peno hasegawa
JF-Expert Member
- Feb 24, 2016
- 14,255
- 23,949
Uhuni huu enzi ya Hayati Magufuli haukuwepo ila naona umerudi kwa kasi baada ya Mama Samiah Suluhu kutwaa madaraka.
Kwa ufupi ni kwamba mamlaka ya uteuzi chini ya ofisi ya Rais ikulu imejaa na inanuka rushwa, hili limedhilika kwa baadhi ya wateule wa Rais katika nafasi mbalimbali ikiwemo DC, DAS, DED, RAS na RC ambao huteuliwa na mamlaka hiyo baada ya kutoa rushwa ya fedha /ngono ama vyote kwa pamoja, kutapeliwa hovyo kwa lengo la kuweza kulinda nafasi hizo za uteuzi.
Kinachoonekana hapa, ni kwamba nafasi hizi hupewa watu ambao hawana vigezo, ambapo mwisho wa siku huishia kutapeliwa na wahuni mbalimbali ambao hujitambulisha kama watu kutoka ofisi ya raisi (ofisa usalama) ama katibu/ naibu katibu mkuu wa raisi.
Na wengi wameingia mkenge huo wa kutapeliwa sio kwa bahati mbaya ni kwa sababu tu wamezoea kutoa rushwa ya fedha/ngono ama vyote kwa pamoja kwa mamlaka ya uteuzi ili wapate kukumbukwa katika kulamba asali ya awamu ya sita.
Ni muda rasmi sasa kwa Raisi mpendwa Mama samiah Suluhu kuwachukulia hatua ya kuwaondoa wale wote waliobanika kutapeliwa na kuunda mamlaka mpya ya uteuzi kuondoa uhuni na ukiritimba uliokithiri kwa mamlaka hiyo ya kupachika majina ya watu ambao hawana sifa stahiki kushikilia nafasi hizo.
Katibu wa CCM wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro ameharibu uchaguzi wa ndani kwa kuchukua fomu za wagombea wa Kata zote kabla hazijajadiliwa
Katibu mkuu wa CCM Taifa fika Jimbo la Hai huko Kilimanjaro ukakutane na kituko cha mwaka 2022, tena ukizingatia kuwa tangu uteuliwe kuwa Katibu mkuu wa CCM huu ndio uchaguzi wako wa kwanza, nenda Jimbo la Hai ukajifunze somo la uchaguzi wa CCM kutoka kwa Katibu wa CCM wa wilaya ambaye...