DOKEZO Mamlaka ziko wapi? Machinjio ya Vingunguti karibia ng'ombe 100 wanapotea kila siku kwa uzembe wa kuchinja ng'ombe wenye mimba

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
276
Reaction score
473
"Ukistaajabu ya Musa,Utayaona ya Firauni", katika hali ya kushangaza katika soko la Vingunguti lililopo jijini Dar es salaam ambapo huchinjwa zaidi ya ng'ombe 500 kwa kila siku, ni kwamba kati ya idadi hiyo karibia ng'ombe 100 huchinjwa wakiwa na mimba.

Mara ya kwanza nilisikia suala hili nikawa nadhani ni utani lakini katika kufuatilia kwa baadhi ya vyanzo ikiwemo wanaohusika na zoezi la kuchinja kwenye machijio hayo nimebaki kushangaa zaidi baada ya kunithibitishia suala hilo.

Katika kudadisi kwangu ni kwamba baadhi ya wafanyabiashara ambao huchukua mifugo hiyo kwenye minada, ni kwamba hujenga ushawishi wa kupata mifugo yenye mimba kwa lengo la kuja kupata faida zaidi baada ya ng'ombe hao kufikishwa kwenye machinjio na kuchinjwa.

Faida hiyo inapatikanaje?

Ni kwamba baada ya ng'ombe hao kuchinjwa zile mimba (vichanga) kutolewa, huuzwa kwa wafanyabiashara wanaouza vyakula vya mbwa pamoja na kuku.

Wafanyabiashara huweka oda kwa ajili ya kuchukua vichanga hivyo, ambapo watu wao hufika kila siku na kuvichukua hususani kwa ajili ya kuandalia chakula cha mbwa na kuingizwa sokoni. Chanzo kutoka kwenye kampuni Xxx ambayo inajihusisha na biashara ya uuzaji wa vyakula vya mifugo, anakiri kuwa wamekuwa wakichukua vichanga mara kwa mara kwenye machinjio hiyo kwa ajili ya kutumia kuandalia chakula cha mbwa wakati mwingine hadi chakula cha kuku.

Udadisi unabaini sababu ya vichanga hivyo upendelewa kwa kuwa inaelezwa kuwa mifupa ya vichanga ni milaini, hivyo baada ya kuvipata uvikatakata na kuvianika kisha kuvisaga kihurahisi kupitia mashine maalum kisha kuchanganya na bidhaa nyingine kwa ajili ya kwenda sokoni.

Hata hivyo wengine ambao sio wafanyabiashara nao hufika sokoni hapo na kuchukua vichanga hivyo kwa ajili ya matumizi ya moja kwa moja ili kuwapikia mbwa.

Katika kudadisi vyanzo tofauti vilibainisha wazi kwamba vichanga hivyo huuzwa kwa kupimwa kwenye ndoo ambapo gharama yake ni elfu 30 hadi elfu 50 kulingana na hali ya vichanga hivyo.

Kutokana na hali hiyo, inaibua maswali na tafakari inayohitaji majawabu ya kina, mfano kwa hali hiyo inapelekea Taifa kukosa ng'ombe wangapi kwa mwaka mzima?, maana vyanzo mbalimbali kutoka kwenye machinjio vinaeleza kuwa hali hiyo imekuwa ni endelevu, sio suala la siku moja.

Lakini pia napata wasiwasi juu ya usimamizi pamoja na uendeshaji wa masoko na biashara ya mifugo unaoratibiwa kupitia mwongozo unaotambulika kama (Mwongozo wa masoko ya mifugo wa mwaka 2012), ambapo muongozo huo umebaunisha wazi kuwa ng'ombe wenye mimba hawatakiwi kuuzwa kwa ajili ya kuchinjwa.

Kwa kunukuu sehemu ya muongozo huo inaelezwa kuwa Mpanga madaraja ya mifugo kwenye mnada "Kwa kushirikiana na Mkuu wa Mnada kuzuia mifugo yote ya daraja la chini(Daraja la tatu na la nne) na wenye mimba wasiuzwe kwa nia ya kuchinja"

Napata mashaka juu ya uwajibikaji wa wasimamizi wa muongozo huo pamoja na taratibu nyingine. Kwa hali ilivyo kuna viashiria vya rushwa au uzembe kwa wakaguzi na wasimamizi kuanzia ngazi za masoko hadi kwenye machinjio husika.

Hivyo ili kubaini changamoto hiyo na mnyororo mzima wa wahusika ni vyema mamlaka zikachunguza suala hilo kwa kina ili kubaini wahusika na kuwawajibisha kisheria kwa sababu wanachangia Taifa kukosa rasilimali muhimu ambazo mbeleni zingeweza kuleta tija zaidi.

Kuacha hali hii iendelee ni kujiandaa na kesho yenye uhaba wa nyama au gharama kuwa juu zaidi kutokana na kukosa ng'ombe wa kutosha, mfano andiko hili linabainisha hali hii kwenye machinjio ya Vingunguti pekee, je hali ipoje kwenye machinjio na maeneo mengine nchini?

Huenda tunapoteza rasilimali nyingi ambazo tutashindwa kunufaika nazo mbeleni kutokana na uzembe unaofanywa na baadhi ya watendaji waliopewa dhamana kwa kutanguliza maslahi yao au kushindwa kuwajibika ipasavyo.

Pia, soma;
 
Ng'ombe wapimwe mimba kabla ya kuuzwa minadani...

ikionekana umenunua mjamzito faini laki moja.
Ng'ombe ni Wengi sana Wengi sana Wengi sana yaan usichukulie poa Ng'ombe ni Wengi sana ukiona wanauzwa mpaka wenye Mimba jua kuna Ng'ombe Wengi sana wenye Mimba sasa unataka wapelekee Wapi na Ng'ombe wote Wana Mimba na Tajiri anataka Pesa kwanini asiuze?
 
Asante sana
 
Back
Top Bottom