A
Anonymous
Guest
Takriban mwezi mmoja uliopita, katika jukwaa hili kuliripotiwa malalamiko ya wadau wa elimu wa Wilaya ya Kigamboni Mkoa wa Dar es Salaam, wakiwalalamikia wamiliki wa shule ya sekondari ya wasichana ya 'Competence' Girls' Islamic Seminary, kuwa wameweka Mkuu wa Shule anayetuhumiwa kwa vitendo vya unyanyasaji wa kingono kwa wanafunzi wa shule hiyo anayoisimamia.
Aidha, ilielezwa kwamba mkuu huyo ana historia ya vitendo hivyo vya kinyume cha maadili mema, kutokea shule aliyowahi kuwepo awali huko Bagamoyo mkoani Pwani; ikielezwa kuwa huko aliondolewa kazini kwa tabia yake hiyo mbovu baada ya kupatikana ofisini akimfanyia vitendo vya unyanyasaji wa kingono kwa nguvu mwanafunzi msichana, (jina linahifadhiwa); na hiyo ikawa sababu ya kuondolewa kazini hapo.
Baadhi ya wadau (waliopenda kuhifadhiwa majina yao), wamejaribu kufuatilia madai haya na kugundua yafuatayo:
1. Ni kweli mwalimu mkuu huyo, (jina linahifadhiwa), anatuhumiwa kwa madai hayo na mwajiri wake anafahamu jambo hilo, ila anamlinda kwa sababu mwalimu huyo amekubali kiwango kidogo sana cha mshahara.
2. Katika shule hiyo kuna kiongozi mmoja mkuu aliyejipachika jina la 'babu wa wanafunzi' ambaye pia ana tabia za maadili mabovu. Miongoni mwa tabia zake ni kuwaita wanafunzi hao wasichana mmoja mmoja na kukaa nao faragha, akidai hao ni wajukuu zake tu, naye huzungumza nao mambo yanayohusu 'babu na wajukuu zake' tu. Aidha, baadhi ya wanafunzi wameripotiwa kulalamikia tabia hiyo ya 'babu' yao wakidai anawapotezea muda wao wa masomo kwa kuwaita mara kwa mara, na pia kuwaumiza kisaikolojia.
3. Shule hiyo licha ya mandhari yake nzuri, lakini haina udhibiti mzuri wa wanafunzi, na kwa hivyo baadhi ya wanafunzi wameripotiwa kumrubuni mlinzi kwa kumpa pesa ili awaruhusu kutoka nje na kuingia mtaani kwa siri. Majina ya wanafunzi ambao wameshawahi kufanya hivyo yanahifadhiwa, na mmoja aliacha shule.
4. Adhabu ya viboko kwa kosa la kutofikisha alama za daraja la kwanza na la pili katika mitihani, ni iliyozidi kiwango na yenye kudhuru afya za wanafunzi hao, (picha za majeraha zilizopatikana, zimehifadhiwa).
5. Uongozi wa shule umeweka mganga wa kienyeji shuleni kwa madhumuni ya kuvutia wateja na kuwadhibiti wazazi wasihamishe watoto wao.
Haya na mengine ambayo hayajaelezwa hapa, ni kero kwa baadhi ya wazazi na wadau wengine wa elimu ambapo inaelezwa kuwa wamiliki wa shule hiyo wamelalamikiwa mara kadhaa bila kuchukua hatua yoyote ya marekebisho.
Mamlaka za elimu Kigamboni chunguzeni madai haya na ikithibitika mchukukue hatua stahiki kwa manufaa na ustawi wa elimu ya wanafunzi wa shule hiyo na jamii kwa ujumla.