Mamlaka ya Palestina yaungana na Israel kupiga marufuku Al Jazeera.

Mamlaka ya Palestina yaungana na Israel kupiga marufuku Al Jazeera.

Chama tawala cha Fatah cha Mamlaka ya Palestina (PA) kimepiga marufuku shirika la habari la Al Jazeera lenye makao yake nchini Qatar kufanya kazi katika maeneo ya Judea na Samaria, likilituhumu kwa uchochezi, miezi kadhaa baada ya Israel kufanya hivyo.
Kwa mujibu wa ripoti ya World Israel News Staff, Mamlaka ya Palestina imepiga marufuku mtandao wa Al Jazeera kufanya shughuli zake ndani ya maeneo ya uhuru wa Judea na Samaria, kwa mujibu wa ripoti ya chombo cha habari cha Israeli, Walla.
Ripoti hiyo ilidai kuwa chama tawala cha Palestina, Fatah, kilitoa marufuku hiyo katika sehemu za Maeneo A na B – sehemu mbili za Judea na Samaria zilizo chini ya udhibiti wa kiraia wa PA – kutokana na jinsi Al Jazeera inavyoripoti kuhusu vurugu zinazoendelea kati ya Kikosi cha Usalama wa Taifa cha Palestina (PNSF) – polisi ya kijeshi ya PA – na muungano wa makundi ya kigaidi yanayofanya kazi katika mji wa kaskazini wa Samaria, Jenin.
Ripoti hiyo ilisema kuwa Fatah imelituhumu Al Jazeera kwa “kusababisha migogoro na uchochezi” dhidi ya juhudi za PA za kudhibiti machafuko ya wananchi, ikiwemo mapigano katika Jenin.
Kwa miezi kadhaa, vikosi vya PNSF vimejaribu kudhibiti machafuko ya wananchi katika maeneo ya Judea na Samaria.
Mapema mwezi huu, vikosi vya PNSF vilivamia Jenin kupambana na Kikundi cha Jenin Brigades, muungano wa makundi ya kigaidi, yakiwemo Hamas, ambayo yamekuwa yakidhibiti mji huo tangu mwaka 2022.
Tangu Desemba 5, vikosi vya PA vimekuwa vikikabiliana na Kikundi cha Jenin Brigades wakiwa wanajaribu kurejesha udhibiti wa mji huo.
Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya Palestina, Walla iliripoti kwamba uamuzi huo unalenga hasa shughuli za Al Jazeera katika Samaria, ikijumuisha miji ya Shechem (Nablus), Jenin, Tubas, Tulkarem, Qalqilya, na Salfit.
PA inaripotiwa kulituhumu shirika hilo la Qatar kwa kuripoti kwa upendeleo kwa niaba ya Hamas, ikirejea madai yaliyotolewa na Israel wakati wa vita dhidi ya kundi hilo la kigaidi lenye makao yake Gaza.
“Tumeamua kupiga marufuku kuingia kwa Al Jazeera, na tunawahimiza wananchi kutojihusisha kwa njia yoyote na kituo hiki,” ripoti hiyo ilinukuu chama cha Fatah kikisema.
“Al Jazeera ina jukumu hatari nchini Palestina. Inasambaza chuki na kuchochea vita vya wenyewe kwa wenyewe. Al Jazeera inaunga mkono wavunjaji wa sheria na inajaribu kuwaonyesha kama mashujaa wanaopigana dhidi ya ukoloni.”
Mwezi Mei, serikali ya Israel ilipitisha uamuzi wa kuzuia Al Jazeera kufanya kazi nchini humo, ikilituhumu kwa kuendeleza makundi ya kigaidi, yakiwemo Hamas, ambapo marufuku hiyo ilianza kutekelezwa na kusababisha kufungwa kwa shughuli za shirika hilo nchini Israel.

Links:

Al Jazeera condemns Fatah campaign against it in West Bank

Al Jazeera slams Fatah, Palestinian Authority over northern West Bank operations ban
Mamlaka ya Palestine inaionyesha Israel na Marekani kwamba inaweza kuwa na udhibiti mzuri ikikabidhiwa Gaza baada ya Israel kujiondoa.
 
Aljazeera iliwahi zungumzia involvement ya Qatar kwa Al Shabaab ya Somalia?

Aljazeera iliwahi zungumzia mikakati maalum ya Qatar kushawishi kuanguka kwa tawala za Kiarabu? Unahisi ilikuwa bahati mbaya Aljazeera kufanya coverage ya Arab Spring kuanzia Tunisia, Libya, Misri, Syria?

