Mamlaka za Ushirika Lindi: Wakulima wa Ufuta wamelipwa, mwenye changamoto ya malipo awasiliane nasi

Mamlaka za Ushirika Lindi: Wakulima wa Ufuta wamelipwa, mwenye changamoto ya malipo awasiliane nasi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Baada ya hoja ya Mdau , kuandika Vyama vya USHIRIKA vinavyonunua mazao Lindi hasa Kilwa wafanyakazi wake wanazungusha malipo ya Wakulima ufafanuzi umetolewa na mamlaka zinazohusika:
Screenshot 2026-07-20 140305.jpg
Mwenyekiti wa Bodi ya Chama Kikuu Cha Ushirika Lindi Mwambao Ltd anapenda kuwataarifu Wakuliwa na wadau wote walio katika mnyororo wa zao la ufuta kuwa;

Chama Kikuu Cha Ushirika Lindi Mwambao kwa Msimu huu wa ufuta 2026 kimeshafanya Jumla ya Minada Sita (06) ya ufuta ambapo Minada yote sita hadi kufikia leo tarehe 18.07.2026 imeshalipwa kwa wakulima.

Hivyo, Uongozi unaomba kwa mkulima yoyote mwenye changamoto ya malipo hasisite kuwasiliana Nasi kwa Nambari 0654827498 au 0685 543 131 ili aweze kupata Maelezo ya malipo yake.

TAARIFA HII IMETOLEWA NA,
ISMAILI M. NALINGA, MWENYEKITI WA BODI, CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA LINDI MWAMBAO.


Screenshot 2026-07-20 140242.jpg

TAARIFA KWA WAKULIMA NA WADAU
19 JULAI, 2026

Mwenyekiti wa Chama Kikuu Cha Ushirika RUNALI Ltd anawataarifu wanaushirika, wakulima na wadau wote kuwa.

Hadi kufikia leo tarehe 19/07/2026 RUNALI Ltd imefanya jumla ya Minada Saba (7) ya zao la Ufuta kwa Msimu wa 2026/2027, ambapo minada sita (6) tayari imelipwa kwa wakulima na malipo ya mnada wa saba (7) yanaendelea.

Aidha Uongozi unawataarifu wakulima wenye changamoto ya malipo kuwasiliana nasi kwa namba hii 0764 361 536.

TAARIFA HII IMETOLEWA NA:
ODAS ODAS MPUNGA
MWENYEKITI
CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA RUNALI LTD
 
Back
Top Bottom