saidoo25
JF-Expert Member
- Jul 4, 2022
- 624
- 1,456
Wakati anaapishwa kuwa Waziri wa Nishati, Januari Makamba aliapa kuilinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyowekwa kwa mujibu wa sheria.
Pia wakati anakula kiapo cha Maadili ya Viongozi wa Umma aliapa kutotumia cheo chake kutoa upendeleo kwa ndugu yake au rafiki yake kwenye kazi za umma sasa hiki anachokifanya cha kugawa mitungi ya Kampuni moja ya Taifa Gas je mamlaka zinazosimamia viapo vya viongozi ziko wapi.
Na kama jambo hili ni jema na halina hila yoyote ndani yake kwanini lisingetangazwa kwa uwazi ili Kampuni zote zinazouza gesi zishiriki mpango huo mzuri wa Serikali.
Makamba haoni kuitangaza kampuni moja pekee kwa kutumia ofisi ya Umma katika mikoa ya Kanda ya Ziwa kunaweza kuwahariba biashara kampuni zingine zinazouza gesi maana wananchi wetu wanaweza kudhani hiyo ndio kampuni yenye ubora iliyopitishwa na Serikali.