Aljazeera wameishazungumzia Qatar inavyotoa silaha kwenye vita ya Sudan?

Je Aljazeera wamezungumzia jinsi Qatar ilivyokuwa nchi ya kwanza ya Kiarabu kuunga mkono waasi wa Libya kumtoa Gaddafi? Walitoa fedha nyingi, mafuta, msaada kidiplomasia kabla hata NATO hawajaingia.

Umejiuliza wanafanya kwa faida ya nani.

Kama Muslim Brotherhood ni kundi zuri, Qatar au Turkey lipo?
Huu kama sio upumbavu ni nini, yaani Muslim Brotherhood inapewa support na Qatar na Turkey itawale Egypt na nchi nyingine, ila kwa supporters haitakiwi. Sasa intelligence agencies za hizo nchi zikikataa influence ya Qatar ndio unasema tawala zao haziitaki Aljazeera.
Wewe ulisikia wapi North Korea inalazimisha vuguvugu za kidemokrasia kwenye nchi nyingine, ila kwake haitaki demokrasia.

Syria hapo Aljazeera ilisema watu wanavyokufa, Gaza ilikuwa inapendelea kusema wanakufa watoto na wanawake.

Ndio maana mwaka 2017 Waarabu kina Misri na Saudi walitaka waitandike Qatar ikakimbilia kuleta majeshi ya Uturuki na kununua silaha kwa fujo, ina bahati ina kambi za Marekani.

Hawazingatii progress ya Waarabu, hawasisitizi innovation au prosperity, wao wanasubiri kichafuke wakashadadie magaidi na waasi kuharibu nchi za Kiarabu. Wewe ukiwa na jirani anatangaza unavyopigana na mke wako, ulivyochepuka, ulivyoshindwa ada ya watoto, ila ukinunua gari hasemi; vibaka wanaiba kwako wanaenda kujificha kwake anawahifadhi, anachangia wabaya wako. Huyo si ni wa kukata mawasiliano nae.
Aljazeera inafanya kazi ya kueneza Ushawishi wa Qatar ndio maana Misri, UAE na Saudia hawaipendi kabisa.
 
Hili la Al Jazeera kufanya upendeleo kwa kundi la Hamas walianza kitambo. Ukute Hamas wana hisa Al Jazeera.

Weka link ya taarifa basi

Kuna clip Youtube kuna youtuber mmoja mwarabu aliwa expose kuwa channel zao kwenye jamii ya kiarabu wanatoa taarifa tofauti na channel Inazooenyeshwa upande wa western alisema ukiangalia aljazeera ukiwa uarabuni utaona wako ant western ila ukiwa western countries utawaona kama wako neutral aljazeera walipoona jamaa kawa expose wakaamua kuanza kumtengenezea zengwe.. kwenye channel za kiarabu wakawa wanarusha kuwa analipwa na israel kuwasifia ila Cha ajabu
Vipindi hivyo wakawa hawavitoi kwenye international channel zao

Watu wanafikiri Aljezeera ni chombo
Huru. 100% Aljazeera inapokea funds kutoka Qatar Govt. Na Qatar mwaka
1996 kimakakati walitafuta mtu ambaye ataanzisha chombo cha habari kiwe kama BBC au CNN lakini wenyewe Govt wasiwe front kionekane ni private
 
Aljazeera iliwahi zungumzia involvement ya Qatar kwa Al Shabaab ya Somalia?

Aljazeera iliwahi zungumzia mikakati maalum ya Qatar kushawishi kuanguka kwa tawala za Kiarabu? Unahisi ilikuwa bahati mbaya Aljazeera kufanya coverage ya Arab Spring kuanzia Tunisia, Libya, Misri, Syria?

Aljazeera wameishazungumzia Qatar inavyotoa silaha kwenye vita ya Sudan?
Usizungumze uongo Na uongo huwa haukupendezi.
Unaweza kuleta ushahidi wa Qatar kuhusika na Vita za Sudan??
Unaweza ukaleta ushahidi wa Qatar kuunga mkono waasi waliompindua Gaadafi?
Ishu ya Qatar Libya ni kuwa Qatar alimuunga mkono Halif Aftar ambaye ndiye aliyekua mfuasi wa Zama za Gaddafi ili kurejesha utawala wa Zamani wa Libya.
Wewe unasema kuwa Muslim Brotherhood hawapendwi na walikuwa hawatakiwi,mbona Gaddafi raia walisema hawampendi kwa uchochezi wa USA hadi kufikia kumpindua lakini sasa hivi wanamlilia??
Mbona hata Mandela alifanyiwa unafiki hadi Na Kenya ndio tuamini kuwa Mandela alikuwa gaidi kisa alitangazwa na mabeberu na kunafikiwa na baadhi ya nchi za Afrika??
Je Aljazeera wamezungumzia jinsi Qatar ilivyokuwa nchi ya kwanza ya Kiarabu kuunga mkono waasi wa Libya kumtoa Gaddafi? Walitoa fedha nyingi, mafuta, msaada kidiplomasia kabla hata NATO hawajaingia.

