DOKEZO Mamlaka ziko wapi? Machinjio ya Vingunguti karibia ng'ombe 100 wanapotea kila siku kwa uzembe wa kuchinja ng'ombe wenye mimba

DOKEZO Mamlaka ziko wapi? Machinjio ya Vingunguti karibia ng'ombe 100 wanapotea kila siku kwa uzembe wa kuchinja ng'ombe wenye mimba

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Unakuta waziri wa mifugo haelewi chochote hapa. Amekaa zake ofisini tu anasubiri burungutu la mshahara. Hata kwenye social media hayupo
 
Ng'ombe wapimwe mimba kabla ya kuuzwa minadani...

ikionekana umenunua mjamzito faini laki moja.
Inawezekana lakini si rahisi kuna rushwa minadani asikuambie mtu
Ujue kwanza mfugo yoyote mpk atoke mnadani anatakiwa Dr.wa mifugo athibitishe kwa mhuri na sahihi,lakini kinachofanyika ni kuweka sahihi ,kulipa permit na ushuru baasi ukaguzi big noo wao wanaangalia maokoto tu

Mimi hua naumia mnooo yaani mtu analeta mnadani mbuzi,kondoo au ng'ombe ina mimba kuubwa na maafisa mifugo wapo na hawafanyi lolote lile
Hii nchi kila sehemu ni hovyo tu.
 
Sidhani km mfugaji atauza ng'ombe wake mwenye mimba coz ni hasara kwake!!
Itokee mimba labda ilikuwa changa sana na mfugaji hakujua au ilipatikana huko safarini!!
Nani kasema tuulizie sie tulioko hukooo
Mtu analeta mfugo una mimba ukimuuliza anakuambia nna shida na hii ndo mali yangu nauza
Shida ni viongozi wa minada wapo kwa kupokea tu kodi ba rushwa zao,hilo jambo ni gumu sana kutekelezeka kwa nchi hii
 
Mwenye kosa ni nani kati ya mfugaji na mnunuzi?
Wote wana makosa ila mnadani kuna viongozi na kisheria mfugo mwenye mimba au mgonjwa hatakiwi kuuzwa ila wanauza kila siku ,afisa mifugo,Dr.wa mifugo wajibu wao kukagua mfugo ila hawakagui wao wanahesabu tu idadi na kuchukua pesa baasi
 
Back
Top Bottom