Mshangazi mdogomdogo
Member
- Sep 23, 2024
- 73
- 73
Sisi Wafanyabiashara wa Soko la Mfaranyaki lililopo Mtaa wa Mbalika, Kata ya Mfaranyaki tuna changamoto ya mazingira kwenye eneo letu la kazi hilo, uchafu umekuwa ukitawala katika mitaro iliyojaa maji machafu.
Hali hiyo imekuwa ya muda mrefu kutokana na kupasuka kwa mabomba ya maji taka, na sasa maji hayo yamekuwa yakinuka vibaya, hali inayohatarisha afya zetu na kuna uwezekano wa kuwa na hatari ya mlipuko wa magonjwa.
Taka ambazo zinatupwa zimechangia kuziba kwa baadhi ya mifereji, kinachoshangaza ni kuwa sisi tunalipa malipo mbalimbali lakini mbona Viongozi wetu hawashughulikii changamoto kama hizo ambazo ni hatari kwa afya?