Umejiuliza wanafanya kwa faida ya nani.

Kama Muslim Brotherhood ni kundi zuri, Qatar au Turkey lipo?
Huu kama sio upumbavu ni nini, yaani Muslim Brotherhood inapewa support na Qatar na Turkey itawale Egypt na nchi nyingine, ila kwa supporters haitakiwi. Sasa intelligence agencies za hizo nchi zikikataa influence ya Qatar ndio unasema tawala zao haziitaki Aljazeera.
Wewe ulisikia wapi North Korea inalazimisha vuguvugu za kidemokrasia kwenye nchi nyingine, ila kwake haitaki demokrasia.

Syria hapo Aljazeera ilisema watu wanavyokufa, Gaza ilikuwa inapendelea kusema wanakufa watoto na wanawake.

Ndio maana mwaka 2017 Waarabu kina Misri na Saudi walitaka waitandike Qatar ikakimbilia kuleta majeshi ya Uturuki na kununua silaha kwa fujo, ina bahati ina kambi za Marekani.

Hawazingatii progress ya Waarabu, hawasisitizi innovation au prosperity, wao wanasubiri kichafuke wakashadadie magaidi na waasi kuharibu nchi za Kiarabu. Wewe ukiwa na jirani anatangaza unavyopigana na mke wako, ulivyochepuka, ulivyoshindwa ada ya watoto, ila ukinunua gari hasemi; vibaka wanaiba kwako wanaenda kujificha kwake anawahifadhi, anachangia wabaya wako. Huyo si ni wa kukata mawasiliano nae.
Usizungumze uongo Na uongo huwa haukupendezi.
Palestina vyombo vya habari vyote ikiwemo Al-Jazeera vinatangaza Sawa kuwa wengi wao wanaokufa ni wanawake Na watoto.
Kwahiyo hivyo vyombo vingine vya habari vimeongopa au vinapewa rushwa Na Qatar vitangaze kama Qatar??

Usituletee uongo hapa aiseee.

Nenda kaitizame Misri kipindi anaitawala Mohammed Morsi na sasa hivi Misri ipi Ina nguvu!?
Misri ya sasa haina ile nguvu ya baba wa waarabu kama Misri ya kipindi like cha Morsi.
Ndio maana influence yote sasa hivi imehamia Qatar.
Wewe kaa endekeza propaganda ilhali ukweli unafahamika Qatar ikoje Na mchochezi wa Vita ni nani.
Hao mamlaka ya Palestina wenyewe pesa wanatoa Qatar za kuendesha serikali Yao.
Kaa ipakazie ubaya Qatar ilhali ni Taifa linalokua kiuchumi Na kiushawishi.
 
Kuna clip Youtube kuna youtuber mmoja mwarabu aliwa expose kuwa channel zao kwenye jamii ya kiarabu wanatoa taarifa tofauti na channel Inazooenyeshwa upande wa western alisema ukiangalia aljazeera ukiwa uarabuni utaona wako ant western ila ukiwa western countries utawaona kama wako neutral aljazeera walipoona jamaa kawa expose wakaamua kuanza kumtengenezea zengwe.. kwenye channel za kiarabu wakawa wanarusha kuwa analipwa na israel kuwasifia ila Cha ajabu
Vipindi hivyo wakawa hawavitoi kwenye international channel zao

Watu wanafikiri Aljezeera ni chombo
Huru. 100% Aljazeera inapokea funds kutoka Qatar Govt. Na Qatar mwaka
1996 kimakakati walitafuta mtu ambaye ataanzisha chombo cha habari kiwe kama BBC au CNN lakini wenyewe Govt wasiwe front kionekane ni private
Hizi ni propaganda tushazizoea.
Wahariri wa habari za Al-Jazeera ni wazungu Sio waarabu tena waandishi wa habari ambao wabobezi waliowahi kufanya kazi vyombo vikubwa vya habari kabla mathalan kina Kimberly Halket.
 
Back
Top Bottom