii Uhuru wa habari zaidi ya mapambio tu.
Kazi imeanza!Mamlaka Tanzania zaifungia Mwananchi kuchapisha habari mtandaoni kwa 'ukiukaji wa kanuni'
![]()
Chanzo cha picha,MCL
Mamlaka ya mawasiliano nchini Tanzania (TCRA) imesitisha kwa muda huduma za maudhui ya mtandaoni za Mwananchi Communication Limited (ML) kwa 'ukiukaji wa kanuni'
Katika tangazo lake kwa umma TCRA imesema imesitisha leseni ya huduma za maudhui ya mtandaoni dhidi ya kampuni ya habari ya MCL nchini humo, kwa ukiukaji wa kanuni ya mwaka 2020.
TCRA imesema tarehe 01 Oktoba 2024, MCL ilichapisha maudhui mjongeo na sauti (audio-visual kwenye mitandao yake ya kijami, maudhui yaliyozuiwa kwa mujibu wa Kanuni ya 16 ya Kanuni za Maudhui Mtandaoni za mwaka 2020.
''Maudhui hayo yameleta tafsiri hasi kwa taifa, jambo ambalo linaathiri na kuharibu umoja, amani na mshikamano wa taifa’’, imeeleza taarifa ya TCRA , iliyotumwa kwenye mitandao yake ya kijamii:
''Umma unaarifiwa kuwa, kufuatia kuchapishwa kwa maudhui yaliyokatazwa na yanayopingana na sheria, TCRA imesitisha kwa muda leseni za huduma za maudhui mtandano za Mwananchi Communication Limited (The Citizen, Mwananchi Digital, Mwananchi na Mwanaspoti) tangu tarehe ya kutolewa taarifa hii, wakati masuala mengine ya kiusimamizi yanafanyiwa kazi,’’ limehitimisha tangazo hilo.
Mwananchi Communication Limited imesemaje?
Kufuatia kuondolewa kwa leseni hiyo, MCL imetangaza kuondoa maudhui yake ya michoro kwenye mitandao yake ya kijami.
Kupitia gazeti lake la lugha ta Kiingereza The Citizen, kampuni hiyo imesema: ‘’Tumeamua kuondoa michoro iliyoshirikishwa Oktoba 1, 2024 kwenye mitandao ya kijamii (X na Instagram), kwa kuwa ilionyesha matukio yaliyoibua hofu kuhusu usalama wa watu binafsi nchini Tanzania.’’
''Uamuzi wetu wa kuondoa katuni unatokana na kusababisha tafsiri mbaya ambayo ni kinyume na nia yetu’’, taarifa hiyo iliongeza.
Maudhui yaliyoiweka MCL lawamani ni ya katuni ambayo ilikuwa ikionesha raia wa nchi hiyo wakilalama kwenye runinga juu ya matukio ya watu kutekwa na kuuawa nchini humo. Katuni hiyo ilikuwa ikimuonesha mtu ambaye alikuwa akitizama runinga ambaye wengi wametafsiri kuwa ni Rais wa nchi hiyo Samia Suluhu Hassan.
Matukio ya watu kutekwa, kupotezwa na kuuawa katika mazingira ya kutatanisha yamezua gumzo katika miezi ya hivi karibuni nchini Tanzania.
Chanzo.BBC
Wakuu huko Venezuela, kituo kimoja cha habari kimefungiwa kwa sababu editors walichapisha katuni inayoelezea matukio ya utekaji na mauaji yanayoendelea kwenye nchi hiyo.
Hivi mtu unamiliki jeshi, FFU nzima iko chini yako na unaweza kuamua kila kitu kwa kauli moja tu, unaanzaje kufungia media just because kuna kikatuni cha dakika moja kinaelezea matukio yanayoendelea nchini? Still bado tunaogopa vikatuni?
Sasa kama katuni tu inakuogopesha kiasi cha kufungia media nzima upande wa digital kwa siku 30, wale wakina Netanyahu wanaopambana na makombora kutoka Iran, mashambulizi kutoka Hezbollah na mabomu kutoka Hamas mngekuwa kwenye nafasi yao mngeweza?
Je ni sahihi kusema kuwa Venezuela inaongozwa na viongozi dhaifu zaidi kuwahi kutokea?
Nawaonea huruma sana wananchi wa Venezuela na yangu matumaini viongozi wake watajitafakari maana kama vikatuni tu wanaogopa, vita ikitokea bila shaka watakimbia kabisa nchi.
Naomba kuwasilisha!
Uovu wa watawala unapowekwa wazi hadharani matokeo yake huwa ni watawala hao kushikwa na hofu Kuu na huwa wanaamua kuwashughulikia Watu walioanika uovu wao hadharani. Ukweli mchungu daima huwa una kawaida ya kuchoma Sana moyoni.Hii imekuja dakika chache baad ya kuposti pia mauaji y kijana alieuliwa unguja na wasiojulikana, mwananchi ndo wakwanza kuposti hiiii
Hii nchi imemshinda